Prof. Tibaijuka: Chato haina sifa kuwa Mkoa
"Katika mazishi Wazee Chato walimuomba Rais Samia mkoa wakidai ni ahadi ya mtangulizi wake.kwa hekima akasema ataangalia vigezo.Kama Mbunge Mstaafu jirani Muleba Kusini najua vigezo havipo.Wazo halitekelezeki. Wazee jirani na sisi naamini tutapewa nafasi kushauri"Anna Tibaijuka

---
Anaandika PROF. ANNA K. TIBAIJUKA

Ramani inaonyesha Chato ni sehemu ya Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera. Kiuhalisia. Na kihistoria. Mengine ni kulazimishalazimisha tu.

Naendelea kusisitiza hakuna hoja yoyote ya kiuchumi kuunda mkoa wa Chato. La sivyo basi tuelimishwe.

Ila kama mnapenda siasa za upendeleo wa sehemu fulani ama kwa kuwa mkubwa aliwahi kuzaliwa pale au mtu apewe nafasi kwa sababu ni mtoto wa kiongozi endeleeni kuwabebesha wananchi mizigo ya kulipa kodi kusudi wateule wajichane. Period.

Kwanza ikumbukwe Mkoa wa Geita ulianzishwa kusudi Chato iwe Makao Makuu. Ikakosa vigezo. Geita mjini ikaonekana ndiyo yenye sifa za kuwa Makao Makuu ya Mkoa mpya wa Geita. Hii ilikuwa 2010. Sasa 11 years later Chato ati ina vigezo kuwa Makao Makuu ya Mkoa wake wenyewe? Are we serious with our development? Really? Na Rais wetu mpendwa SSH tunataka kweli kumtwisha zigo la kuamua jambo hili na controversy zake? Elimu haina mwisho. Mimi kama kuna vigezo naomba viorodheshwe. Labda ndiye sina taarifa. Ila so far Hoja ya kuwaletea maendeleo Kakonko, Biharamulo, Ngara na Muleba inayokatwa vipande ninazikataa. Mkoa unaweza kuleta maendeleo gani kwa Wilaya yake wakati Mkoa unategemea bajeti ya Serikali Kuu. Mkoa una mapato gani zaidi ya kutumia kodi? Lets be serious. Maendeleo yanatokana na uwekezaji na uwezeshaji kwa wananchi. Siyo watumishi wa Serikali tena baadhi bila maadili wanaweza kuishia kuwabugudhi wananchi badala ya kuwa msaada.

Njia pekee kumuenzi Hayati Magufuli ni kurekebisha mambo ambayo kama binadamu hakufanya vizuri. Mengine yote ni ubinafsi. Na kufifisha sifa zake katika historia ya nchi hii. Tumuache apumzike.

Miundombinu iliyowekwa Chato siyo kigezo kuunda mkoa hapo. Tuikamilishe na kuitafutia matumizi mbadala ya kitaifa. Mfano Airport ya Chato inaweza kufanywa Hub ya kilimo cha contract floriculture na horticulture...(kilimo mkataba cha maua na mboga) ili tuwe na ndege za mizigo kuja kubeba. Na maziwa .

Hospitali ya Kanda Chato.... naomba tutathmini kwanza maendeleo ya hospitali ya Mloganzila. State of the Art buildings only 40km away from Dar City Centre na Muhimbili. Mojawapo ya mafanikio makubwa ya Awamu ya nne. Lakini Angalia changamoto zake. Uhaba wa madaktari hadi leo. Sasa hao specialist doctors watakaokubali kuishi Chato mtawalipa fedha kiasi gani?. A hospital is not just buildings. Its manpower resources and the economy surrounding it. Katika dhana ya mipango miji na maendeleo ya makazi lazima vigezo vyote hivyo kuangaliwa. Kwa uelewa wangu Chato haina vigezo. Tusidanganyane.
Haya ndio maoni ya kisomi japokuwa watakushambulia sana hasa hao wanaotaka kuikana asili yao kwamba mvuyekule hata mimi niongezee kujiundia wilaya au mkoa hakuwezi kufuta uasilia wa lolote katika yote.
 
