Prof. Tibaijuka: Chato haina sifa kuwa Mkoa
Mimi niliwahi kusema hili kuwa Chato haina HADHI kuwa Mkoa. Leo ninamuunga mkono Prof. Tibaijuka kuwa Chato haina hadhi kuwa Mkoa. Kwa nini tunaharibu kodi za wananchi kuunda Mkoa wa Chato. Pili, Kisesa, Katoro hazina hadhi ya kuwa Wilaya. Tuachane na upendeleo aliotaka kuonyesha Rais wa Awamu ya Tano.
 
Idadi ya watu wangapi inaunda mkoa?
Fafanua zaidi kuhusu kigezo cha eneo na rasilimali.
Mkoa hauanzishwi kwa kufuata vigezo alivyovitoa bali ni idadi ya wakazi, eneo na rasilimari. Watu wanawaza mji wa Chato tu badala ya kuunganisha eneo zima yaani kuanzia Kankonko hadi Karagwe ukijumuisha na hiyo Chato na pori la Burigi
 
Kwa nini jina la mkoa liitwe Chato??? Kwa nini mkoa usiitwe Biharamulo au kakonko au Nyakanazi?? Kwa nini jina la mkoa mpya liitwe Chato? Na kwa nini makao makuu yawe Chato? Hii ndiyo hoja ya msingi
Naomba tuache porojo pembeni. Tuchukueni mikoa 5 ya sasa tulinganishe na mkoa pendekezwa kwa vigezo vinane:

1. Area in aquarelle kilometres
2. Longest route in kilometres within the Region
3. Population
4. Number of District, Regional and Referral hospitals
5, Number of secondary schools
6, number of universities.
7. GDP
8. GDP PER CAPITA

Mikoa hii: SINGIDA, KILIMANJARO, KATAVI, LINDI, KUSINI PEMBA
 
Vigezo vya eneo kuwa mkoa ni vipi kwa miaka yote?
Hapana.
Labda wewe ndiye unayetaka nifikiri hivyo.

Kiufupi ni hivi:

Miaka yote pamekuwepo na taratibu zinazotumika na kupata vigezo vya kuianzisha hii mikoa.

Tukiondoa mifano michache, hasa ya hivi karibuni, utaratibu na vigezo hivyo ndivyo vinavyostahili kufuatwa bila kujali matakwa ya mtu au watu fulani wanaosukuma uamzi wao unaoegemea matakwa yao.

Hili ndilo tatizo nisilokubaliana nalo. Acha Chato ipitie kwenye taratibu hizo, na ikionekana vigezo vipo, basi na iwe mkoa.
 
Yupo sahihi, kuna mikoa kama Morogoro, Lindi na Ruvuma inasifa zaidi ya kugawanywa, Geita haina hata miaka 10 tangu igawanywe.........
 
Sumu aliyoieneza Hayati hapa Tanzania bado inatumaliza, yule mtu alikuwa wa hovyo sana
 
Vigezo vya eneo kuwa na hadhi ya mkoa ni vipi?
Mimi niliwahi kusema hili kuwa Chato haina HADHI kuwa Mkoa. Leo ninamuunga mkono Prof. Tibaijuka kuwa Chato haina hadhi kuwa Mkoa. Kwa nini tunaharibu kodi za wananchi kuunda Mkoa wa Chato. Pili, Kisesa, Katoro hazina hadhi ya kuwa Wilaya. Tuachane na upendeleo aliotaka kuonyesha Rais wa Awamu ya Tano.
 
Vigezo gani vinatumika kugawa eneo kuwa mkoa?
Yupo sahihi, kuna mikoa kama Morogoro, Lindi na Ruvuma inasifa zaidi ya kugawanywa, Geita haina hata miaka 10 tangu igawanywe.........
 
