Profesa Kabudi: Trilioni 360 za makinikia haikuwa kodi sahihi, Nilikosea kutumia neno “Jalala”

Profesa Kabudi: Trilioni 360 za makinikia haikuwa kodi sahihi, Nilikosea kutumia neno “Jalala”

Mbogi

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2021
Posts
803
Reaction score
997
Kauli hii ya Profesa Kabudi inadhihirisha kuwa Lissu alikuwa sahihi Sana kwa sababu hata kama ni mbinu za kutaka mjadala, kwa wasomi kama maprofesa kutumia mbinu ya uongo "ulio dhahiri" kiasi hiki ulikuwa ni upungufu wa weledi.

Labda tuwasikie Wataalam wa daplomasia ya uchumi waje watufafanulie mbinu hii ya "Uongo mkubwa wa dhahiri" kama Lissu alivyokuwa "Profesorial Rubbish".

======

F7CB78F5-D1DA-4F09-A5F4-BE65BF0CB989.jpeg

  • Asema zilikuwa mbinu za majadiliano, ataja tishio la Acacia
  • Afafanua suala hilo limekwisha, atamtafuta mwigulu amweleze
  • Atamba uamzi ule umeleta heshima, faida kubwa kwa nchi
  • Asema alikosea kutumia neno jalala, asisitiza kibiblia ni sahihi.

Nukuu za Prof. Palamagamba Kabudi kwenye gazeti la leo la Jamhuri, Oktoba 4, 2022


=============


Mpatanishi Mkuu wa Scrikali (Chief Government Negotiator) Profesa Palamagamba Kabudi amesema Dola Bilioni 190 za kimarekani sawa na Tsh Trilioni 360 walizotakiwa kulipa kampuni ya Acacia, Julai 2017 kama kodi, malimbikizo na faini ya ukwepaji kodi, hakikuwa kiwango sahihi

Kabudi, aliyeteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mpatanishi Mkuu wa Serikali baada ya kutenguliwa uwaziri wa Katiba na Sheria, Januari, 2022 ameliambia Gazeti la JAMHURI mwishoni mwa wiki kuwa serikali ilifahamu tangu mwanzo kuwa kiwango hicho cha Dola bilioni 190 ambazo wakati huo zilikuwa sawa na Sh trilioni 360 kilikuwa hakilipiki.

"Jamani mtu yeyote anayejua, ile haikuwa kodi halali, ilikuwa ni kodi inayobishaniwa. Kwani watu wangapi mmetoa "assessment' (makadirio) ya kodi halafu mnakaa chini? Sasa nikasema siku nyingine nikipata nafasi na nikipata ruhusa, nita-share na wewe, na siyo siri, kwa sababu hata sasa wamekwishalipa ile installment (mkupuo) ya pili ya zile milioni 300.

"Lakini kuna faida nyingine nyingi ambazo tuliingia nazo kwenye mkataba... na ule mkataba sikusaini mimi, ulisainiwa na Waziri wa Madini, Dotto Biteko, mimi nilichokuwa nimekisaini kilikuwa kinaitwa Agreement of Undertaking (Makubaliano ya Utekelezaji), lakini yote, ningependa siku moja nikupe details (taarifa) zote kwa sababu ule mkataba sivo siri. Mimi nasoma JAMHURI kila siku," amesema.

Amesema kati ya mambo ambayo nchi katika Kiswahili ni uandishi wa kutumia lugha ya Kiswahili nchini, ila utaalamu huo umesalia katika JAMHURI.

"Unajua bahati mbaya nilikuwa nasema hata leo, umepoteza ladha ya uandishi wa Kiswahili, sasa miongoni mwa watu ninaopenda kusoma ni safu ya SITANII [unayoandika Balile], sasa mtu ambaye hajajua tamathali atasema, 'huyu anaandika nini?”

"Lakini mimi ninachokipenda ni ile aina ya lugha, kwa hiyo nashukuru na nikija Dar es Salaam nitakutafuta ili tukamilishane mawazo katika mambo yatakayotusaidia kujenga.

Lakini mambo mengine mimi hapana, kwa sababu ni vizuri kuona watu wanavyotafsirivitu. "Namtafuta Mwigulu (Waziri wa Fedha) nimwambie kuwa ile ilikuwa ni kodi inayobishaniwa. Na wao pia walitupeleka
kwenye ICSD (Kituo cha Kimataifa cha Kusuluhisha Migogoro) na wenzetu wakawa wanasema mtashitakiwa, mtafilisiwa.

