Prof Shivji: Barua kwa Rais; Ardhi mali ya nani?

Prof Shivji: Barua kwa Rais; Ardhi mali ya nani?

Porapesa
Mbona tunalipia kodi ardhi tuliyojenga nyumba zetu na kukodishiwa kwa a ,muda maalum wa miaka 33,66,99?
Unazungumzia kuondolewa Wamaasai kwa ajili ya uwindaji wa kitalii lakini umefunga macho juu ya ushiroba na mazalia ya wanyama wala huzungumziii kuwa ni vyanzo vya maji kwa kanda nzima ya uhitadhi.
Huzungumziii kuongezeka mno kwa idadi ya watu na mifugo.
Professor alivyokosa usingizi, akili yake ikawa imeenda upande kidogo. Kwa jinsi ninavyofahamu, ownership of land kwa TZ ni aina nne----Communal, public, private, state.

Sasa inategemeana Professor Shivji, kwa vile sheria zetu ni mbovu, tutaambiwa kwenye ardhi yako ikipatikana mafuta au Tanzanite, serikali inakuondoa na kukulipa labda millioni chache tu.

Suala la kuvamia mbuga za wanyama, hiyo siyo sawa kama suala la Ngorongoro, hao Wamaasai wanapaswa kuondolewa.
 
Suala sio ardhi kuwa mali ya nani, suala ni uoto wa asili kwa miaka mingi ijayo.

Hawa wasomi wetu wanajua sana kukosoa, ni watu wa nadharia zaidi kuliko vitendo.

Loliondo ikipoteza sifa za kutunza wanyama, watakaolamiwa ni SSH na serikali yake.
 
Yaani hadi Sasa wabunge 300 hawajui Sheria za ardhi,vijiji na vitongoji !Halafu najiuliza maswali mbona waziri anayehusika na maliasili yupo kimya!
 
Kuna wakati mwingine naona wanataka Kiki tu
Tangu lini hifadhi ikawa ya binadamu
Viherehere tu
Wanyama wapewe amani na watalindwa kwa nguvu zote
Hivi nani alitangulia hapo nyani au mmasai
 
Watanzania tukianza kumwandikia raisi barua ya wazi kwa kero zetu, is that the effective way of communication? Kwa swala la Loliondo, kama nchi, hatuwezi kupanga what to do effectively, kwa manufaa ya nchi yetu?

Kwa Loliondo ipo kwa kuwanufaisha wakenya kuleta mifugo yao kulisha, kwa sababu tu ni wamasai?

Mtu asijiite mwanazuoni mwenyewe. Sisi tunajua qualifications zake, na tukipima material facts, ndiyo tuseme" mwazuoni" kaandika au kasema! Na akiandika mavi, tutasema hivyo. Shivji asitangulize kujitambulisha, yeye ni ni mwanazuoni kama kinga! Sisi tunayo haki ya kuijadili na kutoa maamuzi. Kwa hiyo aipeleke kwa debate, watu waijadili, na kupitia majadiliano hayo, raisi will pick the facts!

Duniani, nchi nyingi zimehamisha watu wao ndao kwa manufaa makubwa ya nchi. Eg: USA, Canada (red indians), Brazil, Botswana (Basarwa), n.k. Kama raia hawatakiwi kuachwa porini bila huduma muhimu kama; maji Safi, hospital services, schools, and many other social services.
 
Mimi sina chama chochote nachokiunga mkono asilani. Nasimamia kwenye ukweli tu. Magufuli mwenyewe alipoingia madarakani siku za mwanzo mwanzo kabla hajaharibu nilimsapoti sana sana...
Wewe Fisadi tulia,endelea kulamba asali muda unayoyoma.
 
Prof kaisaidia mambo kadhaa.
Kwamba ili kumhamisha mtu kutoka eneo lake kwenda kwingine, lazima kumlipa...
Ungefafanua kwa kupinga pointi za shivji kwa kunukuu vifungu alivyotaja ungekuwa na hoja , ila k.m ni kwa uelewa wako, nadhani sheria sio fani yako!
 
Bwashe huyu Profesa Shivji sasa ameanza kuwa tapeli. Amefundisha kozi ya sheria UD zaidi ya miaka 30 lakini miaka hiyo yote hajawahi kuona mapumgufu hayo hadi leo na kujifanya kuandika Barua ndefu kwa Rais SSH...
Kuna ya kuongea ili uckike na kuongea ili ujenge hoja, nadhani umeckika ila hauna hoja!
 
Ningependa kujua CV ya mtu fulani..inawezekana tatizo linaanzia hapo pia...hii ndio tofauti ya professor mwenye ngozi nyeupe na hawa weusi...ila ngozi nyeusi jamani laana tupu...
Kuna tofauti ya kilichoongelewa na aliyekiongea, k.m ni fact , hata angeongea asiye na cv ingebaki kuwa fact
 
Watanzania tukianza kumwandikia raisi barua ya wazi kwa kero zetu, is that the effective way of communication? Kwa swala la Loliondo, kama nchi, hatuwezi kupanga what to do effectively, kwa manufaa ya nchi yetu...
Kwa barua ya wazi wengi tutaona facts,k.m sio lazima majadiliano , kuwasilsha ujumbe njia ni nyingi, wewe k.m unaweza ndio uipelke kwa debate ila sio umpangie wapi au namna gani aiwasilishe
 
Nimesoma waraka wa Shivji kwa Rais umenitagakarisha sana. Kumbe ardhi sio mali ya Serikali. Sheria ya ardhi inasema ardhi yote nchini ni "public land" yaani ardhi ni ya kiumma na imewekwa mikononi mwa Rais kama mdhamini kwa niaba ya wananchi.

