Prof. Mbarawa: Tukipata muwekezaji mahiri bandarini, 67% ya bajeti itatoka bandari ya Dar na kuacha kutembeza bakuli

Kwa hiyo Serikali inakili wazi kushindwa kuleta ufanisi inategemea mtu wa kuja aje awajengee uchumi mzuri watanzania. Tulidai UHURU ili tufanye nini?
Serikali hii ina manufaa gani kwa watanzania?
 
Hata wangekusanya fedha nyingi kiasi gani,hata makusanyo yangetishereza kugharamia bajeti nzima, bado nchi itaendelea kuomba na kukopa tu.

Sehemu kubwa ya makusanyo hayo yataishia kubadirisha magari ya viongozi, kugharamia semina, warsha, workshop, per diem.

Zingine nyingi zitaibwa kwa invoice zenye maneno mengi lakini zitaishia mikononi mwa wezi wa serikalini.
 
Sidhani km kuna bandari duniani popote inachangia 67% ya mapato ya inchi...hizi figures ni km za kilimo cha tikiti maji kwa what'sup.
 
Natamani kauli hiyo angeigeuza na kutamka akiiambia familia yake kama ataeleweka kirahisi.

Yaani aseme hivi, kutokana na Hali ngumu ya maisha anayopitia na familia yake,

Akimpata mwekezaji Kutoka nje ya family, familia itaishi vizuri.

Kauli zingine ni MATUSI ya WAZI, ndomana Kuna mtu alivurumisha viatu kumuekekea kiongozi mmoja aitwaye Bush kwenye press conference.
 
Tuna watu ambao sina hakika kama hizi elimu zao hasa za uprofesa kama zina wasaidia .... au wana waz kwakutumia tumbo ...... mtu mwenye akili timamu hapaswi kuwa ivi ..... au Tuna hujumiwa wazi wazi
 
Sidhani km kuna bandari duniani popote inachangia 67% ya mapato ya inchi...hizi figures ni km za kilimo cha tikiti maji kwa what'sup.
Tatizo la VIONGOZI wa TANGANYIKA wanawaona Wananchi hawana UELEWA wa MAMBO
 
Tanzania ni chi donor - kwa sauti ya marehemu.
 
Mim najiulizaga maswali mengi ivi kuna haja gani ya CAG kutusomea yale makaratasi ilihali hatua yeyote haichukuliwi ...... ninashawishika kusema hata mamlaka ina husika na ubathilifu wa mali za uma .... haiwezekani serikali ikawafumbia macho wezi .....au na yenyewe inahusika kwa namna moja au nyingine ..... KATIBA MPYA , KATIBA MPYA NI LAZMA
 
faida si ndiyo kama hii ya DP World, unafikiri ilianza tu yenyewe? Ilitokana na ripoti za CAG, jisomee:

 
Hiyo DP wold haito saidia chchte tuna mifumo mibovu sana ..... na wew ni miongoni mwa watu wa hovyo cjapata kuona
 
Huo ndio ukweli,
Mwekezaji anakupa robo ya mapato!
Ukifanya mwenyewe mapato yote yanakuwa yako!
 
Hivi anajua maana ya asilimia 67 ya bajeti?. Tatizo tunapigwa maneno ila siku mambo yakiharibika sisi ndio tutaumia, mabarawa hata kuwepo
 
Miaka 60 ya uhuru hatujui hatuna wasomi wa kuendesha bandari alafu tunasema tupo huru
 

Ni mpumbavu asiye na akili. Vita za dunia zimeanzia wapi? Ni nchi gani ya ulaya ndani ya miaka 60 toka wameanza taifa lao wanamaendeleo kama yetu?
 
Huo ni akili za kufikirika za Abdunuwasi .ni sawa na ndo y kummaliza chuo kuwa utakuwa na gari nyumba na mke .ukimaliza ndo utajua haujui
 
Tukipata mwekezaji inamaana wao wenyewe hawajawaamini waarabu 😊😊
 
Acha uzwazwa wewe Tics wamekuwepo miaka mingapi na wameshindwa?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Huyo Mabarawa ni bora akajikita kupambania haki za Fei Toto na sio hayo mambo ya bandari za Tanganyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…