Profesa Assad aliumia sana kuvuliwa u-CAG. Mpaka leo namwona bado ana chuki kubwa sana. Tatizo ni nini?

Ndugai ni profesa?
Ana professional ipi kuishawishi ama kuipa miongozo nchi?

Anacho kifanya Assad ni kuwa anaitendea haki elimu yake, anaitendea mema nchi yake na vizazi vijavyo. Kasoro yake ni moja tu, hajafunguka vyakutosha anayo takikana kuyasema.
 
Kichuguu,
Kwa kutamka maneno hayo ya Assad wewe yanakuhusu vipi?
Unadhani kakuambia wewe?

Unadhani wewe ndiye unaestahili kumjibu?
Hayanihusu mimi na wala hayaniongezei au kunipunguzia chochote kwenye maisha yangu. Ila yanatoa ushahidi kujibu mada iliyoandikwa hapa na aliyeianzisha kuwa Assad bado ana kinyongo.

Assad badala ya kustaafu na kuanza kufanya shughuli za kitaaluma kila anapopata nafasi amekuwa analalamikia mambo ya uteuzi yaliyopita ambayo hawezi kuyabadadili tena. Utafikiri maisha yake yalikuwa ni u-CAG tu; nilitegemea awe anatumia muda huu kueneza alivyochangia kuendeleza taaluma yake kuliko kulalamikia kukosa uteuzi. Anadai kuwa aliondolewa kinyume cha Katiba ilihali Katiba inasema wazi kuwa CAG atahudumu kwa kipindi cha miaka mitano; anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine cha miaka mitano lakini asizidi miaka kumi kwenye nafasi ile. Anakuwa kama siyo msomi anayelewa maana ya ya katiba; ni kama alipoteuliwa alidhani kuwa atadumu automatically miaka kumi bila kuguswa !.
 
Mbona Mzee Ludovick naye huwa anaongea pia, sema akiongea Assad mnaona anachuki?

Yule Mzee alifanyiwa hila sana.
 
Kichuguu,
Kuna kitu hukijui kuhusu mafunzo ya Waislam.
Sisi tumefunzwa kutodhulumu wala tusikubali kudhulumiwa.

Ikiwa dhulma ipo katika jamii njia mojawapo ni kumfahamisha dhalim kuwa anadhulumu na anaedhulumiwa kuikataa hiyo dhulma.

Mimi nimeandika kitabu cha political history ya Tanganyika kuondoa dhulma iliyokuwapo ya kujaribu kufuta historia ya Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Matokeo yake waliokuwa hawajui dhulma hii leo wanajua.
Huu ndiyo mwendo wetu.
 
Hiyo CV umeirudia mara kadhaa ukidhani ni kubwa sana bila hata kuangalia scholarship content yake.

Consultancy report ni sehemu ndogo sana ya scholarship kwani ni matumizi ya standard knowledge katika kutoa jawabu ya swala lililopo mezani. Ingekuwa kila consultancy report ni sifa kuu ya scholarship ya mtu basi consultant engineers wote duniani wangekuwa na sifa zaidi ya Assad kwani ndiyo kazi zao za kila siku.

Uandishi wa vitabu kwa kufanya compilation ya information ambayo tayari ipo duniani ila kwa kutumia ama lugha rahisi au kwa kuipangilia vinginevyo pia ni sehemu ndogo tu ya scholarship.

Scholarship inapimwa kwa contribution ya new knowledge, ambayo inaweza kufanywa kwa kutumia papers au monographs ambapo content yote ni mpya. Vitabu ulivyoonyesha hapo vyote ni compilation ya known information na wala havifikii sifa ya kuwa research monograph.

Iwapo Assad angewa ni scholar mkubwa kama unavyota kuaminisha umma, asingekaa kuwa Senior Lecturer wa UDSM kwa miaka 11 katika institution ambayo hupandisha vyeo kila baada ya miaka mitatu, na kutumia miaka 10 kupata doctorate kutokea Masters degree. Yeye ni mtu wa kawaida tu.
 
Hakuna dini inayofundisha kudhulumu au kukubali kudhulumiwa. Usigeuze mada kuwa mambo ya dini, ambayo ndiyo taaluma yako. Issue hapa ni behavior ya Assad baada ya kukosa utezu wa kipndi cha pili.
 
Mbona Mzee Ludovick naye huwa anaongea pia, sema akiongea Assad mnaona anachuki?