Kijiografia unaposema kuanzisha mkoa wa chato na chato iwe makao makuu ili kusogeza huduma karibu na wananchi huo ni uongo wa kupingwa kwa nguvu zote,

kama tuko serious Nyakanazi ndio eneo liliopo katikati ya Biharamulo, Ngara, Kakonko na Wilaya ya Bukombe,

kwanini isiundwe wilaya ya nyakanazi kisha tukatengeneza mkoa wa nyakananzi utakaoundwa na wilaya za Biharamulo, Nyakanazi, Ngara, Kakonko na Bukombe?

kwanini tunagangania chato kutoka kakonko na ngara kwenda chato bado ni mbali sana,


kama ajenda iliyopo ni kuwasogezea wananchi huduma za karibu basi uanzishwe mkoa wa nyakanazi ila kama kuna ajenda nyingine ya kijinga basi endeleeni na chato yenu
Hizo huduma kwanini zisishuke mpaka level ya kata, kata iwe na idara zote zilizoko manispaa, hiyo ndo njia ya kupelekwa huduma kwa wananchi, na itaongeza Anita za watumishi
 
Mkoa hauanzishwi kwa kufuata vigezo alivyovitoa bali ni idadi ya wakazi, eneo na rasilimari. Watu wanawaza mji wa Chato tu badala ya kuunganisha eneo zima yaani kuanzia Kankonko hadi Karagwe ukijumuisha na hiyo Chato na pori la Burigi
Hivi mkoa wa Katavi una wilaya ngapi, una watu wangapi?
 
Sasa sisi wa kakonko kigoma hatuyakubali kua sehemi ya mkoa wa chato sisi ni waha iweje mkatuchanganye na wasukuma kwa hiyo tuanze makujifunza tena kisukuma warah hatuwezi kukubali
Anzeni sasa kupaza sauti waha wenzangu
 
Kigezo kikubwa ni eneo la utawala kuwa kubwa, Mbeya iliizaa Songwe kwasababu ilikuwa na takribani wilaya 8..........
Hizo Wilaya zilitoka wapi? KUna watu ni wapuuzi tu! Wanaongeza mzigo kwa nchi na kusababisha watu kutengana. Hata wilaya zikifika 100, eneo ni constant, haliongezeki.
 
Maeneo yote ya utawala nchi hii ni makubwa.
Mkoa ukiwa na ukubwa kiasi gani ndio unagawanywa?
Kigezo kikubwa ni eneo la utawala kuwa kubwa, Mbeya iliizaa Songwe kwasababu ilikuwa na takribani wilaya 8..........
 
NB: Mods tafadhari msiunganishe huu uzi, ili kuwapa Nafasi wadau wachambue Vema content ya kile Alichokifafanua humu Humu.[emoji116]

Nanukuuu[emoji116]

"Ramani inaonyesha Chato ni sehemu ya Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera. Kiuhalisia. Na kihistoria. Mengine ni kulazimishalazimisha tu.

Naendelea kusisitiza hakuna hoja yoyote ya kiuchumi kuunda mkoa wa Chato. La sivyo basi tuelimishwe.

Ila kama mnapenda siasa za upendeleo wa sehemu fulani ama kwa kuwa mkubwa aliwahi kuzaliwa pale au mtu apewe nafasi kwa sababu ni mtoto wa kiongozi endeleeni kuwabebesha wananchi mizigo ya kulipa kodi kusudi wateule wajichane. Period.

Kwanza ikumbukwe Mkoa wa Geita ulianzishwa kusudi Chato iwe Makao Makuu. Ikakosa vigezo. Geita mjini ikaonekana ndiyo yenye sifa za kuwa Makao Makuu ya Mkoa mpya wa Geita. Hii ilikuwa 2010. Sasa 11 years later Chato ati ina vigezo kuwa Makao Makuu ya Mkoa wake wenyewe? Are we serious with our development? Really? Na Rais wetu mpendwa SSH tunataka kweli kumtwisha zigo la kuamua jambo hili na controversy zake? Elimu haina mwisho. Mimi kama kuna vigezo naomba viorodheshwe. Labda ndiye sina taarifa. Ila so far Hoja ya kuwaletea maendeleo Kakonko, Biharamulo, Ngara na Muleba inayokatwa vipande ninazikataa. Mkoa unaweza kuleta maendeleo gani kwa Wilaya yake wakati Mkoa unategemea bajeti ya Serikali Kuu. Mkoa una mapato gani zaidi ya kutumia kodi? Lets be serious. Maendeleo yanatokana na uwekezaji na uwezeshaji kwa wananchi. Siyo watumishi wa Serikali tena baadhi bila maadili wanaweza kuishia kuwabugudhi wananchi badala ya kuwa msaada.


