Profesa Kabudi: Trilioni 360 za makinikia haikuwa kodi sahihi, Nilikosea kutumia neno “Jalala”

Profesa Kabudi: Trilioni 360 za makinikia haikuwa kodi sahihi, Nilikosea kutumia neno “Jalala”

Kauli hii ya Prof Kabudi inadhihirisha kuwa Lissu alikuwa sahihi Sana kwa sababu hata kama ni mbinu za kutaka mjadala, kwa wasomi kama maprofesa kutumia mbinu ya uongo "ulio dhahiri" kiasi hiki ulikuwa ni upungufu wa weledi.

Labda tuwasikie Wataalam wa daplomasia ya uchumi waje watufafanulie mbinu hii ya "Uongo mkubwa wa dhahiri" kama Lissu alivyokuwa "Profesorial Rubbish".
Wacha kumbagaza professor
 
Mtu yeyote mwenye akili hata kidogo aliona hilo. Bajeti yenu Trilioni 30 sijui kwa mwaka. Uchumi wenu wote hata Trilioni 150 hazifiki.

Halafu unaidai kampuni kodi ya 360 trilioni. Hela ambayo hata kampuni yenyewe haina thamani hiyo. Ulikuwa ujuha ujuha tu.
 
Kwa kawaida kodi hukokotolewa (calculated) sasa cha juu inawekwaje kwenye calculation?! Siyo kama bei ya duka la Mangi ambapo bei hutamkwa tu.
Itambulike tu, hii biashara mwanzo haikuwepo kabisa, ilikuja kama njia ya kutupoza kutokana na kupigwa kwenye mikataba, na nikiangalia vile tunavyopigwa na wazungu kwenye mikataba yetu, bado naona waliochofanya hawakukosea.
 
Huyo atakuwa ni mfanyabiara mjinga. Cha juu ni lazima kiwe within the target ya bei yako. La siyo utafukuza wateja wako. Sasa hii ya Trillion 360 to Billion 700 itakuwa ni akili ya jalalani tu.
Madini sio kama maandazi.
 
Hivi kuna kuwa na shida gani wakinyamaza, kukaa kimya kunaficha mengi sana, ujinga na upumbavu hufichika kwenye ukimya.

Sasa kama huyu ndie profesa, mtu ambaye ameelimika kwa ngazi ya juu kuliko zote katika elimu anaonekana mwenye koso na mimi nilie ishia darasa la saba, ipi faida ya kuwepo kwa wasomi katika taifa hili?
 
I agree, 360 trillions Tshs ilikuwa mbinu za majadiliano, ili waweze kupata walicho plan kwenye majadiliano yale, kumbuka Barrick Gold yale ni mabeberu haswa ya dunia hii, yaani majambazi makuu, sasa mbinu za majadiliano lazima ziwe kubwa mno.

Mie pia nilijua tu Barrick hawawezi lipa tshs 360 tril. Ila badala yake tulipata kishika uchumba $ 300 mil plus tumepata 16% ya Acacia shares (umiliki), pia watu wetu wako ktk management ya Acacia, bado udhibiti umekuwa mkubwa sana sasa hivi..

Walau tumepata kitu kikubwa, nakubaliana na Prof. Kabudi, though ana umaskini wa akili na mali, he has intellectual arrogance kubwa sana Prof . huyu.
 
Yuko sahihi, ni sawa na mfanyabiashara anayeweka cha juu ili ukija kulia akupunguzie bei bado usishuke chini ya target yake, muhimu ijulikane hicho kilichopatikana hapo hata kama kidogo, bado hakikutegemewa kupatikana.
😂😂😂😂😂😂😂
Sukuma gang on the move
 
Vile mama alisema atawatumia kwa kazi MAALUMU, ndo sasa ameanza kuwatumia.

Lukuvi yuko reserve anasubiria muda wa kutumiwa .
 
Back
Top Bottom