TANZIA Profesa Gaudence Mpangala afariki dunia baada ya kuugua ghafla

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Amepoteza uhai akipata matibabu Jijini Dodoma alfajiri ya leo.

Akifundisha Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa miaka mingi kabla ya kuhamia Iringa kwenye Chuo Kikuu cha Ruaha

Mpangala.jpg

Profesa wa Chuo Kikuu Katoliki Ruaha (RUCU) mkoani Iringa, Gaudence Mpangala amefariki dunia jijini Dodoma leo asubuhi Alhamisi Februari 4, 2021 baada ya kuugua ghafla.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo mjukuu wa msomi huyo, Andrew Mpangala amesema, “babu alikuwa Dodoma kikazi lakini leo kati ya saa 2 na saa 3 asubuhi akiwa katika safari kuelekea kwenye kikao alijisikia vibaya na kukimbizwa hospitali na ilivyofika saa tano akafariki dunia.”

Amesema mara ya mwisho kuwasiliana na babu yake ilikuwa jana na alimuagiza amtumie taarifa mbalimbali alizotakiwa kuzifuata Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kisha azitume Dodoma.

“Leo asubuhi nikapiga simu yake akapokea dereva wake ambaye aliniambia babu hali yake sio nzuri na amekimbizwa hospitalini. Pia dereva akaniambia hakuna mtu wetu wa karibu Dodoma ili aende kumuangalia mzee,” amesema.

Profesa Mpangala alikuwa mchambuzi wa masuala mbalimbali hasa ya siasa.

Andrew amesema mwili utapelekwa chuo cha RUCU kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho na baada ya hapo utapelekwa Dar es Salaam.
 
Pana haja ya kumwambia mtu fulani na vibaraka wake kuwa kwa hili big NO!

Hadi wafe wangapi? Hadi afe nani?

Itoshe kusema kwamba this is too much.

Sasa basi!

RIP Profesa Mpangala.
 
Back
Top Bottom