Prof Shivji: Barua kwa Rais; Ardhi mali ya nani?

Prof Shivji: Barua kwa Rais; Ardhi mali ya nani?

Porapesa
Mbona tunalipia kodi ardhi tuliyojenga nyumba zetu na kukodishiwa kwa a ,muda maalum wa miaka 33,66,99?
Unazungumzia kuondolewa Wamaasai kwa ajili ya uwindaji wa kitalii lakini umefunga macho juu ya ushiroba na mazalia ya wanyama wala huzungumziii kuwa ni vyanzo vya maji kwa kanda nzima ya uhitadhi.
Huzungumziii kuongezeka mno kwa idadi ya watu na mifugo.


Usichanganye sayansi na sheria.

Prof Anazungumzia sheria ya kuwahamisha watu na wewe unazungumzia impact katika mazingira, juu ya yote prof amesema kuwahamisha hao wamasai ifuatwe sheria/taratibu zinazofaa na sio nguvu au hiyari tu.
 
Kwani unadhani hili halijulikani. Upinzani gani unalaumu hapa? Kama ni hawa kina Zitto na Lipumba basi siyo wapinzani. Wapinzani wa kweli kama Mhe Lissu kila siku analipigia kelele na huu ufafanuzi alishatoa siku nyingi tu. Ila ukishakuwa na corrupt system kama hii aliyoipandikiza Magufuli hakuna anayesikia. Najua system ilikuwa corrupt hata kabla yake lakini yeye alifanya mambo yazidi kuwa magumu kwa kuweka wabunge wa hovyo kama kina Tale kwa nguvu.
Wewe chagua unaotaka kuwaamini sikupangii. Huwezi kuona picha ninayoona mimi sababu wewe ni mfia vyama...
 
Aisee Mwigulu anamiliki timu ya Singida star, kassimu majaliwa anamiliki Namungo hizi pesa za kulipa wachezaji mishahara wanapata wapi?Timu inawachezaji 30 kila mchezaji analipwa shs 800000 ,watanzania tuwauliza hawa watawala maswali haya na majibu tupate
Subiri watupwe nje ya mfumo na kubaki wabunge wa kawaida tuone kama wataweza kumiliki timu, hapo nyuma tulikuwa na bendi a,bazo wamiliki wao walikuwa mawaziri yaani Akudo ya Kapuya na Mchinga ya Mdhihiri bendi hizi zilitamba sana wamiliki wake walipokuwa mawaziri lakini baada ya kutokuwa mawaziri bendi hizo zikafa kifo cha mende, kifupi kuendesha hizi bendi au timu za mpira ni hela inayotokana na nyadhifa zao kuwa na mrija wa kulamba asali, sasa subiri waondoke kutakuwa hakuna cha Namungo wala Singida
 
Hii nchi imeharibiwa na siasa, too much lobbying hadi upinzani. Ni ngumu sana kuwa na majadiliano yenye maslahi ya umma watu wasitangulize matumbo yao.

Profesa amesimama na amehesabiwa! Salute Profesa, hii ndio shule yenye manufaa kwa umma na si tumbo lako tu!

Hao wapinzani umewataja tu kuficha ukweli huu aliosema Profesa, umeona ikionekana ni CCM tu ndio wamefanya hili dhamira yako itaumia, hivyo namna pekee ni kuwachanganya na wapinzani kwenye hili ili usikwazike.

Kimsingi kwa sasa rais ndio amegeukia kuwa katiba, na kwakuwa anaweza kuingia madarakani kwa kupora uchaguzi, basi anafanya lolote kwa maagizo na ushauri wa wapambe wake.
 
Wewe chagua unaotaka kuwaamini sikupangii. Huwezi kuona picha ninayoona mimi sababu wewe ni mfia vyama...
Mimi sina chama chochote nachokiunga mkono asilani. Nasimamia kwenye ukweli tu. Magufuli mwenyewe alipoingia madarakani siku za mwanzo mwanzo kabla hajaharibu nilimsapoti sana sana. Ila ukweli ni kuwa alichosema Prof Shivji ni ukweli mtupu ambao Lissu amekuwa anausema tangu hili sakata lianze na kabla ya hapo alishazungumzia sana hili jambo. Kumchukia kwako hakubadilishi ukweli. Magufuli mwenyewe aliyekuwa anajiita rais wa wanyonge, huu utata alikuwa na nafasi ya kuutatua once and for all lakini hakufanya chochote na ndiyo maana mafisadi wamepata nafasi sasa hivi.
 
