Prof. Tibaijuka: Chato haina sifa kuwa Mkoa
Ramani inaonyesha Chato ni sehemu ya Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera. Kiuhalisia. Na kihistoria. Mengine ni kulazimishalazimisha tu.
Naendelea kusisitiza hakuna hoja yoyote ya kiuchumi kuunda mkoa wa Chato. La sivyo basi tuelimishwe.

Ila kama mnapenda siasa za upendeleo wa sehemu fulani ama kwa kuwa mkubwa aliwahi kuzaliwa pale au mtu apewe nafasi kwa sababu ni mtoto wa kiongozi endeleeni kuwabebesha wananchi mizigo ya kulipa kodi kusudi wateule wajichane

Njia pekee kumuenzi Hayati Magufuli ni kurekebisha mambo ambayo kama binadamu hakufanya vizuri. Mengine yote ni ubinafsi. Na kufifisha sifa zake katika historia ya nchi hii. Tumuache apumzike

Miundombinu iliyowekwa Chato siyo kigezo kuunda mkoa hapo. Tuikamilishe na kuitafutia matumizi mbadala ya kitaifa. Mfano Airport ya Chato inaweza kufanywa Hub ya kilimo cha contract floriculture na horticulture...ili tuwe na ndege za mizigo kuja kubeba. Na maziwa

Katika dhana ya mipango miji na maendeleo ya makazi lazima vigezo vyote hivyo kuangaliwa. Kwa uelewa wangu Chato haina vigezo. Tusidanganyane.

Hospitali ya Kanda Chato.... naomba tutathmini kwanza maendeleo ya hospitali ya Mloganzila. State of the Art buildings only 40km away from Dar City Centre na Muhimbili. Mojawapo ya mafanikio makubwa ya Awamu ya nne. Lakini Angalia changamoto zake.

Mloganzila Uhaba wa madaktari hadi leo. Sasa hao specialist doctors watakaokubali kuishi Chato mtawalipa fedha kiasi gani?. A hospital is not just buildings. Its manpower resources and the economy surrounding it.

Mkoa una mapato gani zaidi ya kutumia kodi? Lets be serious. Maendeleo yanatokana na uwekezaji na uwezeshaji kwa wananchi. Siyo watumishi wa Serikali tena baadhi bila maadili wanaweza kuishia kuwabugudhi wananchi badala ya kuwa msaada.

Sasa 11 years later Chato ati ina vigezo kuwa Makao Makuu ya Mkoa wake wenyewe? Are we serious with our development? Really? Na Rais wetu mpendwa Samia tunataka kweli kumtwisha zigo la kuamua jambo hili na controversy zake? Elimu haina mwisho.

Prof Anna Tibaijuka

My Take

Mnashangaza mno, mbona hamkusema wakati Meko akiwa hai?tuungane kudai katiba mpya mtake msitake hamko huru mpaka mtu hayupo ndio mnaongea mnajichora mno,mjipunguzia heshima.

Madiwani wengi ni darasa la 7 unategemea waonge nn cha maana km waliwekwa kimkakati wakati wa uchaguz, na wanamadaraka makubwa tu kwenye baraza lao.
Hatuwez vuna samaki nchi kavu.
 
"Katika mazishi Wazee Chato walimuomba Rais Samia mkoa wakidai ni ahadi ya mtangulizi wake.kwa hekima akasema ataangalia vigezo.Kama Mbunge Mstaafu jirani Muleba Kusini najua vigezo havipo.Wazo halitekelezeki. Wazee jirani na sisi naamini tutapewa nafasi kushauri"Anna Tibaijuka....
Maneno haya yaliyojaa hekima hakika yanatoka kwenye kinywa cha Prof. Tibaijuka ninayemfahamu ... Yule aliyekuwa mkuu wa UN Habitat kule Kenya. Naamini amerudia enzi zake. Naunga mkono 100%.
 