Mama wa hela ya mboga ktk ubora wake, [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huyo mama tangu alivyotujibu kuwa milioni 80 ni vi hela vya mboga tu kwa hili tumuangalie tu, CHATO kuna sababu zote kuwa mkoa kama miundombinu ikiwemo Airport, hospital ya kisasa, ofisi za TRA, mahakama, chuo cha VETA miundombinu ya barabara vyote vipo sawa, pia kwa wilaya ambazo zipo mbali na Bukoba mjini na kigoma mjini ni fursa nzuri kwao.
Ulivyovitaja sio sifa ya kuanzisha mkoa na ndio maana kahama na maendeleo yake yote haijaanzishiwa mkoa wake
 
Tunaomba orodha ya sifa zinazotakiwa kwa sehemu ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kufuzu kuitwa mkoa. Tukizipata hizo sifa itaturahisishia kujua kama Chato inakidhi vigezo kwa sasa ama la!
kawaida Hakuna vigezo vikubwa sana vya kuunda mkoa isipokuwa ni serikali kutaka kurahisisha upatikanaji wa huduma na kuwafikia wananchi au kuwapunguzia gharama pale ambapo huduma hiyo huifuata mbali zaidi ya kilomita 200 kutoka wilayani kwenda mkoani
lakini baadhi ya vigezo baadhi ni

Hosptali ya Rufaa moja
Hosptal ya mkoa moja
Chuo kikuu kimoja
idadi ya watu isipungue 500,000
viwanda vidogo visivyozidi 50 kila kiwanda kitoe ajira 250
viwanda vikubwa 5 kila kiwanda kitoe ajira 5000.
Maji angalau yapatikane 65%
umeme wa uhakika
Ajira 60%
mapato 80%
kaya 25,000
Sekondari kila kata na shule za msingi kila kijiji au mtaa.
Barabara zinazopitika na uhakika kutoka wilayani n.k

NB.Muundo huo pia hutumika pia kwenye municipal au majiji.

elimu haina mwisho marekebisho na nyongeza ruksa.
 
Chato haina vigezo? Chato inavigezo maana mkoa haujengwi kwa wilaya moja zitaongezwa na wilaya zingine na mkoa ndo utaitwa wilaya, vitu vilivyopo Chato vimeshaiweka Geita mjini kuwa na uhitaji wa mambo makubwa ya kuheshimisha mkoa hivyo Chato kuwa Mkoa ni muhimu sana.
Tuongee ukweli bila mahaba ivi mikoa kama Morogoro,Tabora na Mbeya kwa kuilinganisha na mkoa wa Geita ipi inastahili kugawanywa? ,Geita haistahili kugawanywa sababu haipo hata katika mikoa mitano mikubwa na yenye population kubwa
 
KUHUSU PROF. TIBAIJUKA NA MKOA MPYA WA CHATO.

Prof Anna Kajumulo Tibaijuka hawez kupenda uwepo wa mkoa mpya wa Chato.

Baadhi ya kata za Muleba zinazomegwa na kuingia mkoa mpya wa Chato ni sehemu ya nyumbani kwake.

Asingependa awe wa Chato bali wa Kagera/Bukoba[emoji851]. Jambo hili linamuuma tangu enzi za marehem. Yuko tayar kwa lolote lakin asiwe raia wa Chato.

Kadhalika sehemu kubwa ya ardhi aliyohodhi na nyingine iliyokatwa na kuingizwa kwenye hifadhi ya Burigi nayo itaenda chato. Kwa hiyo yeye pamoja na mali zake zote za huko rasmi sasa wanakuwa wakazi wa Chato. Inamuuma sana hii mama.

Kwahiyo Her Excellency SSH asipotoshwe na watu wa dizaini hii. Wana yao.

Kikao maalum cha Ushauri cha Mkoa wa Geita kinajua zaidi kuliko Prof. Tibaijuka. Kina wataalam wa uchumi, ardhi, mipango miji, takwimu, makadirio, nk. Prof. hajui kuliko hawa wote.

Zaidi hawa wamekuwa ktk jambo hili kwa muda sasa, taarifa yao ya juzi ni ya kuhitimisha tu. Wameliasses na kulipima kimizania kwa muda.

Prof Tibaijuka akubali tu kuwa mabadiliko huwa yapo na atulie tu awe Mkazi wa Chato.
 
Kwa kihaya jina la " TIBAIJUKA" maana yake " HAWAKUMBUKI"
Majina huumba.
Kwanza.
Fikiria mtu anatoka ngara kuja makao makuu ya mkoa Kagera, si chini ya km 300,ni kama kwenda na kurud moro-dar ,nauli si chini ya elf 18 kwenda ngara- kagera,
Lakini kutoka ngara kwenda chato ni approximately km 70.

Pili,atambue pia ajira zitatengenezwa mkoa mpya ukianzishwa,yeye kashashiba na pesa za mboga za escrow, bahati mbaya jina lake linasadifu yaliyomo ndani yake.

