TANZIA Prof. Mathew Luhanga, aliyekuwa Makamu Mkuu wa UDSM kuanzia 1991 hadi 2006 afariki dunia

Kati ya hao wawili nani alikuwa anabaniwa? Maana Dr David Mfinanga tunamfahamu vizuri sana. He is exceptional!!
 
Tulianza kumuita profesa mwanzoni mwa miaka ya sitini tukiwa naye N. A. Middle School Mbeya, alikuwa Time Keeper wa shule ni mdogo wake Elijah B. Luhanga aliyewahi kuwa mkurugenzi wa Tanesco.
MUNGU AWE NAYE DAIMA.
 
 
Prof. Luhanga akiwa VC iliishauri serikali itilie mkazo sana kwenye elimu ya chekechea na msingi badala ya sekondari, kufeli kwetu kwenye elimu kunatokana na wanafunzi kuanza kujifunza kusoma, kuhesabu na kuandika wakiwa sekondari tofauti na enzi za mkoloni. Alitoa ushauri huo wakati huo baada ya kuona kiwango cha elimu ya wanafunzi wanaoingia chuo kikuu hairidhishi.
 
Mpumzike kwa amani pamoja na msaidizi wako Prof. Mayunga Nkunya. Daima nitawakumbuka kwa ile hotuba yenu tamu na iliyo tukuka siku ya kutukaribisha First Year 2005!

Nakumbuka sana siku ile mlituusia kitu hiki "Graduate with A's and not with AIDS" Huu msemo ulikua ni mpya kabisa kwangu ukichukulia nilikua nimetokea kijijini, halafu moja kwa moja mpaka Udsm!
 
Nakumbuka siku moja tukiwa Mlimani UDSM, nilimsikia akisema alikuwa ana mheshimu Prof. Mark James Mwandosya tu!!!

R.I.P Prof. Mathew Luhanga!
Hata mm nilikuwepo siku hyo, alisema huwezi kuwa professor wa kiswahili au development study kisha ukajisifu eti ww ni professor! Nchi hii maprofessor tumebaki wawili tu mm na mwingine hayupo hapa anaitwa mark mwandosya" mbele ya jk na asha rose migiro nafikiri kulikua na uzinduzi wa coet kama kumbukumbu zangu ziko sahihi.
 
Pole Prof. Mark Mwandosya rafiki mkubwa wa marehemu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…