Yule Mzee alifanyiwa hila sana.
Ludovik huwa anaongea mambo yanahohusu uendeshaji wa ofisi ya CAG kwa jumla, huwa haongei mambo ya yeye kudhulumiwa cheo au kuunganisha ofisi ya CAG na yeye mwenyewe binafsi kwa nia ya ama kujisafisha au kutoa lawama.
 
Mi nadhani mambo ya Ngoswe mwachie Ngoswe. Wewe ukinionesha tusi nililomtukana Ustaadhi wangu Assad hapo nitamuomba msamaha. Hakuna tusi hata moja. Pengine naye aliposema wafanyakazi wa Umma asilimia kubwa ni wajinga alikuwa anatukana watu? Ni mbaya kujivika usemaji kwa mtu ambaye huwa anaropoka wakati mwingine. Mimi ni mfanyakazi wa Umma. Sasa je ni seme alinitukana? Tujivike Utetevu panapofaa.
 
Mradi mbovu wa Magufuli ulikuwa wa Chato tu. Lakini mingine yote tunafurahia matunda yake. Wanaosema alikuwa fisadi wanashindwa kuonesha Ufisadi wake.... Mpaka leo.
 
Marajio gani zaidi wakati katiba inamtaka baada ya kustaafu asitumike tena kwenye public service! Ndio maana hata Otouh hajawahi kuteuliwa kwenye nafasi yoyote tangu alipostaafu, sana sana akajianzishia taasisi yake ya WAJIBU.
 
Professor Assad mwaya endelea kuongea sababu huwa unaongelea mambo yenye hoja za kuweza kuleta manufaa ya watu wote wa Taifa hili.
 
Wewe Komeo Tumia Akili hata za Kuazima Prof Assad sio mdogo kama unavyomdhania Mlidanganywa na yule Jamaa yenu baada ya Kuumbuliwa UFISADI wake mlimwamini huyo Mzee ni ngazi kubwa sana Kama humjui Uliza

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
ALIYEUMIA NI MAGUFULI KUUMBULIWA UFISADI WAKE kwa Hasira akamtoa hugo Mzee UCAG

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
umewahi kuichngulia CV yake? ipo humu tafuta uone shuguli ile afuu uongee
 
umewahi kuichngulia CV yake? ipo humu tafuta uone shuguli ile afuu uongee

CV haisemi chochote kila mtu anaweza kuandila na kuiremba CV anavyotaka na ndio maana kuna interviews, IQ aptitude tests n.k. kabla ya kukubaliwa kazi, hivyo kwangu mimi jinsi tu anavyoongea, tabia yake inanifanya niamini kabisa hana credentials au hazitoshi yeye kumpa hizo sifa mnazompa, na yes overrated, kama mtu kama Zito Kabwe ni“mtaalamu wa uchumi“ Tanzania ambaye kila mtu anamsikiliza wakati hana credentials zozote za Uchumi basi kila kitu kinawezekana Tanzania.

One tip, siku zote ukiona mtu anajifanya ni mtaalamu wa kila kitu basi ujue hajabobea kwenye fani yoyote ile kwa hali ya kawaida yeye mambo ya Katiba yanamuhusu nini ? Hiyo ni fani ya Wanasheria, ulishamsikia kwa mfano S.Muhongo akiongea ? Huwa anaongelea fani yake tu huwezi msikia akiongelea mambo ya Katiba hata siku moja, …
 
Anaweka rekodi sawa kuwa yule hakuwa kiongozi bali mtu muovu aliyekamata madaraka. Sasa anataka kuhakikisha kosa kama lile halirudiwi. Na kwa taarifa yako mpaka Profesa hajamsema dhalimu vizuri, anatakiwa azidishe sauti.
ili anedelee kuonekana ni mzee wa hovyo zaidi.

vijana wa sasa sampuli ya akina mwijaku hamjui kusitiri wazee,si ajabu wanafunzi wake,watoto wake,na hata vijana wake wengine wa karibu wanampigia makofi kwamba anatumia elimu yake vyema.

huyu si imani aliyo nayo,umri wala elimu aliyo nayo vinampa nafasi ya kuwa mtu wa kumtaja taja marehemu,ni dalili ya kujaribu kutibu maumivu aliyo nayo,tunajua viongozi wana mapungufu ila sasa anazidisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…