Tetesi: Prof. Lipumba kuhamia ACT Wazalendo muda wowote

Tetesi: Prof. Lipumba kuhamia ACT Wazalendo muda wowote

Status
Not open for further replies.
Tatzo liko wapi? Kama Lowassa yule, yule aliyeitwa majina yote mabaya na CDM alihamia CDM na ndani ya siku chache akateuliwa kupeperusha Bendera ya CDM kuna ubaya gani Prof. Kuhama CUF kama hajaridhika na maamuzi kama ilivyokuwa kwa Lowassa.
Anyway, hw sure are you that Lowassa's move to CDM wasn't a decoy? Au unaongea tu baada ya kura maharage cjui ya wapi!
Hili BAVOCHA hawalioni,si unajua akili za nyumbuzzzzz,akielekea mmoja wote wanafuata.
Sijui wanaliona jipya lipi hapo,acha waendelee kujifariji,lakini Kiama cha UKAWA na Kaburi lake ni 2020.Watajua tu muda ukifika
 
Pamoja na kwamba watu wanamsema sana Prof, lakini mimi ni mmoja kati ya wale wanaoamini kwamba Prof bado ana mchango mkubwa sana kwa vyama vya upinzani. Ni kweli kabisa kwamba nisingemshauri ajribu tena kurudi CUF kwa sababu siamini kama anaweza kuwa na mvuto tena huko. Lakini generally, hata baada ya kujiuzulu wadhifa wake amebakia kuwa true to himself.... Hajawahi kupanda majukwaani kuwatukana wapinzani wenzake kama alivyofanya yule mwanasiasa mwingine.... Bado namsifia Prof kwa hilo na hasa ukizingatia kwa namna nchi yetu tunavyoendesha siasa za ovyo ambapo kila anayehama chama chake hushawishiwa na kutumiwa kuanza kuvuruga chama chake cha zamani.
 
Nimecheka sana,ingawa ukishaingia kwenye siasa inakupasa uvuwe weredi na kubaki kusikiliza wakubwa wako wanasemaje.

Kiujumla TZ hakuna vyama vya siasa bali kuna magenge ya watu wanaotumia siasa kunufaisha matumbo yao.
Upo sahihi!Wapinzani wa TZ ni hovyo hovyo sana ndiyo yale yale ya akina Mbowe tuandamane sisi na kuwekwa mahabusu lkn wakipata nafasi za uteuzi wanawapa hadi mahawala wao bila kujali mawazo yetu

CCM itatawala milele kwa aina hii ya upinzani
 
Vyama vya upinzani viko vochache sana vinavyotetea na kupigania haki ya mtanzania maskini, halikadhalika viongozi wa upinzani wa KWELI wapo wachache, wengi wao ni wanafiki na wanakatisha tamaa wananchi wapenda mabadiliko ya kweli.. Hii ni moja ya maeneo ambayo CCM lazima itambe kwamba inaweza kutawala inavyotaka.
 
Si jambo la ajabu sana kwenda huko maana wote kiitikadi (Zitto na Lipumba) ni sawa. Sale outs. Hakuna jipya. Kwa wasiolewa watashangalia lakini hii ni political strategy ya CCM kucheza na akili za watu. Ni dhahiri kuwa ACT ni CCM B na kipindi cha uchaguzi kina Slaa walipokuwa wanakaa Serena kwa siri na Lipumba kwenda vacation Rwanda halafu States sasa ni wakati wa kutumikia ruzuku waliozokula. Hamjiulizi Lipumba alikuwa wapi siku zote toka alipojiuzulu asidai ueneyekiti wake tena mpaka juzi na baada ya kuja tu CUF imesambaratika. Alikuwa kwenye mission kaitimiza.

Dhamira hapa ni kudhoofisha upinzani. Kitakochofuata Slaa nae atajiunga ACT na wale wachumia tumbo wa upinzani wote watakwenda huko pia kujifanya wanapigania nchi.

CUF tayari kuna mtafuruku ambao Lipumba ana mkono wake, CHADEMA napo hakukaliki kina Lema na Lissu kutwa wapo lupango, mwenyekiti anadhoofishwa kiuchumi, muda si mrefu watakuwa chali. Hapo sasa ACT wataonekana ndio tegemezi la wanyonge while in reality ni decoy tu.

Come 2020 aidha Lipumba ama Slaa atasimama kugombea urais ambapo in reality itakuwa ni CCM A versus CCM B na mshindi mnajua atakuwa nani. Na hii ndio Tanzania yetu ya kidemokrasia na amani tele............................
Mkuu umeona mbali sana
 
Ninachokiona hapa kama sio tetesi utakuwa uamuzi wa kawaida kwa Siasa za tz ni vigumu kwa chama cha Siasa cha upinzani kuwa na nguvu kwa chaguzi nyingi kama chadema walivyofanya,

hivyo kama lipumba ataongeza nguvu act kutakuwa na nguvu kubwa hivyo kuna uwezekano mkubwa act ikachukua nafasi ya Cdm kuwa chama kikuu cha upinzani
Haitakuwa ajabu kwani CUF walichukua nafasi ya NCCR na baadaye CDM wakachukua nafasi ya CUF hivyo haitakuwa ajabu kwa ACT kuchukua nafasi ya CDM.

Msinishambulie sana ni maoni yangu tu.
Yaheshimiwe.
 
Asante kwa taarifa na kwa kuthibitisha mahaba yako kwa mzee!
Pili angalia ulichoandika mwanzo hukuzungumzia issue za asset au liability bro! Unahoji kwani Prof. Lazima awe kiongoz? Na mm nauliza kwani ilikuwa lazima Mzee agombee yeye? Swala la whether he was an asset or liability alishalijibu siku nyingi Dr.Slaa( siku hizi mnamuita Dr.Mihogo).
Anyway, namimi nikuibie siri na usiwambie wanaCDM, hata mwaka 2010 alishinda Dr.Slaa ila hakutangazwa sisi wana CDM ikabidi tumuite tu Rais wa mioyo yetu.

Ila baadae tukafanya kituko kimoja, 2015 tukamtosa Slaa aliyemushinda a serving president 2010 na tukamchagua Fisadi aliyekubuhu( kwa mjibu wa wana CDM) kugombea urais akiwa na siku tatu ndani ya chama ili apambane na mgeni Magufuli! Usiwambie maana hii ni record na tulistahili kuingia kwenye kile kitabu maarufu ya historia duniani!
Hili nalo usiwambie, pamoja na kushinda uchaguzi wa mwaka huu, na tayari ss tunamuita Rais wa mioyo yetu 2020 hatutampa nafasi ya kugombea kupitia CDM!

Tafadhali usiwambie wenyewe! Hii siri anajua Mbowe tu, kama alivyoijua ile ya Mzee kujiandaa kugombea kupitia CDM!
Bro, Pasco usiniambie uliweza kumjua mgombea wa CCM kabla ya mchakato wa Dodoma ila hukumjua mgombea wa CDM kabla ya mchakato wa Ufipa, hapa utakuwa umeniangusha
!
Sidhani kama Pasco anaweza kujibu nondo hii
 
Vyovyote Itavyokuwa sawa tuu,sisi wafuata upepo tuko tayari kuwasupport kwa shangwe,mori na mahaba!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom