Tetesi: Prof. Lipumba kuhamia ACT Wazalendo muda wowote

Tetesi: Prof. Lipumba kuhamia ACT Wazalendo muda wowote

Status
Not open for further replies.
[HASHTAG]#Lipumba[/HASHTAG] akaungane na wasaliti wenzake huko ACT ndoto za kuendelea kuitwa Mwenyekiti sasa zitatimia.
Pongezi sana kwa uongozi wote wa CUF chini ya Mwenyekiti wao Mtatiro kijana msomi anayejitambua kwa kuwa msimamo kuhusu huyu mchumia tumbo.
 
Ninachokiona hapa kama sio tetesi utakuwa uamuzi wa kawaida kwa Siasa za tz ni vigumu kwa chama cha Siasa cha upinzani kuwa na nguvu kwa chaguzi nyingi kama chadema walivyofanya,

hivyo kama lipumba ataongeza nguvu act kutakuwa na nguvu kubwa hivyo kuna uwezekano mkubwa act ikachukua nafasi ya Cdm kuwa chama kikuu cha upinzani
Haitakuwa ajabu kwani CUF walichukua nafasi ya NCCR na baadaye CDM wakachukua nafasi ya CUF hivyo haitakuwa ajabu kwa ACT kuchukua nafasi ya CDM.

Msinishambulie sana ni maoni yangu tu.
Yaheshimiwe.
Uko sahihi

Usiogope kushambuliwa na mtu aliye na upande, kwani mashambulizi hayataakisi hali halisi na yatabase kwenye ushabiki.

Kwa sasa wanaomshambulia Lipumba hawana hoja, kwani wanayomsemea Lipumba nao waliyafanya na wanaendelea kuyafanya.

Hawana moral authority ya kumkemea prof
 
Huyu Prof. Ni professor wa kitu gani hivi??? Mbona hafanani na uprofessor?? au ni kama wa maji marefu???
Aliondoka CUF kwa hiari tena kwa kukikashfu chama, sasa anatangaza tena kuwa yeye ni mwenyekiti, kagombea lini tena?
Kutumika kubaya, sasa anaaibika!
 
Crl7dwuXgAAZCBH.jpg
Kutokana na uvumi unaendelea kuzagaa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo na mitandao yakijamii kwamba ACT wazelendo wapo kwenye kikao cha ndani wakijadili kumpokea prof Lipumba,ZZK amekanusha habari hizo.

Hapa chini ni nukuu ya kile alichokiandika Zitto kupitia account yake ya twitta.

"Kikao cha Kamati kuu ya Chama kinaendelea. Narudia - hakuna ajenda ya kumpokea Kiongozi yeyote wa chama kingine".

Hayo ndio maneno ya yake kwa msingi huo taarifa hizi si za kweli.
 
Wanafalsafa mmoja wa India aliwahi kusema:
"When Education Failed to Enter a MIND and HEART and Change The Way Of THINK and ANALYSE Things Objectively, Then That Education Has No Different With A Shirt/Underwear Worn In The Morning and Taken Off in Evening"

Pia huwa wanasema "Old Age Comes With WISDOM" but huyu Mzee Lipumba proves that there is a time, Old Age Comes Alone

Kikubwa zaidi hii ndiyo true reflection ya wasomi wetu wengi na elimu ya nchi hii ilipotufikisha. Wengi walikuwa wanasoma kwa kutafuta Titles and kuwa na vyeti vingi, elimu yao imeshindwa kabisa kubadili uwezo wao wa kufikiri na kufanya maamuzi yenye busara.

Ni urithi au mfano gani? anaouachia kizazi hiki cha sasa?

Huko Tunakoenda ni hatari zaidi kama hawa ndiy tumekubali wawe viongozi wetu wa sasa tukitegemea watujenge misingi ya uongozi na utawala bora wa baadae.
 
Si Lipumba anatoka CUF kwenda Act Wasaliti?
 
Lakini si vikao vya ndani na nje vya vyama vya siasa vimepigwa marufuku? Au ACT wana kibali maalumu?
 
Sasa anaogopa nini wakati wao wote wanafanana

Lipumba Msaliti

zitto Msaliti

ACT---Chama cha wasaliti
 
Zito hawei mpisha,,,next election ana timiza 40+ atataka kugombea urais.
Zito awezi kugombea urais hiyo nafasi ni lipumba kwa sababu anajua awezi shinda ili wawe Na mgombea wa kudumu lazima wawe Na lipumba kama kitilya alivyokataa kugombea kwa kuwa akuwa Na maslai Na zito hivyo hivyo zito ataendelee kugombea ubunge tu maana awana uhakika Na mbunge mwingine
 
Upo sahihi!Wapinzani wa TZ ni hovyo hovyo sana ndiyo yale yale ya akina Mbowe tuandamane sisi na kuwekwa mahabusu lkn wakipata nafasi za uteuzi wanawapa hadi mahawala wao bila kujali mawazo yetu

CCM itatawala milele kwa aina hii ya upinzani
Mkuu kiujumla Tanzania hakuna upinzani unao jitambua.Huwezi kucheza kamali katika siasa,kamali inachezwa mpirani tu.Wapinzani mpaka sasa wanabanwa sana na mtukufu na huku wanagawanyika pia.

