Tetesi: Prof. Lipumba kuhamia ACT Wazalendo muda wowote

Status
Not open for further replies.
Hili BAVOCHA hawalioni,si unajua akili za nyumbuzzzzz,akielekea mmoja wote wanafuata.
Sijui wanaliona jipya lipi hapo,acha waendelee kujifariji,lakini Kiama cha UKAWA na Kaburi lake ni 2020.Watajua tu muda ukifika
 
Pamoja na kwamba watu wanamsema sana Prof, lakini mimi ni mmoja kati ya wale wanaoamini kwamba Prof bado ana mchango mkubwa sana kwa vyama vya upinzani. Ni kweli kabisa kwamba nisingemshauri ajribu tena kurudi CUF kwa sababu siamini kama anaweza kuwa na mvuto tena huko. Lakini generally, hata baada ya kujiuzulu wadhifa wake amebakia kuwa true to himself.... Hajawahi kupanda majukwaani kuwatukana wapinzani wenzake kama alivyofanya yule mwanasiasa mwingine.... Bado namsifia Prof kwa hilo na hasa ukizingatia kwa namna nchi yetu tunavyoendesha siasa za ovyo ambapo kila anayehama chama chake hushawishiwa na kutumiwa kuanza kuvuruga chama chake cha zamani.
 
Nimecheka sana,ingawa ukishaingia kwenye siasa inakupasa uvuwe weredi na kubaki kusikiliza wakubwa wako wanasemaje.

Kiujumla TZ hakuna vyama vya siasa bali kuna magenge ya watu wanaotumia siasa kunufaisha matumbo yao.
Upo sahihi!Wapinzani wa TZ ni hovyo hovyo sana ndiyo yale yale ya akina Mbowe tuandamane sisi na kuwekwa mahabusu lkn wakipata nafasi za uteuzi wanawapa hadi mahawala wao bila kujali mawazo yetu

CCM itatawala milele kwa aina hii ya upinzani
 
Vyama vya upinzani viko vochache sana vinavyotetea na kupigania haki ya mtanzania maskini, halikadhalika viongozi wa upinzani wa KWELI wapo wachache, wengi wao ni wanafiki na wanakatisha tamaa wananchi wapenda mabadiliko ya kweli.. Hii ni moja ya maeneo ambayo CCM lazima itambe kwamba inaweza kutawala inavyotaka.
 
Mkuu umeona mbali sana
 
Ninachokiona hapa kama sio tetesi utakuwa uamuzi wa kawaida kwa Siasa za tz ni vigumu kwa chama cha Siasa cha upinzani kuwa na nguvu kwa chaguzi nyingi kama chadema walivyofanya,

hivyo kama lipumba ataongeza nguvu act kutakuwa na nguvu kubwa hivyo kuna uwezekano mkubwa act ikachukua nafasi ya Cdm kuwa chama kikuu cha upinzani
Haitakuwa ajabu kwani CUF walichukua nafasi ya NCCR na baadaye CDM wakachukua nafasi ya CUF hivyo haitakuwa ajabu kwa ACT kuchukua nafasi ya CDM.

Msinishambulie sana ni maoni yangu tu.
Yaheshimiwe.
 
Sidhani kama Pasco anaweza kujibu nondo hii
 
Vyovyote Itavyokuwa sawa tuu,sisi wafuata upepo tuko tayari kuwasupport kwa shangwe,mori na mahaba!!!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…