Prof. Palamagamba Kabudi has admitted on BBC FOCUS ON AFRICA that Azory Gwanda has “disappeared and died”

Prof. Palamagamba Kabudi has admitted on BBC FOCUS ON AFRICA that Azory Gwanda has “disappeared and died”

Amesema kati ya waliokufa mmoja wao ni ndugu Azory
Umesikia hivyo tu?
Itendee haki nafsi yako ndugu mtanzania, upotoshaji hautosaidia taifa hili bali kujaza chuki zisizo sababu..
Ukisha jilisha upepo Wa aina hii kisha unarejeshaje maisha ya hao watu waliopotea na kufa mkiru?
 
Basi lugha inakushinda unasikiliza lakini huelewi basi nakuwekea kwa kwa kiswahili halafu tafuta link
View attachment 1150955
Mimi sipo kumtetea mtu yeyote. Natetea ukweli.

Nimesikiliza clip lakini sijasikia Waziri aliposema khusu kufariki.

Unaweza kutuwekea clip hiyo tumsikie Waziri mwenyewe anaongea kuhusu kufariki?

Jambo hili ni muhimu. Kwa sababu kama Waziri kasema habari za kufariki, tunataka tumbane, amejuaje habari za kwamba mtu aliyepotea amefariki?

Tuwekee clip ya Waziri kusema habari ya kufariki.
 
Heeee. .inapaswa aulizwe maiti yake ilipo na kama walii teketeza ..basi aseme walii teketeza kwa njia zipi. .. Pia atueleze yeye aliyajuaje hayo?
Nimeona BBC FOCUS ON AFRICA amesema Azory Disappeared and Died, nimeumia sana
 
Diplomat wa wapi huyu? Anaongea hovyo hovyo bila kupima maneno, aje kukanusha sasa
 
Nimesoma kichwa cha thread, nikasema kama kapotea, Waziri atajuaje kwamba kafariki?

Nikasema ngoja nisikilize clip nimsikie Waziri.

Nimemsikia Waziri anachemka kama kawaida yake, kakosea jina, anataja Azory Rwanda.

Naona Rwanda imemkaa sana kichwani.

Lakini sijasikia Waziri akisema lolote kuhusu kifo.

Mtoa mada anaweza kutupa uhakikisho kwamba hiyo habari ya kifo kusemwa na Waziri ni ya kweli na si ya kutungwa tu?

Ndugu Kiranga

Palamagamba Kabudi: 'Azory Gwanda alitoweka na kufariki'

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Tanzania Palamagambo Kabudi
Kutoweka kwa mwandishi mpekuzi nchini Tanzania Azory Gwanda hatimaye kumechukua mwelekeo mpya baada ya waziri wa maswala ya kigeni nchini humo kusema kwamba mwandishi huyo 'alitoweka na kufariki'.
Katika mahojiano na BBC katika kipindi cha FOCUS ON AFRICA mjini London waziri Palamagambo Kabudi alinukuliwa akisema kwamba visa vya watu kutoweka vimesababisha uchungu mwingi nchini humo.
''Wacha nikwambie unapozungumzia kuhusu kisa hicho, ni mojawapo ya visa ambavyo vimesababisha uchungu mwingi nchini Tanzania''.

Aliendelea: Katika eneo la Rufiji sio tu Azory Gwanda aliyetoweka na kufariki, nataka kukuhakikishia kwamba tunachukua kila hatua sio tu katika eneo la Rufiji bali pia maeneo mengine ya Tanzania ili kuhakikisha kuwa watu wetu wako salama-sio tu waandishi , bali pia Polisi na raia wa kawaida.
Na baada ya mahojanio hayo wanaharakati wa haki za kibinadamu na raia walisambaza kanda ya video ya mahojiano hayo mitandaoni wakimtaka waziri huyo kuelezea familia ya mwandishi huyo ni wapi mwili wake ulipatikana.
Mwandishi mpekuzi Azory GwandaHaki miliki ya pichaHRW

Wakili maarufu nchini humo Fatma Karume maarufu Shangazi aliandika katika mtandao wake wa twitter: Mungu wangu Palamagamba amekiri katika BBC FOCUS ON AFRICA kwamba Azory alitoweka na kufariki. Je alijuaje kwamba amefariki?
 
Mimi sipo kumtetea mtu yeyote. Natetea ukweli.

Nimesikiliza clip lakini sijasikia Waziri aliposema khusu kufariki.

Unaweza kutuwekea clip hiyo tumsikie Waziri mwenyewe anaongea kuhusu kufariki?

Jambo hili ni muhimu. Kwa sababu kama Waziri kasema habari za kufariki, tunataka tumbane, amejuaje habari za kwamba mtu aliyepotea amefariki?

Tuwekee clip ya Waziri kusema habari ya kufariki.
 
Mimi sipo kumtetea mtu yeyote. Natetea ukweli.

Nimesikiliza clip lakini sijasikia Waziri aliposema khusu kufariki.

Unaweza kutuwekea clip hiyo tumsikie Waziri mwenyewe anaongea kuhusu kufariki?

Jambo hili ni muhimu. Kwa sababu kama Waziri kasema habari za kufariki, tunataka tumbane, amejuaje habari za kwamba mtu aliyepotea amefariki?