Porapesa
Mbona tunalipia kodi ardhi tuliyojenga nyumba zetu na kukodishiwa kwa a ,muda maalum wa miaka 33,66,99?
Unazungumzia kuondolewa Wamaasai kwa ajili ya uwindaji wa kitalii lakini umefunga macho juu ya ushiroba na mazalia ya wanyama wala huzungumziii kuwa ni vyanzo vya maji kwa kanda nzima ya uhitadhi.
Huzungumziii kuongezeka mno kwa idadi ya watu na mifugo.
Wewe unaongelea tumbo upate uteuz mwenzio Prof anaitendea haki elimu yake
 
Bwashe huyu Profesa Shivji sasa ameanza kuwa tapeli. Amefundisha kozi ya sheria UD zaidi ya miaka 30 lakini miaka hiyo yote hajawahi kuona mapumgufu hayo hadi leo na kujifanya kuandika Barua ndefu kwa Rais SSH. Asitumike na wanaharakati, Wakenya na wanasiasa uchwara.

Mwalimu wa Sheria hajawahi kuona wala kushauri mapumgufu hayo ya kisheria toka uhuru huku akifundisha sheria. Kama siyo kuwalisha matango pori wanafunzi UDSM ni nini?

Huenda yeye siyo Mwalimu wa Sheria ya ardhi. Fine! Lakini inaonesha hata kozi anazofundisha huenda zina mapumgufu mengi tu Ila hajawahi kushauri hata siku moja.

..Prof.Shivji ni mtetezi mkubwa wa masuala ya haki za ardhi hapa nchini.

..kwa kumbukumbu zangu aliwatetea sana wananchi wa jamii ya Wabarbaig / Datoga waliohamishwa kwa nguvu ktk ardhi yao maeneo ya Basuto.

..pia Prof.Shivji, kama sijakosea, alikuwa ktk Tume ya uchunguzi ya Raisi iliyohusisha masuala ya ardhi.
 
Walirithishwaje? Maana kwa sheria za nchi arshi ni mali ya serikali. Hakuna ardhi ya mtu. Ndio maana una nunua kiwanja na bado unalipia kodi
Ardhi mali ya serikali umetoa wapi?
 
Ningependa kujua CV ya mtu fulani..inawezekana tatizo linaanzia hapo pia...hii ndio tofauti ya professor mwenye ngozi nyeupe na hawa weusi...ila ngozi nyeusi jamani laana tupu...
 
Kwa heshima na taadhima pokea barua yangu nikikutumia kwa nia njema na katika kutekeleza wajibu wangu kama mwananchi na mwanazuoni kwa mujibu wa Ibara 26 ya Katiba “kuhakikisha hifadhi ya Katiba na sheria za nchi.”

Awali ya yote nakutakia maisha marefu yenye afya njema na furaha tele ili uendelea kutuongoza kwa busara na hekima na kwa kulinda Katiba yetu bila hofu au upendeleo.

Katika sakata la Loliondo na Ngorongoro nimesikia mara kwa mara Waheshemiwa Mawaziri husika wakitamka Bungeni kwamba ardhi yote nchini ni mali ya umma na hakuna mwenye ardhi. Kwa heshima, kwa maoni yangu, tafsiri hiyo ya sheria sio sahihi.

Ni kweli kwamba Sheria ya Ardhi inasema ardhi yote nchini ni ‘public lands’ yaani ardhi ya kiumma na imewekwa mkononi mwa Rais kama mdhamini kwa niaba ya wananchi. Kifungu 4, kifungu kidogo 1, cha Sheria ya Ardhi 1999 (sura 113) kina tamka kwamba ardhi yote nchini Tanzania itaendelea kuwa ardhi ya kiumma na itaendelea kuwa mkononi mwa Rais kama mdhamini kwa niaba ya wananchi wa Tanzania.

Kifungu hiki kinahitaji ufafanuzi. Kwa nini sheria inatumia neno ‘itaendelea’? Kwa sababu tangia mwaka 1923, sheria ya ardhi ya kikoloni ili tamka kwamba ardhi yote nchini ni ardhi ya kiumma na ikawekwa mkononi mwa Gavana. Mfumo huo haukubadilika baada ya Uhuru isipokuwa tu badala ya neno ‘Gavana’ ikawekwa neno ‘Rais’. Mfumo huu umeendelezwa na Sheria ya Ardhi ya 1999 ambayo ni sheria mama kuhusu mfumo wa umilikaji ardhi (land tenure system) Tanzania.

