Prof Shivji: Barua kwa Rais; Ardhi mali ya nani?

Pascal Mayalla unakubaliana na mkufunzi wako ?
 
Spika wa bunge letu huwa anamsaidia mwanasheria mkuu kutoa tafsiri ya sheria au anaingilia majukumu yake ?
Pascal Mayalla Tindo Nguruvi3 JokaKuu zitto junior Mag3
 
Hujaelewa kilichoandikwa. Leave this discussion to those with human brains!
 
Hii nchi imeharibiwa na siasa, too much lobbying hadi upinzani. Ni ngumu sana kuwa na majadiliano yenye maslahi ya umma watu wasitangulize matumbo yao.

Profesa amesimama na amehesabiwa! Salute Profesa, hii ndio shule yenye manufaa kwa umma na si tumbo lako tu!
 
Kwani unadhani hili halijulikani. Upinzani gani unalaumu hapa? Kama ni hawa kina Zitto na Lipumba basi siyo wapinzani. Wapinzani wa kweli kama Mhe Lissu kila siku analipigia kelele na huu ufafanuzi alishatoa siku nyingi tu. Ila ukishakuwa na corrupt system kama hii aliyoipandikiza Magufuli hakuna anayesikia. Najua system ilikuwa corrupt hata kabla yake lakini yeye alifanya mambo yazidi kuwa magumu kwa kuweka wabunge wa hovyo kama kina Tale kwa nguvu.
 
Shivji alisemaje wakati Nyerere anahamisha watu na kuwapeleka kwenye vijiji vya Ujamaa? Alisemaje pale wengine waliporwa nyumba zao halafu zikataifishwa baada ya Azimio la Arusha? Kama mambo hayo hayakupingwa kisheria, ni sawa na kukubali serikali ndiyo inamiliki ardhi.
 
Ame Professional uchwara huyo! Profesa gani hajui kuwa Loliondo ni Game Controlled area tangu mwaka 1951 na Sheria hiyo haijawai kufutwa
 
Muulize shivji! Loliondo ni Game Controlled Area tangu mwaka 1951 Tanzania ikiwa chini ya ukoloni inakuwaje anadai ni eneo la Wamasai?

Kweli ukizeeka akili inapungua
 
Ahsante Prof
Bwashe huyu Profesa Shivji sasa ameanza kuwa tapeli. Amefundisha kozi ya sheria UD zaidi ya miaka 30 lakini miaka hiyo yote hajawahi kuona mapumgufu hayo hadi leo na kujifanya kuandika Barua ndefu kwa Rais SSH. Asitumike na wanaharakati, Wakenya na wanasiasa uchwara.

Mwalimu wa Sheria hajawahi kuona wala kushauri mapumgufu hayo ya kisheria toka uhuru huku akifundisha sheria. Kama siyo kuwalisha matango pori wanafunzi UDSM ni nini?

Huenda yeye siyo Mwalimu wa Sheria ya ardhi. Fine! Lakini inaonesha hata kozi anazofundisha huenda zina mapumgufu mengi tu Ila hajawahi kushauri hata siku moja.
 
Sheria za ardhi kama zilivyo hazina tofauti na ile experiment ya ujamaa. Migogoro haitamaliza hadi pale tutaposema sasa wanasiasa waondoke kwenye umiliki wa ardhi.

Pengine akili yangu ni fupi, kwanini kuna tofauti kati ya umiliki wa ardhi na mali zengine kama gari / duka / nguo ? Sijawahi kusikia mtu kusema nguo za wananchi zote mfadhili wake ni raisi !
 

Ukidhibiti ardhi ni rahisi kutawala. Atakaye kupinga unamfukuza. Ndiyo maana wakomunisti na wajamaa wanapenda kupora ardhi.
 
Nadhani hayo mengine unaweza kuyazungumzia wewe..., pia ungemsoma issue sio wasihame (bali wahamishwe kwa utaratibu wa kisheria) pia kama wanahama iwe ni kwa manufaa ya taifa; sasa anajiuliza kama kupishwa wawindaji wasibughudhiwe ni manufaa ya taifa (yeye hajui jibu ingawa hilo swali linamyima usingizi)
 
Ndiyo maana tunahitaji Katiba mpya ,itakayogusa maeneo yote haya.
Rasimu ya katiba hiyo isiandikwe na wanufaika wa uovu unaoendelea (wanasiasa/viongozi wastaafu).

Tujifunze tulipokosea kwenye jopo la kina Warioba.
 
Thats a lot of hot air from Prof Shivji.
Angekuwa in the same situation sidhani kama angekuwa na solution yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…