"Unajua hizo trilioni zilipigwa baada ya wao kuwa wamepeleka mashitaka makubwa ICSD ya kudai close to two billion US dollars (karibu dola bilioni 2 za Marekani), sasa vitu vingine huwezi kuvieleza kwa sababu hizo ni mbinu za negotiations (upatanishi).

“Ukivieleza utavuruga, lakini ulichosema ni kweli... wewe hiyo kodi utaitoa wapi? Inazidi GDP za nchi zote, halafu nikasema huyu bwana kweli hatanii," amesema Kabudi.

Amesema tangu mwanzo walijua kuwa kiasi hiki hakilipiki ila walitumia kiwango hicho kama mbinu za majadiliano na upatanishi.

Ameliambia JAMHURI kuwa kwa vyovyote iwavyo, katika mgogoro kati ya Acacia na serikali, Tanzania iliibuka na ushindi na kwa masilahi mapana ya biashara hata Acacia walipata ushindi kwa kufanya biashara inayokubalika kwa pande zote mbili.

"Mimi nasoma JAMHURI kila ikitoka, sasa huko nyuma uliandika kitu nikakaa kimya, lakini cha jana nimekisomaa, nikatafakari, nikasema hebu nirudi kwa Balile niongee naye," amesema Kabudi.

Amesema kabla ya mgogoro huu, Tanzania haikuwahi kupata kitita cha Dola milioni 300 sawa na Sh bilioni 700, ambapo Acacia mwaka 2019 walitoa Dola milioni 100 kwa mpigo na wameendelea kutoa gawio mwaka hadi mwaka bila kuacha.

Huku akisisitiza kuwa hata mwaka huu serikali imepokea fedha nzuri tu kutoka kwenye madini, akaongeza kuwa nchi imepata hisa asilimia 16, inapata mgawo wa asilimia 50 ya faida inayopata Kampuni ya Twiga ambayo ni tanzu, inayomilikiwa kwa ubia kati ya Tanzania (16%) na Barrick (84%), uwazi umeongezeka kila kinachofanywa kinaonekana.

Ameongeza kuwa kuna faida kubwa na Tanzania imekuwa mfano kwa mataifa mengi ya Afrika ambayo sasa yanaiga.

Kabudi amesisitiza kuwa mgogoro wa Acacia/Barrick ulikwisha Oktoba, 2019, hivyo waliruhusiwa kusafirisha makinikia yaliyokuwa yamezuiwa bandarini, wakaanza kulipa kodi kwa mujibu wa makubaliano na deni la Dola bilioni 190 likafutwa katika vitabu vya serikali.

Kati ya fedha hizo, Dola bilioni 40 zilitajwa kuwa ni kodi iliyokwepwa na Dola bilioni 150 zilitajwa kuwa ni faini, malimbikizo na riba ya kukwepa kodi tangu mwaka 2000.

Katika kinachoonekana kuwa Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, ana hoja mahususi aliyoishikilia, Novemba 5, 2021 ikiwa ni miezi sita baada ya kifo cha Rais Dk. John Magufuli, alihoji zilipo Sh trilioni 360 ambazo Serikali ya Awamu ya Tano iliwadai Acacia na kupeleka shauri kwenye Baraza la Kodi....
 
F7CB78F5-D1DA-4F09-A5F4-BE65BF0CB989.jpeg


  • Asema zilikuwa mbinu za majadiliano, ataja tishio la Acacia
  • Afafanua suala hilo limekwisha, atamtafuta mwigulu amweleze
  • Atamba uamzi ule umeleta heshima, faida kubwa kwa nchi
  • Asema alikosea kutumia neno jalala, asisitiza kibiblia ni sahihi.

Nukuu za Prof. Palamagamba Kabudi kwenye gazeti la leo la Jamhuri, Oktoba 4, 2022

=====

Kumbukumbu: Picha inaonesha Prof. Kabudi akishuhudia utiaji saini wa makubaliano ya kulipwa kodi trilioni 360 za makinikia Mbele ya Hayati JPM Ikulu, Dar es salaam

37F60E50-615B-4160-AD31-0B319BBFAF08.jpeg
 
Yuko sahihi, ni sawa na mfanyabiashara anayeweka cha juu ili ukija kulia akupunguzie bei bado usishuke chini ya target yake, muhimu ijulikane hicho kilichopatikana hapo hata kama kidogo, bado hakikutegemewa kupatikana.
 
