Mwanazuoni na Waziri wa zamani, Profesa Anna Tibaijuka, amebainisha kuwa nchi haiwezi kupata utulivu wa kweli wa kisiasa ikiwa hakuna maridhiano ya dhati, huku akisisitiza kuwa kuendelea kusalia gerezani kwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, hakuna afya kwa ustawi wa taifa.
"Na nchi haiwezi kutulia kama hakuna maridhiano. Mtu kama Lissu anaendelea kuwa gerezani. Mimi nasema kabisa kwamba haina afya. Hiyo haiwezi kuwa kwa maslahi ya wao. Kwa sababu gani? Kwa sababu yule ni kiongozi. Akija hapa, ndio sasa watu wanaona kwamba hilo tumelimaliza. Sasa tunakuja kwenye yale yaliyojiri yaliyotusibu, mambo makubwa, mahafa makubwa, msiba mkubwa. Hakuna hata mmoja wetu mwenye uwezo wa kurudisha gurudumu."