Chato tayari ni mkoa wananchi kupitia madiwani wao wameshamaliza kutoa mawazo yao na wengi wameshapendekeza wilaya za mkoa wao sasa huyo Prof. alikuwa wapi wakati wa kutoa maoni? Haturudi nyuma tunasonga mbele. Tarehe 14/10/2021 wakati wa sherehe za kuzima Mwenge hapa Chato tunategemea Rais wetu mpendwa Samia atangaze rasmi kuwa Chato ni mkoa. Sasa wasiotaka wajiandae kisaikorojia wasije wakafa na stress bure.
Hao madiwani wanawaamulia mpaka wananchi wa mikoa mingine?Kigoma na Kagera haziwezi kuamuliwa mambo yake ya kiutawaka na madiwani wa mkoa mwingine.Kama inawapendeza Sana kuwa na mkoa wa Chato basi muuite mkoa wa Geita uwe mkoa wa Chato.

Mambo ya kuchukua wilaya zingine Ili kulazimisha sifa ni siasa za kidikteta kabisa.Kwanza hivyo vitu vyote vilivyojengwa Chato vinahudumia watu wangapi?
 
Hiyo Bukoba wakati inapewa hadhi ya makao makuu ya mkoa ilikuwa ni pori tu lakini leo ni mji mkubwa.

Mama Tibaijuka wala asiwe na hofu Chato itajengeka kadri muda unavyokwenda.
Inshu sio kujengeka, kuna vigezo vingi tu haikidhi, yaani kutoka geita hadi chato ni kama km 100!!eti na penyewe pawe mkoa?!!
 
hilo halina ubishi, ni kweli kabisa chato bado haijafikia hadhi ya kupewa mkoa. labda baada ya miaka 15 sio hivi karibuni.
kwa sasa tunataka kupoteza tu rasilimali za taifa letu ambalo bado lina changamoto lukuki za kiuchumi, tusiamue mambo kwa mihemuko na jazba.
 
Chato tayari ni mkoa wananchi kupitia madiwani wao wameshamaliza kutoa mawazo yao na wengi wameshapendekeza wilaya za mkoa wao sasa huyo Prof. alikuwa wapi wakati wa kutoa maoni? Haturudi nyuma tunasonga mbele. Tarehe 14/10/2021 wakati wa sherehe za kuzima Mwenge hapa Chato tunategemea Rais wetu mpendwa Samia atangaze rasmi kuwa Chato ni mkoa. Sasa wasiotaka wajiandae kisaikorojia wasije wakafa na stress bure.
Wasimege ardhi za mikoa ya watu, tuta hasi. Wabaki na chato yenyewe km mkoa
 
Mpango huu upo kitambo, ulikuwa unaongelewa kwa sauti ya chini, sasa wamelipuka rasmi... Nimeanza kusikia tangu Chato ilipomegwa kutoka Biharamlo na muasisi mwendazake.
Mbona mwendazake alipokuwepo walikuwa wame mute sahv ndiyo wanaongea

Ova
 
Kwanza marehemu Jiwe alivyoingia madarakani alikataa kuongeza mikoa mipya na wilaya imekuaje tena nyie fisiemu .
 
Hiyo Bukoba wakati inapewa hadhi ya makao makuu ya mkoa ilikuwa ni pori tu lakini leo ni mji mkubwa.

Mama Tibaijuka wala asiwe na hofu Chato itajengeka kadri muda unavyokwenda.
Mlidekezwa sana nyie !!! Hakuna kitu chato ni wilaya tuuu !!!
 
Huwa najiuliza JPM asinge itwa na Mungu hii inchi sijui ingekuwaje jamani!!!alikuwa ni kiongozi mbinafsi kuwahi kutokea Tanzania!??? Yan watanzania tunalakujifunza hapa kwenye chaguzi zijazo !! Sio kila MTU anafaa kuwa kiongozi ngazi ya URais ni hatari sana!!!
Hivi kila anaepewa mamlaka akisema atoe upendeleo kwao nchi ingekuwaje!??
Butiama mkoa
Msoga mko
Lupaso mkoa
Mkuranga mkoa he!???
Tutafika kweli!??
 
Back
Top Bottom