Bora umeleta ushahidi, JAMAA alitaka kutupotosha hapa
 
Sipingani na mwenyekwao, billionea kashasema na hafuti.
 
Acha utoto
 
Weka sawa hapo kwenye asilimia 15, ikiwa mkoa inabidi uwe na wakazi asilimia 15 ya wakazi wa nchi, maana yake nchi nzima itabidi iwe na mikoa 6 tu ! Hichi kigezo hakipo sawa
 
Suala siyo kigezo au vingine. Umejiuliza Mkoa wa Katavi una watu wangapi?, eneo kiasi gani? Wilaya zipo 3 tu! Tunachojadili hapa hakifuatwi! Katavi ni mkoa ambao idadi ni kama wilaya mbili tu, ~laki6 tu!
 
Inawezekana ukaitwa mkoa wa chato lakini makao makuu ya wilaya pendekezwa si vizuri yawe chato. Sehemu hii imekuwa na changamoto za kiulinzi, ujambazi nk. Kuna ukanda wa misitu nk. Katika kuhakikisha linakuwa na usalama mkoa ungefaa. Lakini ningependekeza patafutwe makao makuu ya mkoa. Ukitoka ngara kwenda chato siyo saw a. Pia bihalamulo, kakonko, na bukombe. Makao makuu yawe Nyakanazi au lusahunga.
 
Vigezo vya eneo kuwa mkoa ni vipi kwa miaka yote?
Ni swali halali, ambalo sina nafasi ya kulijibu wakati huu, lakini ninajuwa ukiweka juhudi kidogo tu kutafuta taarifa hiyo utapata jibu.

Tayari hata kwenye mada hii hii, baadhi yake vimekwishatajwa.
 
Nani asiyeogopa njaa?, nani asiyeogopa kufilisiwa? Nani asiyeogopa kesi za kubambikiwa? Nani asiyeogopa kifo? Msiwatupie lawama watu wanapo pata wasaa wa kutoa maoni yao waache watoe...leo Ikulu wote wanavaa barakoa, unadhan kipindi kile waliogopa nini...? Ni kwamba hawakuwa na la kusemea sasa hivi wana pa kusemea acha watu waseme
 
Weka sawa hapo kwenye asilimia 15, ikiwa mkoa inabidi uwe na wakazi asilimia 15 ya wakazi wa nchi, maana yake nchi nzima itabidi iwe na mikoa 6 tu ! Hichi kigezo hakipo sawa
Huyu jamaa hajui hesabu, PERIOD.
 
Mkuu fanya favour kama una audio yake
 
Legacy ya prof. Tiba ni kupanda kwa kodi ya ardhi
 


Nakumbuka mwaka 1988 PM wa wakati huo Mzee Jaji Warioba akiwa Njombe kwenye ziara ya Kiserikali, aliombwa Njombe iwe Mkoa, alijibu sawia kabisa na huyu Mama Prof. Tibaijuka kwamba wananjombe wasililie mkoa walilie maboresho ya huduma kwakuwa gharama zitakazotumika kulipa viongozi na matumizi ya ofisi zao ni bora vitumike kuboresha huduma za muhimu.
 
Huyu Mama Prof. Tibaijuka ukimwambia aelezee ni kitu gani aliifanyia Tanzania for being International Figure atakupa maelezo kibao lakini hatakuonesha tangible things. Sana sana ametuachia msemo wa "Hela ya mboga"!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…