Tuwekee clip ya Waziri kusema habari ya kufariki.

Kwamba idhaa ya kiswahili wanamsingizia kabudi? Najaribu kuweka ila nimekuwekea maelezo yake hapo
 
kwenye uzi huu nimejifunza jambo moja kubwa, nalo ni kwamba sisi watanzania wengi tuna tatizo sugu la lugha ya kiingereza kuliko kiswahili hivyo kiingereza kuendelea kutumika as a means of instruction mashuleni na vyuoni tutaendelea kutumia kitu tusichokuwa na uwezo nacho vizuri.

hivyo nina ombi kwa serikali, iharakishe mchakato wa matumizi ya lugha ya kiswahili kama lugha ya kufundishia hapo tutakuwa tumejikomboa kwelikweli
 
Ndugu Kiranga

Palamagamba Kabudi: 'Azory Gwanda alitoweka na kufariki'

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Tanzania Palamagambo Kabudi
Kutoweka kwa mwandishi mpekuzi nchini Tanzania Azory Gwanda hatimaye kumechukua mwelekeo mpya baada ya waziri wa maswala ya kigeni nchini humo kusema kwamba mwandishi huyo 'alitoweka na kufariki'.
Katika mahojiano na BBC katika kipindi cha FOCUS ON AFRICA mjini London waziri Palamagambo Kabudi alinukuliwa akisema kwamba visa vya watu kutoweka vimesababisha uchungu mwingi nchini humo.
''Wacha nikwambie unapozungumzia kuhusu kisa hicho, ni mojawapo ya visa ambavyo vimesababisha uchungu mwingi nchini Tanzania''.

Aliendelea: Katika eneo la Rufiji sio tu Azory Gwanda aliyetoweka na kufariki, nataka kukuhakikishia kwamba tunachukua kila hatua sio tu katika eneo la Rufiji bali pia maeneo mengine ya Tanzania ili kuhakikisha kuwa watu wetu wako salama-sio tu waandishi , bali pia Polisi na raia wa kawaida.
Na baada ya mahojanio hayo wanaharakati wa haki za kibinadamu na raia walisambaza kanda ya video ya mahojiano hayo mitandaoni wakimtaka waziri huyo kuelezea familia ya mwandishi huyo ni wapi mwili wake ulipatikana.
Mwandishi mpekuzi Azory GwandaHaki miliki ya pichaHRW

Wakili maarufu nchini humo Fatma Karume maarufu Shangazi aliandika katika mtandao wake wa twitter: Mungu wangu Palamagamba amekiri katika BBC FOCUS ON AFRICA kwamba Azory alitoweka na kufariki. Je alijuaje kwamba amefariki?
Nimesikia.

For such a highly reputed academician, Kabudi is such a poor speaker.
 
Unajaribu kulazimisha hisia zako ziwe maneno ya MTU mwingine....
Ama hakika taifa lina tatizo kubwa sana kwa watu wazushi aina yenu, na bahati mbaya ni kelele zinazowafuatia wasiojielewa pekee...

Mzushi mimi au walitoa habar? We vipi nimekuwekea waliotoa habar sasa mimi ndo bbc? Angalia post zako yaani unanilenga mimi kama ndio bbc kama wanadanganya kwa nini serikali wasilishtaki shirika la utangazaji la bbc kwamba ni wapotoshaji?
 
Nimemsikiliza mara mbili ili nione kama ni tatizo la grammar lakini bado nasikia .... not the only who disappeared and died. Neno 'and' limeleta tatizo! Sijui ni tatizo gani lakini nadhani binadamu wote tunatakiwa tusijue saaana! Sijui kama ana uhakika huo au ni tatizo la kuonyesha hawezi kushindwa swali na akajikuta anashindwa kuchagua maneno. Kutoonekana huwa siyo uthibitisho wa kifo, hata kama ni ajali ya meli kama MV Bukoba, tusiowaona tunasema kadhaa hawakupatikana. Kwa maneno yake anao ushuhuda wa kifo hiki kweli?

Namuangalia tena usoni; ni ushujaa ajabu. Lakini hii naiona kwa wanasheria wengi wanapokuwa wanahojiwa. Kila wakati wanakuwa tayari ku-counter badala ya kulegeza mambo ili iwape nafasi ya kufikiri. Ni hivyo kwa Lissu, akina Fatuma, Mwakyembe, ... ni tatizo.

Waandishi wa habari pia wana matatizo. Kwa Tanzania wao wanatafuta mwandishi mwenzao tu! Hata kama ni siku ya uhuru wa habari, suala hilo la watu kupotea siyo waandishi tu. Yaani kila taaluma inahangaika kujitetea yeneywe tu na kusahau jamii. Wanasheria nao hawataki wenzao waguswe. Hii inatunyima nafasi ya uungwana!
 
Kwamba idhaa ya kiswahili wanamsingizia kabudi? Najaribu kuweka ila nimekuwekea maelezo yake hapo
The guy is such a poor speaker I am not sure if this is a case of "foot in mouth disease" or a Freudian slip.

In logic "disappeared and died" and "disappeared or died" are two very different things.

It indeed appears that, at least by his words, he is saying that he knows Azory died.

The question now becomes, how does he know this?
 
Back
Top Bottom