Napenda ni sistize jambo moja. Kifungu hiki hakisemi, wala hakimaanisha, kwamba ardhi ni mali ya umma. Kinainisha tu ardhi kama ardhi ya kiumma na sio tamko la umilikaji ardhi. Kuna tofauti ya msingi kati ya kuainisha ardhi na kumilikisha ardhi. Neno ‘mali’ halipo kabisa katika kifungu hiki. Kwa hivyo, ardhi sio mali ya umma wala ya Rais wala ya Serikali. Kama hivyo ilivyo, basi ardhi ni mali ya nani?

Kifungu cha 4, kifungu kidogo cha 3, kinasema kwamba wote waliokuwa wana kaalia ardhi kabla ya Sheria ya 1999 kwa hati rasmi au kwa mujibu wa mila na desturi wataendelea kukaalia ardhi hiyo. Kifungu kidogo hiki kinaendelea kusisitiza kwamba ukaaji wa ardhi chini ya hati rasmi au kwa mujibu wa mila na desturi itahesabiwa kama mali (‘property’). Katika kifungu hiki mara ya kwanza sheria inatumia neno mali, kwa Kiingereza, property. Kifungu hiki kinaendelea kusisitiza kwamba pamoja na ukaaji kuwa mali, pia matumizi ya ardhi kama malisho ya mifugo kwa mujibu wa sheria za mila na desturi inahesabiwa kuwa mali. Moja kwa moja, sheria imeweka wazi kabisa kwamba matumizi ya ardhi na wafugaji kwa malisho ya mifugo yao inahesibiwa kama mali, yaani property.

Sasa ardhi ni mali ya nani? Ardhi ni mali ya wenye hati rasmi au jamii au kaaya au watu binafsi wanaokaalia ardhi kwa mujibu wa mila na desturi, pamoja na wafugaji ambao hutumia ardhi yao kama malisho. Hao ndio wenye ardhi, sio umma wala Rais wala serikali. Kwa hivyo, sio sahihi kabisa kusema kwamba ardhi ya Tanzania haina wenyewe.

Tafsiri ya sheria niliyotoa hapo juu iliwekwa wazi na Mahakama ya juu kabisa nchini, Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Mwanasheria Mkuu dhidi ya Lohay Akonaay na Joseph Lohay iliyoamuliwa mnamo mwaka wa 1994 na kuchapishwa rasmi katika Ripoti za Kesi, Tanzania (Tanzania Law Reports) [1995] T.L.R. 80). Ninanukuu kipengele muhimu cha uamuzi huo:

“Haki za ardhi chini ya mila na desturi, ingawa kwa uhalisia wake ni haki ya kukaa na kutumia ardhi, bado ni mali [property] ambayo inalindwa na ibara 24 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na utwaaji wa haki za mila bila fidia ya haki inazuiliwa na Katiba.” (uk. 81)

Kama kweli hii ndio sheria ya nchi kwa nini upotoshaji na Waheshemiwa Mawaziri umeendelea bila kupingwa au kusahihishwa? Kwa nini Waheshemiwa Mawaziri wanapotamka kwamba ardhi ya Tanzania ni mali ya umma hawabanwi, (kama wanaobanwa waheshimiwa wabunge wengine), kunukuu kifungu cha sheria kinachosema ardhi ni mali ya umma?

Kwa kadri ya uelewa wangu, mwenye dhamana na wajibu wa kutoa tafsiri ya sheria Bungeni na kushauri wabunge (bila kujali vyama vyao) na Bunge juu ya sheria ni Mwanasheria Mkuu. Kama tunajuwa, hatimaye kauli ya mwisho juu ya tafsiri ya sheria ni Mahakama lakini anyetakiwa kutoa tafsiri ya sheria Bungeni pale ambapo kuna ubishi ni Mwanasheria Mkuu, sio Mheshemiwa Spika wala mbunge mwingine yeyote hata kama yeye ni mwanasheria.