Kuondoka kwa Lipumba Cuf ndio kuondoka kwa Cuf Tanganyika.Jalibu tu kufanya tathmini ya haraka nguvu lipumba aliyonayo mikoa ya pwani,na pia angalia watu walioukuwa wanamsapoti liprofeseli kama Magdalena Sakaya na Kambaya hawa wote ndio walioukuwa wanategemewa na Cuf.

Tujiandae tu kuona Chadema ikitafuta Muunganiko na ACT ili kutotawanya kura za wale jamaa wa mikoa ya pwani.Chadema na Ukawa kiujumla kamali waliyocheza yakumpokea Edo itawaghalimu sana,labda uongozi wote wajuu ujiuzuru upishe watu wapya.

CCM ni genge hatari sana kwa uchumi wa nchi yetu lakini upinzani wenyewe huu wakina Edo,Sumaye,Lipumba kamwe hautoweza kuwaondoa CCM madarakani.Vyama tu vihangaike kuongeza ruzuku.
 
Hakika hata kama watu wapige vijembe kiasi gani ila ukweli ni kwamba Lipumba ataongeza nguvu ACT kwa kiasi kikubwa sana.
Muda utasema, acha tusubiri ataongeza nguvu gani ACT! Mtu aliyekuwa mwenyekiti wa CUF kwa miaka karibu 20 na mkashuhudia CUF ikipotea bara hadi kuzimia kama si kufa leo atarajiwe kufanya mabadiliko tena baada ya kusaliti chama chake cha zamani hawezi kufanya tofauti zaidi ya kuleta mfarakano pia huko atakakowenda.
 
Mkuu kiujumla Tanzania hakuna upinzani unao jitambua.Huwezi kucheza kamali katika siasa,kamali inachezwa mpirani tu.Wapinzani mpaka sasa wanabanwa sana na mtukufu na huku wanagawanyika pia.

Kuondoka kwa Lipumba Cuf ndio kuondoka kwa Cuf Tanganyika.Jalibu tu kufanya tathmini ya haraka nguvu lipumba aliyonayo mikoa ya pwani,na pia angalia watu walioukuwa wanamsapoti liprofeseli kama Magdalena Sakaya na Kambaya hawa wote ndio walioukuwa wanategemewa na Cuf.

Tujiandae tu kuona Chadema ikitafuta Muunganiko na ACT ili kutotawanya kura za wale jamaa wa mikoa ya pwani.Chadema na Ukawa kiujumla kamali waliyocheza yakumpokea Edo itawaghalimu sana,labda uongozi wote wajuu ujiuzuru upishe watu wapya.

CCM ni genge hatari sana kwa uchumi wa nchi yetu lakini upinzani wenyewe huu wakina Edo,Sumaye,Lipumba kamwe hautoweza kuwaondoa CCM madarakani.Vyama tu vihangaike kuongeza ruzuku.
Lkn Lipumba alijiondoa CUF mwaka jana na CUF wakaongeza viti vya Ubunge huku bara!
 
Vikao vya ndani si vimekatazwa au?
Ndege wafananao huruka pamoja.
 
View attachment 394136 Kutokana na uvumi unaendelea kuzagaa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo na mitandao yakijamii kwamba ACT wazelendo wapo kwenye kikao cha ndani wakijadili kumpokea prof Lipumba,ZZK amekanusha habari hizo.

Hapa chini ni nukuu ya kile alichokiandika Zitto kupitia account yake ya twitta.

"Kikao cha Kamati kuu ya Chama kinaendelea. Narudia - hakuna ajenda ya kumpokea Kiongozi yeyote wa chama kingine".

Hayo ndio maneno ya yake kwa msingi huo taarifa hizi si za kweli.
Thread closed
 
Zito awezi kugombea urais hiyo nafasi ni lipumba kwa sababu anajua awezi shinda ili wawe Na mgombea wa kudumu lazima wawe Na lipumba kama kitilya alivyokataa kugombea kwa kuwa akuwa Na maslai Na zito hivyo hivyo zito ataendelee kugombea ubunge tu maana awana uhakika Na mbunge mwingine
Lowassa nae ni mgombea wa kudumu CDM.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom