Kijiografia unaposema kuanzisha mkoa wa chato na chato iwe makao makuu ili kusogeza huduma karibu na wananchi huo ni uongo wa kupingwa kwa nguvu zote,
kama tuko serious Nyakanazi ndio eneo liliopo katikati ya Biharamulo, Ngara, Kakonko na Wilaya ya Bukombe,
kwanini isiundwe wilaya ya nyakanazi kisha tukatengeneza mkoa wa nyakananzi utakaoundwa na wilaya za Biharamulo, Nyakanazi, Ngara, Kakonko na Bukombe?
kwanini tunagangania chato kutoka kakonko na ngara kwenda chato bado ni mbali sana,
kama ajenda iliyopo ni kuwasogezea wananchi huduma za karibu basi uanzishwe mkoa wa nyakanazi ila kama kuna ajenda nyingine ya kijinga basi endeleeni na chato yenu