Kwa kuwa tafsiri ya sheria iliyotolewa na Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Akonaay imeweka wazi kwamba haki ya kumiliki ardhi chini ya mila na desturi ni mali inayolindwa na ibara ya 24 ya Katiba na kwa kuwa kauli ya Mahakama ya Rufaa ni kauli ya mwisho, basi ardhi ya jamii ya wafugaji wanaoishi na kutumia ardhi yao katika maeneo ya Loliondo na Ngorongoro kwa malisho, haiwezi kutwaaliwa na serikali bila kufuata taratibu za sheria zilizowekwa katika Sheria ya Utwaaji wa Ardhi, sura 118 (Land Acquisition Act). Mwenye mamlaka kutwaaa ardhi ni Rais na hanabudi afuate hatua zote za kutwaa ardhi zilizotajwa katika Sheria, sura 118. Kinyume na hii, uhamishaji wa wenyeji kutoka maeneo haya, kwa kulazimishwa au kwa hiari, ni batili na moja kwa moja inavunja sheria za nchi na haki za msingi za binadamu kama zilivyo orodheshwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa kuhitimisha barua yangu, Mheshemiwa, naomba nijumuishe hoja zangu kama ifuatavyo:
Mosi, ardhi yote ya Tanzania ni ardhi ya kiumma. Tamko hili la sheria ni tamko la kuainisha ardhi sio tamko la kumilikisha ardhi kwa serikali.

Pili, ardhi imewekwa mkononi mwa Rais kama dhamana. Kazi yake kama mdhamini ni kuhakikisha kwamba ardhi inawanufaisha wananchi na sio vinginevyo. Kisheria na kwa mujibu wa mila za kisheria tunazifuata, mdhamini (trustee) ana wadhifa wa kipekee na ni nzito. Uhusiano kati ya mdhamini na mnufaishwa ni uhusiano mahsusi ambao sheria na mila inaangalia kwa jicho la kipekee.

Tatu, umiliki ardhi wa moja kwa moja unabaki kwa wenye hati rasmi na watu au kaaya au jamii kwa mujibu wa mila na desturi.

Nne, umilikaji wa ardhi kupitia mila na desturi ni mali, property, na inalindwa na Katiba.

Tano, Ardhi ya mila haiwezi kutwaaliwa na Rais bila kufuata hatua zote zilizoainishwa katika Sheria ya Utwaaji wa Ardhi (Land Acquisition Act).

Mwisho, kutokana na mambo ya msingi niliyotaja hapo juu, wakaazi wa Ngorongoro na Loliondo, hususan jamii za wafugaji, hawawezi kuondolewa kutoka ardhi yao bila kufuata taratibu za kisheria na kwa sababu mahsusi ambayo lazima ijulikane na kujadiliwa hadharani.

Mheshemiwa Rais, sisi sote, wananchi pamoja na serikali tujiulize: Je, ondowaji wa wananchi kutoka ardhi yao, ambayo ni uhai na urithi wao, kwa minajili ya kupisha wanyama pori ili makampuni ya uwindaji, kwa mfano, yaweze kufanya shughuli zao kuwaleta wawindaji kuwinda wanyama pori bila kubughudiwa na wananchi, ni kwa manufaa mapana ya umma wa Tanzania? Nakiri sina jibu isipokuwa swali hili limenikosesha usingizi.
Nakutakia kila la kheri Mheshemiwa Rais

Issa Shivji
Profesa Stahiki (Professor Emeritus)
Shule Kuu ya Sheria
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
 
Prof.katema madini muhimu yaani spika wa bunge anajipa mamlaka ya kutoa ufafanuzi wa kisheria wakati mwanasheria mkuu wa serikali yupo only in Africa
20220624_120149.jpg
IMG-20220625-WA0003.jpg
 