Njia pekee kumuenzi Hayati Magufuli ni kurekebisha mambo ambayo kama binadamu hakufanya vizuri. Mengine yote ni ubinafsi. Na kufifisha sifa zake katika historia ya nchi hii. Tumuache apumzike.

Miundombinu iliyowekwa Chato siyo kigezo kuunda mkoa hapo. Tuikamilishe na kuitafutia matumizi mbadala ya kitaifa. Mfano Airport ya Chato inaweza kufanywa Hub ya kilimo cha contract floriculture na horticulture...(kilimo mkataba cha maua na mboga) ili tuwe na ndege za mizigo kuja kubeba. Na maziwa .

Hospitali ya Kanda Chato.... naomba tutathmini kwanza maendeleo ya hospitali ya Mloganzila. State of the Art buildings only 40km away from Dar City Centre na Muhimbili. Mojawapo ya mafanikio makubwa ya Awamu ya nne. Lakini Angalia changamoto zake. Uhaba wa madaktari hadi leo. Sasa hao specialist doctors watakaokubali kuishi Chato mtawalipa fedha kiasi gani?. A hospital is not just buildings. Its manpower resources and the economy surrounding it. Katika dhana ya mipango miji na maendeleo ya makazi lazima vigezo vyote hivyo kuangaliwa. Kwa uelewa wangu Chato haina vigezo. Tusidanganyane."

"Iwapo nia ni kuunda mkoa unaosogeza huduma jirani na wananchi ni busara mkoa huu kuundwa kwa kuweka makao makuu Biharamulo.

Hara hivyo sioni maana/mantiki ya wakazi wa wilaya za Ngara na Kakonko kuvuka wilaya ya Biharamulo wakienda Chato ambayo ni wilaya itakayokuwa pembeni mwa mkoa huu mpya.

Mkoa huu badala ya kunufaisha wakazi wake wengi, utawaumiza.

Pia sioni manufaa atakayoyapata mkazi wa Buseresere na Katoro kwa kuwa ataongeza umbali wa kwenda makao makuu ya mkoa.

Hata hivyo nashauri serikali badala ya kuwaza kuongeza mikoa, ijikite kupunguza ukubwa wa vijiji na kata.
Hili liende sambamba na kuwarahisishia utendaji wa kazi zao viongozi wa vijiji na kata kwa kuwapa usafiri, vifaa vya kazi kama kompyuta mpakato, simu zinazoweza kupata matukio [picha] vema.

Hapa Ngara kwenye kata ya Muganza, umbali kutoka Kitongoji cha Nyakafandi hadi makao makuu ya Kijiji chao cha Mukubu ni km.15.
Kutoka kitongoji hicho hadi makao makuu ya kata ni zaidi ya km.30.

Mtendaji wa kata na kijiji hawana usafiri wowote.
Huko hakuna umeme.
Wangeweza kusaidiwa kupewa umeme wa jua kwenye ofisi zao ili wachaji simu zao ambazo Kwa sehemu kubwa zinafanya kazi za ofisi.

Wananchi hatuna hitaji la mikoa na wilaya.
Tunahitaji zaidi huduma bora za vijiji na kata.

Ikumbukwe miaka michache iliyopita ukubwa wa vitongoji uliongezwa badala ya kupunguzwa. Kuna sehemu mitaa/vitongoji vitatu viliungwa kuwa kimoja.
Mzigo uliongezeka."
 
Hayo Mambo ya the so called 'Sukuma gang' ni hatari...machafuko huwa yanaanzia kwa kauli Kama hizi za ubaguzi..
Sukuma gang lipo na itachukua muda sana kupotea ....sasa bado wanajinamizi la mwendazake baada 2025 labda litayeyuka
 
Back
Top Bottom