Kifungu 4, kifungu kidogo 1, cha sheria ya Ardhi 1999 (sura 113) kinatamka kwamba ardhi yote nchini Tanzania itaendelea kuwa ardhi ya kiumma na itaendelea kuweka mkononi mwa Rais kama mdhamini kwa niaba ya Watanzania.

Mwaka 1923 Sheria ya ardhi ya Kikoloni ilitamka kwamba ardhi yote ya nchi ni ya kiumma na itawekwa mkononi mwa Gavana, mwaka 1999 neno Gavana likatolewa likawekwa neno "Rais", Shivji akasisitiza kuwa kifungu hakisemi ardhi ni mali ya umma, kinamaanisha ardhi ya kiumma.

Kumilikisha ardhi. Kifungu cha 4, kifungu kidogo cha 3, ukaaji wa ardhi chini ya hati rasmi au mujibu wa kimila na desturi itahesabiwa kama mali (property). Kwa hiyo ardhi ni mali ya wenye hati rasmi au jamii au kaya au watu binafsi wanaokalia ardhi kwa mujibu wa mila na desturi, pamoja na wafugaji wanaotumia ardhi kama malisho.

Sasa swala la Ngorongoro ardhi ile wanataka kumilikisha kwa nani? Tukumbuke kuna mtoto wa mfalme wa kiarabu alimilikishwa adhi maeneo hayohayo kwa mkataba ambao labda Magu ndio angewza uvunja na hadi leo ni yake sikumbuki awamu ya ngapi..
 
Walirithishwaje? Maana kwa sheria za nchi arshi ni mali ya serikali. Hakuna ardhi ya mtu. Ndio maana una nunua kiwanja na bado unalipia kodi
Vipi kama serikali iliwakuta wao wapo hapo tangia kipindi cha ukoloni?
 
Muulize shivji! Loliondo ni Game Controlled Area tangu mwaka 1951 Tanzania ikiwa chini ya ukoloni inakuwaje anadai ni eneo la Wamasai?

Kweli ukizeeka akili inapungua
Usichoelewa ni kwamba hata wakoloni waliwakuta Wamasai hapo. Kwani wakoloni walipokuja na kusema wamevumbua mlima Kilimanjaro Wachaga walikuwa hawapo hapo?
 
Prof. ameeleza waziwazi kinagaubaga, mbinu na mkakati uliotumika na unaoendelea wa kuwatoa Wamasai ktk ardhi yao si sahihi, bali niinavyo utakuwa mpango wa kikundi fulani cha wahuni waliokwisha kulamba asali. Hakika nchi hii tutafika tuendako tukiwa tumechoka sana, mgeni kuthaminiwa kuliko utu na ubinadamu wa mzawa eti! Inasikitisha namna wanavyoondolewa kihuni sana na ajabu baadhi ya watu wamepoteza maisha na wengine kupata ulemavu usiokoma.
 
Bwashe huyu Profesa Shivji sasa ameanza kuwa tapeli. Amefundisha kozi ya sheria UD zaidi ya miaka 30 lakini miaka hiyo yote hajawahi kuona mapumgufu hayo hadi leo na kujifanya kuandika Barua ndefu kwa Rais SSH. Asitumike na wanaharakati, Wakenya na wanasiasa uchwara.

Mwalimu wa Sheria hajawahi kuona wala kushauri mapumgufu hayo ya kisheria toka uhuru huku akifundisha sheria. Kama siyo kuwalisha matango pori wanafunzi UDSM ni nini?

Huenda yeye siyo Mwalimu wa Sheria ya ardhi. Fine! Lakini inaonesha hata kozi anazofundisha huenda zina mapumgufu mengi tu Ila hajawahi kushauri hata siku moja.
Yeye tunajua mchango wake kwa nchi hii, haya hebu tuambie wewe hapa nchini una mchango gani? Ukifa leo utakumbukwa kwa lipi hasa?
 
Kwa hiyo Taifa kama Taifa halina uhalali wa kuitumia ardhi yake kwa manufaa ya Umma wote wa kitanzani na sio jamii ya kabila fulani tu profeseli?
Nadhani hukusoma ukaelewa. Prof ameainisha ili ardhi iweze kutumiwa kwa matumizi mengine ni lazima sheria ya kuitwaa hiyo ardhi itumike itumike. Sasa serikali haijafanya hivyo
 
Watanzania tukianza kumwandikia raisi barua ya wazi kwa kero zetu, is that the effective way of communication? Kwa swala la Loliondo, kama nchi, hatuwezi kupanga what to do effectively, kwa manufaa ya nchi yetu?

Kwa Loliondo ipo kwa kuwanufaisha wakenya kuleta mifugo yao kulisha, kwa sababu tu ni wamasai?

Mtu asijiite mwanazuoni mwenyewe. Sisi tunajua qualifications zake, na tukipima material facts, ndiyo tuseme" mwazuoni" kaandika au kasema! Na akiandika mavi, tutasema hivyo. Shivji asitangulize kujitambulisha, yeye ni ni mwanazuoni kama kinga! Sisi tunayo haki ya kuijadili na kutoa maamuzi. Kwa hiyo aipeleke kwa debate, watu waijadili, na kupitia majadiliano hayo, raisi will pick the facts!

Duniani, nchi nyingi zimehamisha watu wao ndao kwa manufaa makubwa ya nchi. Eg: USA, Canada (red indians), Brazil, Botswana (Basarwa), n.k. Kama raia hawatakiwi kuachwa porini bila huduma muhimu kama; maji Safi, hospital services, schools, and many other social services.
Ni ukweli umeandika ila huna hoja. Karejee andiko la Prof kwanza! Ni bahati mbaya tu
 
Back
Top Bottom