Tetesi: Prof. Lipumba awafukuza kazi wakurugenzi wote wa CUF

Tetesi: Prof. Lipumba awafukuza kazi wakurugenzi wote wa CUF

Status
Not open for further replies.
Kwa mwendo huu makao makuu yanaweza hamishiwa Zenji, sidhani kama CUF ya Maalim unaweza tena pata support au kuwarudisha wafuasi wengi watakao wapoteza baada ya hii dhoruba.

Lakini kitu kikubwa zaidi ni impact ya huu mgogoro kwa CDM 2020, kuna wabunge wengi wa UKAWA watadondoka kwa sababu ya huu mgogoro. Ni wazi majimbo ya Dar na Tanga yatarudi CCM kama hakutakuwa na UKAWA. CDM wanafikiria kuhusu umeya wa kesho kutwa ambao hata kama UKAWA ikivunjika bado wanaweza kuwa confront madiwani wachache tu wa CUF na kushinda badala yake inabidi waanze kufikiria 2020. Hiyo ni kete dume imerushwa na CCCM.


Wanapaswa kuzungumza nae.....
kama ana wafuasi hadi wabunge kugombana nae hadi mpoteze wabunge sio akili wala busara
 
ukawa jinamizi la lowasa linawatesa ni ukweli japokuwa ngumu kumesa...kama namuona padri slaa alivyo kimyaaaa....wapi mnyiikaaa....dah bongo politics bora ninywe lite zangu tuuu
 
Lipumba Anafanya Alicho Ambiwa Kufanya na Waliomtuma,ila Yatakwisha Haya!
Na Hapa Ndipo Ninapo Wapendea CHADEMA!
Chama Kikiongozwa na Wasomi Wengi na Kuwa Wanachama Wengi Waliopitia Shule,Ujinga Kama Huu Hauwezi Kuwepo!
Ashakum Si Matusi:
Kuna Muda Huwa Nawaza Kuwa Matatizo Mengi Yanayoikumba CUF,Kiundani Ukichunguza Utangudua Kuwa Inachangizwa na Uelewa Mdogo wa Wanachama Wake!
Mathalani,ni Kweli Lipumba Alijiuzuru na Kuwakimbia UKAWA Katikati ya Mapigano Makali,na Barua Yake Haikujibiwa,na Ana Haki ya Kurudi Maana Mkutano Mkuu wa Chama Haukufanya Maamuzi ya Kura ya Aidha Kumrudisha au La!
Lakini,Chakushangaza,Japo Aliwakimbia Wana CUF Wakati wa Vita,Lakini Bado Kuna Wafuasi Wanamkubali!
Quite Strange!
 
Pambano linaweza kuvunjika. ..lakini likirudiwa ushindi unaweza kubaki pale pale. ...kwa usiyempenda
 
Watu wengi wanapenda kufanya mambo kihisia tu
hawataki kutazama reality....Lipumba hata kama kanunuliwa na CCM..
akiweza kuwa na wafuasi tu basi ni tatizo
siasa ni watu na sio sheria...
BANG! Ulichosema ni ukweli mtupu! Lakini hapa niweke unafiki pembeni! Maalim Seif hayupo interested kabisa na siasa za Tanzania-- zake yeye ni za Zanzibar! Kutokana na hilo, Maalim Seif anahitaji mtu wa kumsaidia kumvuta Mwanasesele Tanzania! Good enough, amempata CHADEMA kupitia UKAWA ambao (Seif) anaamini watakuwa wanavuta mkono wa kuume (Tanganyika) wa Mwanasesele huku akina Seif wakivuta mkono wa kushoto (Zanzibar) wa Mwanasesele!! Kutokana na msimamo ambao alionesha Lipumba dhidi ya Lowassa; Maalim Seif anafahamu ujio wa Lipumba utadhohofisha ushirikiano wa kumvuta Mwanasesele mikono! Kama isingekuwa hivyo, hizi sinema wala zisingewepo hivi sasa!!
 
Yaani juhudi zote Maalim na washirika wake wote wamesanda kwa akili kubwa Mnyamwezi wa Tabora kawachoresha chini amerudia kukalia kiti chake, Professor siyo elimu ya mchezo mchezo mjue kawapiga chali Maalim na Misukule yote ya Ufipa
Mkuu umesahau kutaja na matumizi ya risasi
 
duh, inabidi watafute njia ya kudeal na huyu jamaa kabla hajaleta further damage
Cause hali ikiendelea hivi, chama kinaonekana kiko on the edge ya kuparanganyika
Ila this prof should REALLY be ASHAMED of himself kwa huu ujinga anaofanya na kukubali kupelekeshwa kuharibu/dhoofisha chama ambacho amekuwa nacho na kukitumikia for years.

Kulikuwa na umuhim gani lowasa kuja wakati katika vyama vyao ukawa walikuwa wanafanya maamuzi yao kwa vikao ,na uchaguzi wa serikali za mitaa walifanya vizuri tu bila huyo nyangema
 
Huo ni uenyekiti wa chama tu..tena chama chenyewe ushawishi wake ni mdogo sana katika Tanzania...

Hivi huyu mtu angepewa urais "angebanduka" pale magogoni kweli??..angeyashinda majaribu ya raha za ving'ora huyu mtu???

Tunaendelea kupewa funzo..kama kuna wanaomtumia ajue kabisa wanammaliza na wataitumia hii tamaa yake kuaminisha umma kuwa hafai kabisa kupewa uongozi wa nchi..

Huyu hata ukimpa uwaziri hatobanduka ofisini hata kama baraza likivunjwa!!
 
Hichi ndio chama kinachotaka kukabidhiwa nchi?? Kinaendeshwa kivituko hata kufata katiba yake yenyewe nshida? Mwenyekiti anajiuzulu anakula vyake na kujirudisha anavyojiskia!!! Asante Jecha...
 
BANG! Ulichosema ni ukweli mtupu! Lakini hapa niweke unafiki pembeni! Maalim Seif hayupo interested kabisa na siasa za Tanzania-- zake yeye ni za Zanzibar! Kutokana na hilo, Maalim Seif anahitaji mtu wa kumsaidia kumvuta Mwanasesele Tanzania! Good enough, amempata CHADEMA kupitia UKAWA ambao (Seif) anaamini watakuwa wanavuta mkono wa kuume (Tanganyika) wa Mwanasesele huku akina Seif wakivuta mkono wa kushoto (Zanzibar) wa Mwanasesele!! Kutokana na msimamo ambao alionesha Lipumba dhidi ya Lowassa; Maalim Seif anafahamu ujio wa Lipumba utadhohofisha ushirikiano wa kumvuta Mwanasesele mikono! Kama isingekuwa hivyo, hizi sinema wala zisingewepo hivi sasa!!


Siasa za Tanzania zina mengi sana
Lipumba kabla hajajiuzulu aliwahi kutaka kujiuzulu zamani
sababu ni Seif kuwaburuza wana CUF wa bara
na wana CUF wa bara wanalijua hilo
alianza kupata 'die hard fans' kwa hilo..kitendo cha juzi Seif kumchagua
Mtatiro kimezidisha tatizo......wao hawataki 'mwenyekiti kibaraka'
na Seif kafanya exactly wasichotaka.....na sasa kila kitu kinaamuliwa Zanzibar...

Hili la kusema Lowassa ndo sababu nil la juu juu sana...
Hawa wafuasi wa Lipumba wana mengi sana...ndo maana huu mgogoro unazidi kuwa mkubwa....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom