Prof. Mkenda, waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2023 kutoka shule ya msingi moja wote wamehamishiwa sekondari moja

Prof. Mkenda, waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2023 kutoka shule ya msingi moja wote wamehamishiwa sekondari moja

Mimi labda sijaelewa.

Unakuta shule ya msingi A, ina wanafunzi 123 waliomaliza darasa la saba na wamafaulu wote kuingia kidato cha kwanza mwaka 2023.

Cha kushangaza wanafunzi wote wa hiyo shule ya msingi A wamepangiwa shule moja tu ya sekondari iliyopo kwenye hiyo kata kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023.

Sasa kwanini wamehamishwa wote kutoka msingi moja kwenda sekondari moja iliyopo kiji hicho hicho na kata hiyo hiyo?

Kwanini wasingebakia hapo hapo msingi waendelee na kidato cha kwanza kwa shule ya msingi kuongezewa madarasa, walimu na vitendea kazi? Kulikuwa na haja gani kujenga shule jirani ya kuhamishia watoto wale wale , wa kijiji kile kile, kata ile ile?

Kulikua na haja gani kukopa mikopo ya Bank ya Dunia kujenga madarasa mapya kibao shule ya jirani na ilipo shule ya msingi kwa ajili ya kuhamishia hapo watoto?

Je Prof, huoni kuwa mitihani ya darasa la saba unaofanyika kwenda kidato cha kwanza sasa ni ya kufutwa na kuboresha shule za msingi ziwe hadi kidato cha nne?

Huoni sasa ni wakati wa shule za sekondari za kata kugeuzwa kuwa vocational training kwa ajili ya wanaomaliza kidato cha nne na kushindwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano?
Mkuu huu ni mpango mkakati wa CCM kuzalisha vilaza wasioweza kuhoji kitu chochote ili waendelee kubaki madarakani milele kwa maslahi ya matumbo yao mapana yasiyoshiba kamwe!
 
Na wote wapangiwe shule moja so kama ni ujinga na tabia za kijinga wanazihamishia kwenye shule mpya waliyopangiwa
Mkuu hata mimi nimejiuliza swali kama hili hili. Kama labda kuna wanafunzi walikuwa na "wachumba" wao si ndio wamewafungisha ndoa kabisa? Huu ni uamuzi wa kijnga kabisa kuwahi kuamuliwa na kiongozi hapa nchini.
 
The vice versa is true km watakuwa watoto wenye tabia Njema
Na wote wapangiwe shule moja so kama ni ujinga na tabia za kijinga wanazihamishia kwenye shule mpya waliyopangiwa
 
Back
Top Bottom