Prof. Tibaijuka: Chato haina sifa kuwa Mkoa
"Katika mazishi Wazee Chato walimuomba Rais Samia mkoa wakidai ni ahadi ya mtangulizi wake.kwa hekima akasema ataangalia vigezo.Kama Mbunge Mstaafu jirani Muleba Kusini najua vigezo havipo.Wazo halitekelezeki. Wazee jirani na sisi naamini tutapewa nafasi kushauri"@AnnaTibaijuka
Chato tayari ni mkoa wananchi kupitia madiwani wao wameshamaliza kutoa mawazo yao na wengi wameshapendekeza wilaya za mkoa wao sasa huyo Prof. alikuwa wapi wakati wa kutoa maoni? Haturudi nyuma tunasonga mbele. Tarehe 14/10/2021 wakati wa sherehe za kuzima Mwenge hapa Chato tunategemea Rais wetu mpendwa Samia atangaze rasmi kuwa Chato ni mkoa. Sasa wasiotaka wajiandae kisaikorojia wasije wakafa na stress bure.
 
Kiukweli lipo tatizo la kufikirika,ni Bora kuongeza halmashauri na kupandisha hadhi palipo na vigezo, ofisi ya RC Haina impact kubwa kwa ustawi wa Jamii. Kwa dunia ya leo mawasiliano hata wazo la kuhamia Dodoma halina tija Bora fungu like lingetumika boresha sector kilimo, SGR ingepata mizigo ya kutosha mbeleni.
Jiandae kisaikorojia tarehe 14/10/2021.
 
Mama pumzika zako makongo Dar ya huko waachie wana Chato na Mama Mkoa Geita wameshakubali .....acha iwe utaambiwa ya kuambiwa wilaya mojawapo au 2 Kagera itamegwa kwenda Chato....pambana na wajukuu mama awamu 6 hii sukuma gang wanalia huko legacy ......ya kulazimishia
Sisi wana Kagera tunaimiss Kagera ya zamani na wilaya zake zote
 
Watu wameingia vitani tena.

Sasa hivi wanagombea kama Chato iwe mkoa ama la. Ndani kabisa ya wahusika wa huu ugomvi ni walewale wa 'legacy' na 'yule hana legacy yoyote'

Kwa urahisi zaidi nasema ni upuuzi unaendelea. Huu ni ushindani bado wa kupimana kama marehemu alikua au hakua sahihi, cha kufurahisha ni kwamba pande zote hazijui na hazitaki kujua sifa za eneo kua mkoa.

Watanzania tupo kwenye mtego, watu hawataki kusonga mbele wameganda zama iliyopita na kuna dhihaka kwa waliobaki huko.

Ni upuuzi unaendelea.
 
Ajira zinajileta kuanzia post ya mkuu wa mkoa na watumishi wote wa mkoa yaani RPC, RTO, makatibu n.k alafu zinapingwa na wenye opportunities wenyewe.

Sikusemei Tibajoka, we ushakula mboga za bilions! Huhitaji mboga tena!
 
Hiyo Bukoba wakati inapewa hadhi ya makao makuu ya mkoa ilikuwa ni pori tu lakini leo ni mji mkubwa.

Mama Tibaijuka wala asiwe na hofu Chato itajengeka kadri muda unavyokwenda.

Chato haina sifa wala vigezo vya kua mkoa, aidha si kipaumbele kwa sasa. Kama airport acha waendelee kuanikia mpunga.
 
Back
Top Bottom