Yuko sahihi, ni sawa na mfanyabiashara anayeweka cha juu ili ukija kulia akupunguzie bei bado usishuke chini ya target yake, muhimu ingependeza atuambie wao walipata ngapi hasa anaposisitiza ule uamuzi umeleta heshima kwa nchi.
Kutoka trillion 360 mpaka bilioni 700! Hakyamama tumeonekana vilaza namba 1 duniani
 
Kwa hiyo zile Noah zetu kila mtanzania ilikuwa janjajanja ya majadiliano?

Kumbe ukihitaji fanya majadiliano na mtu ya kubadilishana ie bidhaa kwa fedha au huduma kwa fedha unapaswa kuweka makadililio ambayo hujawahi kuwa nayo ama kuyapata na kile unaenda kufanya?

Kwa mazingira haya kamwe hatutakuja kuendelea maana vitu vya msingi tunaleta masiharaa hivi.

Hongera kwake TAML
 
Yuko sahihi, ni sawa na mfanyabiashara anayeweka cha juu ili ukija kulia akupunguzie bei bado usishuke chini ya target yake, muhimu ingependeza atuambie wao walipata ngapi hasa anaposisitiza ule uamuzi umeleta heshima kwa nchi.
Kibongo bongo ni sawa, kama vile mtu anauza kitu elf 25 mwisho unanunua elfu 3.
Si tulipewa zile 700b? Na hisa 16%, umesahau?
 
Huu ni uthibitisho kwamba JPM alikuwa anaendesha nchi kwa ulaghai, utapeli, uzandiki, na propaganda. Alizungukwa na waongo na wanafiki, na yeye alipenda uongo na unafiki.

Ajabu mpaka Leo Kuna mijitu mijinga inaendelea kuimba ujinga wa awamu ya tano. Anajifanya kupambana na ufisadi huku pembeni ana Makonda, na Sabaya. Tenda za kujenga stiglers, sub contractors wote ni vikampuni vyake, pamoja na inner cycle yake. Wenye vikampuni hivyo ndio wanapiga mdomo sana kuhusu mradi, kwa sababu wamekaa pale wananyonya nchi. Akina polepole, ana kikampuni pale kina tenda, kinafiki anajifanya mzalendo kuupenda mradi, nyuma ya pazia ana kampuni inakula Hela zetu pale stiglers.

Stendi ya Magufuli Mbezi, kikampuni chake, kimevuta Hela, na stendi hakijaimaliza, inabidi Hela itafutwe kwingine, masoko mapya nchi nzima, stendi ya nyamhongolo, barabara za Kanda ya ziwa via mayanga construction, barabara ya kigoma inayojemgwa na nyanza road, kampuni ambayo ana hisa, imejengwa miaka zaidi ya 20 haiishi huku akiwa bize kufutia ukandarasi kampuni za wenzake.

Wafanyakazi anatimua timua huku wale wa Chato wakiajiriwa bila interview na kujazwa serikalini.

Uwanja wa ndege Chato, imejenga kampuni yake, hospitali ya Kanda Chato...endless list.

Hakuna utawala mchafu kama wa awamu ya JPM.

Miradi mingi ya ujenzi wa madaraja na barabara ni kampuni za JPM lakini alikuwa anawapachika wachina.

Oohh masikini na wanyonge, jitu limejaza matrilioni kwenye akaunti za Siri, mfugale anaulizwa hizi Hela vipi, badala ya kujibu, na yeye anakufa

Sasa hao jamaa wa mgodi wakaidai bilioni 700 ambayo waliilipa kupitia professorial rubbish
 
Yuko sahihi, ni sawa na mfanyabiashara anayeweka cha juu ili ukija kulia akupunguzie bei bado usishuke chini ya target yake, muhimu ingependeza atuambie wao walipata ngapi hasa anaposisitiza ule uamuzi umeleta heshima kwa nchi.
Kwa kawaida kodi hukokotolewa (calculated) sasa cha juu inawekwaje kwenye calculation?! Siyo kama bei ya duka la Mangi ambapo bei hutamkwa tu.
 
Yuko sahihi, ni sawa na mfanyabiashara anayeweka cha juu ili ukija kulia akupunguzie bei bado usishuke chini ya target yake, muhimu ingependeza atuambie wao walipata ngapi hasa anaposisitiza ule uamuzi umeleta heshima kwa nchi.
Huyo atakuwa ni mfanyabiara mjinga. Cha juu ni lazima kiwe within the target ya bei yako. La siyo utafukuza wateja wako. Sasa hii ya Trillion 360 to Billion 700 itakuwa ni akili ya jalalani tu.
 
Back
Top Bottom