Profesa Kabudi: Trilioni 360 za makinikia haikuwa kodi sahihi, Nilikosea kutumia neno “Jalala”

"Collective Responsibility" maana yake si kudanganya.

In fact ukidanganya kwa mwamvuli wa "Collective Responsibility" kwa kufuata falsafa za The Nuremberg Trials, umekubali kosa na hukumu ya kosa inakufaa.

Huyu jamaa ameshaweka precedent ya disputes zote za kodi za serikali ya Tanzania kuwekewa shaka kwamba "Hawa jamaa waongo waongo tu kuna waziri wao alishawahi kudanganya na kukubali kwamba kadanganya kama sehemu ya business tactics".

Yani hata kama kweli alidanganya kwa business tactics, kwa maslahi ya taifa, kukubali kwamba kadanganya kama business tactics ni kosa.
 

Hakuna kiongozi wa kuomba radhi ya namna hiyo huku Afrika, hasa inapochukuliwa kuomba radhi ni sawa na udhaifu. Tena ninashangaa Kabudi amewazaje hata kukiri kidogo uongo ule kwenye gazeti!

Ifahamike Kabudi ni baadhi ya watu tuliotambua uongo wao toka wakati ule, hadi tukawa tunashangaa aliwezaje kuwa shabiki wa uongo wa wazi vile na kiwango chake cha usomi. Nikikumbuka ule uzalendo uliosimikwa katika uongo wa wazi, kisha watu wenye heshima zao ikiwemo wasomi, viongozi wa dini nk wakawa wanakusanywa ikulu kwenda kupewa hadithi za uongo, na kwa bahati mbaya wakawa wanajitokeza kusifia ule utapeli! Pale ndio nilijuwa kiwango cha wajinga+ waoga tulionao nchini.
 
Kabudi muongo muongo halafu ana uongo wa kijinga tu.

Alituletea dawa ya Covid-19 kutoka Madagascar akataka kutuaminisha inaponya.

Watu wanauliza, na ile nayo ilikuwa ni mbinu?

Kaondoa credibility ndogo aliyobakisha.

 

Huu anaouita uongo Kabudi leo hii ni baada ya kuona ukweli unaanza kuongelewa wazi wazi, hivyo anaongea hivyo kama kujihami. Lakini wakati ule wa Magufuli walikuwa serious, maana uongo huo huo ndio ulitumika kupora fedha za wafanyabishara hapa nchini. Ni bahati tu hayo makampuni ya kimataifa yana ulinzi wa kimataifa, vinginevyo wangefulisiwa kwa hiki anachosema Kabudi kuwa ni mbinu ya kumzonga unayejadiliana naye ili ajae kwenye mtego wako.
 
Kabudi muongo muongo halafu ana uongo wa kijinga tu.

Alituletea dawa ya Covid-19 kutoka Madagascar akataka kutuaminisha inaponya.

Watu wanauliza, na ile nayo ilikuwa ni mbinu?

Kaondoa credibility ndogo aliyobakisha.


Ni kwakuwa bado CCM wako madarakani, lakini ilipaswa viongozi wote walioshirikiana na Magufuli kufanya uhalifu kinyume na sheria wawe lupango. Hili lingekuwa fundisho kwa watu wengine kutotii maagizo ya viongozi yaliyokinyume na sheria. Ni vyema hizi rekodi zikatunzwa ili utawala ukibadilika hata kama mtu kazeeke alipie uharamia wake.
 

Hakuna collective responsibility kwenye nia ovu. Hiyo ondoa.
 
Yuko sahihi, ni sawa na mfanyabiashara anayeweka cha juu ili ukija kulia akupunguzie bei bado usishuke chini ya target yake, muhimu ijulikane hicho kilichopatikana hapo hata kama kidogo, bado hakikutegemewa kupatikana.
Yuko sahihi wapi?Huwezi kuendesha nchi kama duka; pengine ndo maana hatuaminiki.
 
KUNA MTU ANAITWA "OLD MOSHI" KULE CLUB HOUSE..SASA NDO NIMEANZA KUMUAMINI MANENO YAKE😂😂😂😂
 
Siku nyingi sana sijaingia humu. Naona pamejaa madini
 
Watu waliandika nyuzi humu na kwenye vyombo vya habari hakukukosekana wasomi waliokwenda kuongeza intellectual weight kwenye hili. Bahati nzuri kwao hatuna utamaduni wa accountability kwa maneno yetu. Kesho wataandika na kuhojiwa kwenye media kama wasomi na hamna atakayewakumbusha haya.

Hivi akina Mzee Mwanakijiji na @Kilatha bado wapo humu?
 
Mimi naona kusema alitolewa jalalani hakumkosea Mungu bali alikikosea chuo alichosoma na kufanya kazi.Alimkosea Mungu siku alipomtaja marehemu Mulyankende "Mtukufu Mungu!!!
 
Kabudi baada ya kuzielewa akili za Mwendawazimu Jiwe... walipanga makampuni na wawekezaji wa kimataifa wakiwa na migogoro na Serikali basi watumie Mahakama zetu.. Na sio za kimataifa

Jiwe akabadili sheria ili aweze kuzibana makampuni ya kimataifa..

Bahati mbaya wengi walitaka kuondoka na pia wawekezaji wapya walistuka sana kuona hiyo sheria..
Baada ya miezi mitatu akaondoa hiyo sheria.. Bila hivyo kampuni zilikuwa zinaondoka nchini..
 
Kabudi aelewe TU kuwa hii nchi siyo soko la machinga Wala duka la mangi! Kodi ikikadiriwa kinachofuata ni malipo Kama utekelezaji na Kama mkadiriwa Kodi akiona hakutendewa haki anatakiwa arudi Kwa kamishna wa tra napo akishindwa anakwenda trat na trab! Yeye akubali TU kuwa hakutimiza wajibu wake vema na huenda aliambulia ka10%. Aache kutuona wajinga!
 
Anachokisema Prof. KABUDI ni kwamba HAKUZINGATIA kiapo cha "UADILIFU" na MISINGI yake chini ya Ibara 132 ya Katiba ya nchi. Amekiri KUVUNJA Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya 1995! Huku akifahamu, kwa mujibu wa Sheria ya "MAFAO YA VIONGOZI", anaweza POTEZA mafao yake yote!
 
Kiongozi, andiko lako kila ninapozidi kulisoma moyo unapata fadhaa. Tuombe sana MUNGU asitupitishe kwenye sintofahamu kama ya awamu ya tano. Athari zake mpaka leo zinaendelea kutuumiza. Umeandika kwa ukweli na haki.
UBARIKIWE.
 
Kabudi kwahiyo ni nani kati ya Magufuli na mwananchi ulimgeuza mpumbavu?
Huwezi kujua, maisha matamu ingawa siku hizi watu wanasema bia tamu!

Naona kabisa nafasi ya gazeti hilo la Jamhuri kwenye masuala ya kizalendo ipo wapi.

Hivi ni nani ananufaika na utoaji "Siri" hii iliyochapishwa na gazeti la Jamhuri? Tuanzie hapo kwanza.
 
tuwekee video ya maneno haya mimi sina imani na hayo maelezo ya gazeti moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…