Prof. Mwandosya ateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA

Aisee!!? Hiv sifa za kuwa mwenyekiti wa hizo bodi huwa ni zipi?
Kwa kweli naona kuna tatizo, hivi mtu kama Prof Mwandosya anaongeza nini kwenye utendaji???? Kwani hakuna vichwa vingine Tanzania? Nadhani tunahitaji katiba mpya. Nafasi kama hizi ni bora wangepewa watu baada ya interview.
 
CcM ni ile ile
 
Hii ndio bongo raia hadi wa awamu ya 3 wanarudi kulamba asali. Vijana hili liwape akili kua ukondoo hautaleta mabadiliko. [emoji23][emoji23][emoji23]

Vijana aina ya makonda, mnyeti, kheri james, sabaya, hepi, hapana bora wazee waendelee kuongoza vijana wengi walipewa nafasi wakawa watu wa hovyo sana
 
Huyu mzee wangemuacha tu apumzike katumika vya kutosha. Hata yeye alisema sasa anarudi kijijini kumalizia uzee wake sasa wamarudisha tena kwenye mbio mbio na kudhalilishana leo umeteuliwa kesho unatenguliwa kama mbwa.
 
1660904949791.png

Rais Samia amemteua Profesa Mark Mwandosya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA).

Prof Mwandosya anachukua nafasi ya Prof Jamidu Yahaya ambaye amemaliza muda wake.

Tukumbuke Prof Mwandosya alitofautiana msimamo na Rais Magufuli katika masuala kadhaa ya kijamii.

Mawili kati ya hayo ni kusikitika hadharani Mbunge wa Mbeya mjini, Mr Mbilinyi aka "Sugu" kufungwa kwa sababu ambazo hazikuwa wazi, na alimtembelea huko lupango.

Pili, ni kuonyesha masikitiko yake alipopigwa risasi Tundu Lissu..

Magufuli alimvua uongozi katika nafasi za Uenyekiti wa Bodi mbili, ile ya Mwalimu Nyerere College-Kigamboni na MUST-Mbeya University od Science and Technology.

Mama kasawazisha.

Viva Mama Samia.
 
View attachment 2328366

Kulikuwa na haja gani kuelezea tofauti zake na Magufuli??

Hivi maana ya kustaafu ni nini hasa katika nchi za ulimwengu wa tatu????

Halafu na wewe mtoa mada uanze kukua. Badala ya kuandika shida wanazopitia Watanzania unasifia tu.
 
Magufuli alimtumbua kwa roho mbaya, mama kamrudisha.
Hilo nalo neno, au huelewi?
 
Nchi ya hovyo na teuzi za hovyo zinazozaa matokeo ya hovyo..........watu Wanataka mpaka mtu afie kwenye kordo za maofisinj ndio wajue kuwa umri umekwenda na anatakiwa kupumzika.....mbona taifa Lina vijana wengi tu wenye elimu na ujuzi wa kutosha kuongoza.....kwanini kila siku ni wao tu.....??
 
Kulikuwa na haja gani kuelezea tofauti zake na Magufuli??

Hivi maana ya kustaafu ni nini hasa katika nchi za ulimwengu wa tatu????

Halafu na wewe mtoa mada uanze kukua. Badala ya kuandika shida wanazopitia Watanzania unasifia tu.
Kuna akina nyie ambao hamkupitia shida wakati wa Magufuli.
Teuzi zote zilikuwa zenu, toka Uwaziri hadi ukuu wa mikoa.
Kilio cha ubaguzi mlikuwa hamioni.
Leo ndio mnagundua kuwa kuna shida za wananchi.
Basi kwa rtaarifa zenu shida zimepungua sana alipoingia Mama Samia.
Ingalau hela tunaiona mitaani.
 
Back
Top Bottom