Ramani inaonyesha Chato ni sehemu ya Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera. Kiuhalisia. Na kihistoria. Mengine ni kulazimishalazimisha tu.
Naendelea kusisitiza hakuna hoja yoyote ya kiuchumi kuunda mkoa wa Chato. La sivyo basi tuelimishwe.
Ila kama mnapenda siasa za upendeleo wa sehemu fulani ama kwa kuwa mkubwa aliwahi kuzaliwa pale au mtu apewe nafasi kwa sababu ni mtoto wa kiongozi endeleeni kuwabebesha wananchi mizigo ya kulipa kodi kusudi wateule wajichane
Njia pekee kumuenzi Hayati Magufuli ni kurekebisha mambo ambayo kama binadamu hakufanya vizuri. Mengine yote ni ubinafsi. Na kufifisha sifa zake katika historia ya nchi hii. Tumuache apumzike
Miundombinu iliyowekwa Chato siyo kigezo kuunda mkoa hapo. Tuikamilishe na kuitafutia matumizi mbadala ya kitaifa. Mfano Airport ya Chato inaweza kufanywa Hub ya kilimo cha contract floriculture na horticulture...ili tuwe na ndege za mizigo kuja kubeba. Na maziwa
Katika dhana ya mipango miji na maendeleo ya makazi lazima vigezo vyote hivyo kuangaliwa. Kwa uelewa wangu Chato haina vigezo. Tusidanganyane.
Hospitali ya Kanda Chato.... naomba tutathmini kwanza maendeleo ya hospitali ya Mloganzila. State of the Art buildings only 40km away from Dar City Centre na Muhimbili. Mojawapo ya mafanikio makubwa ya Awamu ya nne. Lakini Angalia changamoto zake.
Mloganzila Uhaba wa madaktari hadi leo. Sasa hao specialist doctors watakaokubali kuishi Chato mtawalipa fedha kiasi gani?. A hospital is not just buildings. Its manpower resources and the economy surrounding it.
Mkoa una mapato gani zaidi ya kutumia kodi? Lets be serious. Maendeleo yanatokana na uwekezaji na uwezeshaji kwa wananchi. Siyo watumishi wa Serikali tena baadhi bila maadili wanaweza kuishia kuwabugudhi wananchi badala ya kuwa msaada.
Sasa 11 years later Chato ati ina vigezo kuwa Makao Makuu ya Mkoa wake wenyewe? Are we serious with our development? Really? Na Rais wetu mpendwa Samia tunataka kweli kumtwisha zigo la kuamua jambo hili na controversy zake? Elimu haina mwisho.
Prof Anna Tibaijuka
My Take
Mnashangaza mno, mbona hamkusema wakati Meko akiwa hai?tuungane kudai katiba mpya mtake msitake hamko huru mpaka mtu hayupo ndio mnaongea mnajichora mno,mjipunguzia heshima.
Madiwani wengi ni darasa la 7 unategemea waonge nn cha maana km waliwekwa kimkakati wakati wa uchaguz, na wanamadaraka makubwa tu kwenye baraza lao.
Hatuwez vuna samaki nchi kavu.