Profesa Kabudi: Trilioni 360 za makinikia haikuwa kodi sahihi, Nilikosea kutumia neno “Jalala”

Profesa Kabudi: Trilioni 360 za makinikia haikuwa kodi sahihi, Nilikosea kutumia neno “Jalala”

20210320_205744.jpg
200 (22).gif
 
Kibongo bongo ni sawa, kama vile mtu anauza kitu elf 25 mwisho unanunua elfu 3.
Si tulipewa zile 700b? Na hisa 16%, umesahau?
Kutoka trillion 360 mpaka bilioni 700! Hakyamama tumeonekana vilaza namba 1 duniani
Baada ya majadiliano, ilithibitika hatuwadai hata dola 1 Acacia ila Barrick wanapendekeza Acacia atupatie msaada wa dola milioni 120 maana milioni 180 wanatudai. Hivyo kutoka ile dola milioni 300 waliyoipendekeza Acacia kutusaidia, ukiondoa dola milioni 180 wanayotudai Acacia, inabakia dola milioni 120 tu.
 
Kwanini uonekane kilaza ikiwa hata hiyo bil 700 hukutegemea kuipata?

Mimi nakuona wewe ndie kilaza.
Sasa mkuu kama kweli tulikuwa na haki ya kupata kiasi halisi cha kodi yetu palikuwa na ulazima gani wa kuwalaghai wananchi kwamba tunawadai trilioni 360 hali ya kuwa tunajua ukweli?

Huoni kwa kauli ya professor Kabudi tayari imeleta kutoaminika kwa serikali ya awamu ya 5?

Inaonekana awamu ya 5 ilikuwa ni serikali ya propaganda.

Ukimdai mtu bilioni 700 mwambie ninachokidai hiki hapa kilipe sio kuweka cha juu hadi mwananchi wa kawaida anakuwa na wasiwasi juu ya deni tunalodai.
 
Tukisema mwendazake aliitumia TRA kusingizia watu madeni mnakataa... huo ushahidi sasa?
Kodi inatumia Sheria, haiamuliwi from nowhere.
Bado Kabudi ameongeza upuuzi juu ya upuuzi kwenye utetezi wake.
Huyo jamaa alikuwa anakusingizia Kodi halafu anafyeka Hela zote kwenye akaunti, ulikuwa utawala wa kishetani kabisa
 
Sasa mkuu kama kweli tulikuwa na haki ya kupata kiasi halisi cha kodi yetu palikuwa na ulazima gani wa kuwalaghai wananchi kwamba tunawadai trilioni 360 hali ya kuwa tunajua ukweli....
Usijichoshe kufikiria mbali, hapo kilichofanyika ni kucheza na maneno tu, mimi binafsi siamini kama kweli tulikuwa tunawadai wazungu hata mia, kama ingekuwa hivyo, wale wangeshafukuzwa siku nyingi sana kwa kukiuka masharti ya mkataba, ni sound za kina Kabudi kwa wazungu ndio zilifanya wakapata hizo pesa, ndio maana nawapongeza kwa sound zao.
 
Yuko sahihi, ni sawa na mfanyabiashara anayeweka cha juu ili ukija kulia akupunguzie bei bado usishuke chini ya target yake, muhimu ijulikane hicho kilichopatikana hapo hata kama kidogo, bado hakikutegemewa kupatikana.
Target ya trillion 360 ili kupata billion 700 (something less than 6% out of 100%) ambazo haziwezi kuwa enforced- Just a favor? Ni ujinga mtupu kwa macho ya mwenye akili.
 
"One of the things that cost our country is the fact that, the smart and patriotic people/heroes in this country have only platforms to express their views and ideas but without power to implement them; whereas, the less intelligent and unpatriotic ones, have not only platforms to express their views and ideas, but also have power to implement their ideas even if those ideas are sometimes detrimental to the country and bad enough, they can do it with impunity.
 
Kauli hii ya Profesa Kabudi inadhihirisha kuwa Lissu alikuwa sahihi Sana kwa sababu hata kama ni mbinu za kutaka mjadala, kwa wasomi kama maprofesa kutumia mbinu ya uongo "ulio dhahiri" kiasi hiki ulikuwa ni upungufu wa weledi...
Kama Professor alishiriki kuudanganya umma wa Watanzania,

Basi afungiwe jiwe kubwa na ATOSWE baharini.
 
Huu ntindo haukurithiwa na TRA kweli? Maana makodi kwa wafanyabiashara yalitaradadi.
 
Back
Top Bottom