Tatu,
Dhana ya kwamba kagera itapitwa kimaendeleo na Chato ikiwa itakuwa mkoa hiyo ni inferiorty complex.
Wahaya mmeuchelewesha mkoa wenu kuendelea kwa sababu ya ubinafsi wenu pia na ujuaji mwingi kama huu ambao huyu mama "Asiyekumbuka" anataka kuuanzisha

Acheni uzushi na propaganda. Si ajabu watu wanawaita 'sukuma gang'.

Umbali wa kutoka chato mjini mpaka ngara mjini ni kilometa 257.

Ukweli utabaki pale pale Chato haina hadhi ya kuwa Mkoa na pia haina geograhical au historical prerequisites za kufanywa kuwa makao makuu ya mkoa. Yaan ukiangalia history, population, geograghia ya eneo husika na social ecomical factors zingine huwezi kuifanya chato kuwa makao makuu ya Mkoa wowote ule ndani ya kanda ya ziwa.
scv20210530_163441.jpeg
 
Vigezo vya kupafanya mahali mkoa ni nini?
KUHUSU PROF. TIBAIJUKA NA MKOA MPYA WA CHATO.

Prof Anna Kajumulo Tibaijuka hawez kupenda uwepo wa mkoa mpya wa Chato.

Baadhi ya kata za Muleba zinazomegwa na kuingia mkoa mpya wa Chato ni sehemu ya nyumbani kwake.

Asingependa awe wa Chato bali wa Kagera/Bukoba[emoji851]. Jambo hili linamuuma tangu enzi za marehem. Yuko tayar kwa lolote lakin asiwe raia wa Chato.

Kadhalika sehemu kubwa ya ardhi aliyohodhi na nyingine iliyokatwa na kuingizwa kwenye hifadhi ya Burigi nayo itaenda chato. Kwa hiyo yeye pamoja na mali zake zote za huko rasmi sasa wanakuwa wakazi wa Chato. Inamuuma sana hii mama.

Kwahiyo Her Excellency SSH asipotoshwe na watu wa dizaini hii. Wana yao.

Kikao maalum cha Ushauri cha Mkoa wa Geita kinajua zaidi kuliko Prof. Tibaijuka. Kina wataalam wa uchumi, ardhi, mipango miji, takwimu, makadirio, nk. Prof. hajui kuliko hawa wote.

Zaidi hawa wamekuwa ktk jambo hili kwa muda sasa, taarifa yao ya juzi ni ya kuhitimisha tu. Wameliasses na kulipima kimizania kwa muda.

Prof Tibaijuka akubali tu kuwa mabadiliko huwa yapo na atulie tu awe Mkazi wa Chato.
 
Ndugu kuna sababu gani chato kupewa kipaumbele? mbona mikoa kama Tabora,Morogoro na Mbeya ambayo ni mikubwa, yenye population kubwa na jiografia ngumu kuliko huo mkoa mpya unaopendekezwa yenyewe haipewi kipaumbele?
 
Uwanja wetu pendwa tumeingia gharama nyingi sana Ili usiharibike ni vyema tuwape wakulima na wavuvi waanikie mazao yao Ili wautunzen

Chato tayari ni mkoa wananchi kupitia madiwani wao wameshamaliza kutoa mawazo yao na wengi wameshapendekeza wilaya za mkoa wao sasa huyo Prof. alikuwa wapi wakati wa kutoa maoni? Haturudi nyuma tunasonga mbele. Tarehe 14/10/2021 wakati wa sherehe za kuzima Mwenge hapa Chato tunategemea Rais wetu mpendwa Samia atangaze rasmi kuwa Chato ni mkoa. Sasa wasiotaka wajiandae kisaikorojia wasije wakafa na stress bure.
Mama hajakosea. Huyu Profesa hatoi mawazo kwa kukurupuka hili jambo kalifanya analysis ya kutosha japo anachokoza mjadala kwa kudai kuwa anayejua vigezo avitaje.Hapa sio suala la madiwani kupendekeza.Kumbuka kuwa sio lazima kinachoamuliwa na wengi kiwe sahihi mambo mengine yamekaa kiushabiki.
 
Kumbe kaongea yule bibi wa hela ya mboga😂😂😂😂😂😂
Hadi hapo hoja haina mashiko maana n mchumia tumbo tuu prof ushwara😂😂
 
Harafu utasikia
$$$serikali haitengenez nafasi za ajira😂😂😂 . Mm natuliazana najua hapo nishapata pa kumpenyeza mtoto wangu akachume keki ya taifa huku nyumbu wakibweka tuu kama mbwa koko
 
Back
Top Bottom