Sasa ukisikia kutimiza ahadi ya kumi ya TANU ndio huku.
Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu wote na nitaitumia elimu yangu kwa faida ya wote. Hongera Profesa.
Wengi hatuna mwanga wa kutosha wa masuala mengi ya kisheria,na pengine tumeshabikia Kama tunavyobikia yanga na Simba,kwa issues ambazo ni very sensitive zinagusa maisha ya watu na pia kuleta taharuki isiyokuwa lazima.
Swali, Ni kweli Mwanasheria mkuu hajui haya aliyoandika Profesa? Kama anajua amenyamaza kwa maslahi ya nani? Inawezekana kuna nia njema kwa watawala kuwahamisha wamasai,hata hivyo ni muhimu sana kuheshimu sheria na katiba yetu.
Mwaka 1984, aliyekuwa waziri mkuu Hayati Edward Sokoine alianzisha operesheni ya kupambana na wahujumu wa uchumi, pamoja na nia njema ya operesheni ile,njia zilizotumika hazikuwa halali. Zilileta umaskini mkubwa kwa watu wengi na baadaye wale walioathirika walikwenda mahakamani na wakati ule tulikuwa na majaji kweli, hawakuiogopa serikali, waliheshimu Sana taaluma zao,waliona kweli serikali ilikosea na waliamuru watu wale walipwe fidia. Na sifa pekee ya Mwalimu Nyerere aliyokuwa nayo kwa sehemu kubwa aliwaheshimu sana majaji na mahakimu.
Suala la Loliondo na Ngorongoro liendeshwe kwa kuheshimu katiba na sheria, nyakati huwa zinabadilika,huko mbele kama kuna dhuluma imetendeka itatupa madhara huko mbele. Mambo hubadilika na kati ya mambo ambayo hatuwezi kuyqzuia bila kujali uwezo wa kijeshi,uchumi na elimu ni MUDA na MABADILIKO. Tunapenda hatupendi kuna nyakati zinakuja watanzania hawatakuwa hivi walivyo. Rumi ilitawala dunia kwa miaka mia tano,where is Romans now? Haki na kweli ni marafiki wakubwa,huwezi kutaka haki na ukaitaa Kweli na huwezi kutaka kweli na ukaitaa haki.
 
Porapesa
Mbona tunalipia kodi ardhi tuliyojenga nyumba zetu na kukodishiwa kwa a ,muda maalum wa miaka 33,66,99?
Unazungumzia kuondolewa Wamaasai kwa ajili ya uwindaji wa kitalii lakini umefunga macho juu ya ushiroba na mazalia ya wanyama wala huzungumziii kuwa ni vyanzo vya maji kwa kanda nzima ya uhitadhi.
Huzungumziii kuongezeka mno kwa idadi ya watu na mifugo.
Profesa amejikita kwenye ufafanuzi wa umiliki wa Ardhi kisheria, hayo mengine na ww muandikie Raisi barua ataisoma ulitaka barua ya profesa ieleze kila kitu?itakuwa barua au kipamfleti Cha Msabila na Mabala?
 
Umetoa somo zuri sana professor. From my little knowledge kwenye sekta nzima ya Ardhi ni kuwa Raisi ni msimamizi mkuu wa Ardhi but sio mmiliki wa Ardhi nzima ya nchi yetu na hana mamlaka ya kuchukua ardhi kwa mwananchi pasipo kufuata sheria zote za wamiliki wa ardhi katika eneo husika. Na ukisoma vizuri hizi sheria zipo kwenye land act zote but hawa wabunge wanaochanganua hizo sheria huko bungeni sidhani kama wanajua hata hizo land act kwakweli
 
Porapesa
Mbona tunalipia kodi ardhi tuliyojenga nyumba zetu na kukodishiwa kwa a ,muda maalum wa miaka 33,66,99?
Unazungumzia kuondolewa Wamaasai kwa ajili ya uwindaji wa kitalii lakini umefunga macho juu ya ushiroba na mazalia ya wanyama wala huzungumziii kuwa ni vyanzo vya maji kwa kanda nzima ya uhitadhi.
Huzungumziii kuongezeka mno kwa idadi ya watu na mifugo.

NB:kisheria pale mwananchi anapotokea na kuliendeleza eneo lolote kwa kilimo, ufugaji au activity yoyote kwa zaidi ya miaka 10 basi eneo hilo litatambulika kama ni mali yake kwa asilimia 60-70 pale ambapo atatokea mtu na document halali basi hana budi kuishi katika hizo sheria hapo. So kimsimgi wale wamasai wana haki ya kutolewa eneo lile kisheria na kwa mikataba watakayoridhia wao sio serikali.
When it comes to your suggestion hapo ni kwamba sisi wamiliki wa ardhi kupitia hati au document zozote ni watunzaji wa ardhi hii ambayo ipo chini ya raisi. Na lolote ambalo litatakiwa kufanyika chini ya kipande chako cha ardhi ni lazma haki za msingi za umiliki wako ufatwe kwanza. Mfano mzuri ni fidia utakayolipwa wewe mwenye hati ni tofauti kabisa na yule ambaye hana document zozote za umilikishwaji
 
Back
Top Bottom