Prof Shivji: Barua kwa Rais; Ardhi mali ya nani?

Profesa Shivji hoja na ushauri wako utaeleweka kwa mawaziri wachache! ni muhimu kufuata sheria za nchi.
 
Nadhani hukusoma ukaelewa. Prof ameainisha ili ardhi iweze kutumiwa kwa matumizi mengine ni lazima sheria ya kuitwaa hiyo ardhi itumike itumike. Sasa serikali haijafanya hivyo
Huyo profesa kazeeka mkuu,hata kufikiria kwake kumezeeka pia,yaani tuseme baba mzazi kwenye kuamua matumizi ya mali yake kwa manufaa watoto wake wote ndio atake ridhaa yangu mimi mmoja kweli,sasa ubaba wake utakuwa na manufaa yapi tena?
 
Tupe na wewe references zako za kisheria.
 
Huyo profesa kazeeka mkuu,hata kufikiria kwake kumezeeka pia,yaani tuseme baba mzazi kwenye kuamua matumizi ya mali yake kwa manufaa watoto wake wote ndio atake ridhaa yangu mimi mmoja kweli,sasa ubaba wake utakuwa na manufaa yapi tena?
Tunayo safari ndefu kwa fikra nyepesi kiasi hiki. Haki haiangalii idadi, ukubwa au udogo. Kama hiyo ardhi ilihitajika kwa manufaa ya umma, lazima awashirikishe na wakubaliane jinsi ya kufidiwa, na sio kusombwa tu bila mikataba yoyote inayoeleweka. Hata ardhi ya makaburi inachukuliwa kwa makubaliano na fidia.
 
Muulize shivji! Loliondo ni Game Controlled Area tangu mwaka 1951 Tanzania ikiwa chini ya ukoloni inakuwaje anadai ni eneo la Wamasai?

Kweli ukizeeka akili inapungua
Kwahiyo unataka kusema wamasai hawakuwepo loliondo kabla ya wakoloni kuja nakuweka hizo sheria?.kuna maeneo mengi tu ambayo ni Game controled na bado kuna jamii za wafugaji wanaishi.Kwenye Game Reserve na Nation Parks ndiko ambako sheria imekataza kabisa kufanya shughuli yoyote yakijamii labda kwa kibali maalum.
 
Tasnia ya sheria haijawai kujitosheleza,ndo maana kunakua na mabadiliko ya sheria kila wakati kunapokua na mahitaji.Kwasasa kumeonekana kuna uhitaji wa tafsiri ya sheria ndo maana prof katoa ufafanuzi,na ufafanuzi wake uko clear.kama hujaelewa jielimishe.
 
Teh teh teh teheeheeeee
Kaaaz kweli kweli,ndio maana madikteta wenye akili nchi zao zinatusua sana kimaendeleo kwani hakuna mambo ya kubembelezana,ni kutekeleza tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…