Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
"Collective Responsibility" maana yake si kudanganya.Huenda ilikuwa katika utekelezaji wa 'collective responsibility'...ingekuwa vigumu na dhambi kutofautiana na serikali ambayo na wewe ni sehemu yake.
Kumtaka aombe radhi Sasa kwa makosa ya kipindi hicho ilihali bado wengine waliokuwa naye kwenye majadiliano ni watendaji wa serikali sio sawa ni kumuonea tu.
Nguruvi3 Tindo Kiranga zitto junior
Tuligeuzwa wote wapumbavuKabudi kwahiyo ni nani kati ya Magufuli na mwananchi ulimgeuza mpumbavu?
Tena Kabudi aliwahi kusema '' Degree yangu nimeazimwa, nikiitumia vibaya wataichukua''
Sijui analipi la kusema
Kabudi atoke mbele awaombe Watanzania radhi , aiombe familia ya Lisssu radhi na ajitoe katika kamati ya mikataba huko Ikulu kwasababu hafai na amepoteza heshima na uaminifu kwa umma.
Hata hizo bilioni 700 ni story tuu kwenye makaratasi, hawajapata hata senti tanoKutoka trillion 360 mpaka bilioni 700! Hakyamama tumeonekana vilaza namba 1 duniani
Kabudi muongo muongo halafu ana uongo wa kijinga tu.Hakuna kiongozi wa kuomba radhi ya namna hiyo huku Afrika, hasa inapochukuliwa kuomba radhi ni sawa na udhaifu. Tena ninashangaa Kabudi amewazaje hata kukiri kidogo uongo ule kwenye gazeti!
Ifahamike Kabudi ni baadhi ya watu tuliotambua uongo wao toka wakati ule, hadi tukawa tunashangaa aliwezaje kuwa shabiki wa uongo wa wazi vile na kiwango chake cha usomi. Nikikumbuka ule uzalendo uliosimikwa katika uongo wa wazi, kisha watu wenye heshima zao ikiwemo wasomi, viongozi wa dini nk wakawa wanakusanywa ikulu kwenda kupewa hadithi za uongo, na kwa bahati mbaya wakawa wanajitokeza kusifia ule utapeli! Pale ndio nilijuwa kiwango cha wajinga+ waoga tulionao nchini.
"Collective Responsibility" maana yake si kudanganya.
In fact ukidanganya kwa mwamvuli wa "Collective Responsibility" kwa kufuata falsafa za The Nuremberg Trials, umekubali kosa na hukumu ya kosa inakufaa.
Huyu jamaa ameshaweka precedent ya disputes zote za kodi za serikali ya Tanzania kuwekewa shaka kwamba "Hawa jamaa waongo waongo tu kuna waziri wao alishawahi kudanganya na kukubali kwamba kadanganya kama sehemu ya business tactics".
Yani hata kama kweli alidanganya kwa business tactics, kwa maslahi ya taifa, kukubali kwamba kadanganya kama business tactics ni kosa.
Kabudi muongo muongo halafu ana uongo wa kijinga tu.
Alituletea dawa ya Covid-19 kutoka Madagascar akataka kutuaminisha inaponya.
Watu wanauliza, na ile nayo ilikuwa ni mbinu?
Kaondoa credibility ndogo aliyobakisha.
Huenda ilikuwa katika utekelezaji wa 'collective responsibility'...ingekuwa vigumu na dhambi kutofautiana na serikali ambayo na wewe ni sehemu yake.
Kumtaka aombe radhi Sasa kwa makosa ya kipindi hicho ilihali bado wengine waliokuwa naye kwenye majadiliano ni watendaji wa serikali sio sawa ni kumuonea tu.
Nguruvi3 Tindo Kiranga zitto junior
Yuko sahihi wapi?Huwezi kuendesha nchi kama duka; pengine ndo maana hatuaminiki.Yuko sahihi, ni sawa na mfanyabiashara anayeweka cha juu ili ukija kulia akupunguzie bei bado usishuke chini ya target yake, muhimu ijulikane hicho kilichopatikana hapo hata kama kidogo, bado hakikutegemewa kupatikana.
Siku nyingi sana sijaingia humu. Naona pamejaa madiniHuu ni uthibitisho kwamba JPM alikuwa anaendesha nchi kwa ulaghai, utapeli, uzandiki, na propaganda. Alizungukwa na waongo na wanafiki, na yeye alipenda uongo na unafiki.
Ajabu mpaka Leo Kuna mijitu mijinga inaendelea kuimba ujinga wa awamu ya tano. Anajifanya kupambana na ufisadi huku pembeni ana Makonda, na Sabaya. Tenda za kujenga stiglers, sub contractors wote ni vikampuni vyake, pamoja na inner cycle yake. Wenye vikampuni hivyo ndio wanapiga mdomo sana kuhusu mradi, kwa sababu wamekaa pale wananyonya nchi. Akina polepole, ana kikampuni pale kina tenda, kinafiki anajifanya mzalendo kuupenda mradi, nyuma ya pazia ana kampuni inakula Hela zetu pale stiglers.
Stendi ya Magufuli Mbezi, kikampuni chake, kimevuta Hela, na stendi hakijaimaliza, inabidi Hela itafutwe kwingine, masoko mapya nchi nzima, stendi ya nyamhongolo, barabara za Kanda ya ziwa via mayanga construction, barabara ya kigoma inayojemgwa na nyanza road, kampuni ambayo ana hisa, imejengwa miaka zaidi ya 20 haiishi huku akiwa bize kufutia ukandarasi kampuni za wenzake.
Wafanyakazi anatimua timua huku wale wa Chato wakiajiriwa bila interview na kujazwa serikalini.
Uwanja wa ndege Chato, imejenga kampuni yake, hospitali ya Kanda Chato...endless list.
Hakuna utawala mchafu kama wa awamu ya JPM.
Miradi mingi ya ujenzi wa madaraja na barabara ni kampuni za JPM lakini alikuwa anawapachika wachina.
Oohh masikini na wanyonge, jitu limejaza matrilioni kwenye akaunti za Siri, mfugale anaulizwa hizi Hela vipi, badala ya kujibu, na yeye anakufa
Sasa hao jamaa wa mgodi wakaidai bilioni 700 ambayo waliilipa kupitia professorial rubbish
Kabudi baada ya kuzielewa akili za Mwendawazimu Jiwe... walipanga makampuni na wawekezaji wa kimataifa wakiwa na migogoro na Serikali basi watumie Mahakama zetu.. Na sio za kimataifaHuu anaouita uongo Kabudi leo hii ni baada ya kuona ukweli unaanza kuongelewa wazi wazi, hivyo anaongea hivyo kama kujihami. Lakini wakati ule wa Magufuli walikuwa serious, maana uongo huo huo ndio ulitumika kupora fedha za wafanyabishara hapa nchini. Ni bahati tu hayo makampuni ya kimataifa yana ulinzi wa kimataifa, vinginevyo wangefulisiwa kwa hiki anachosema Kabudi kuwa ni mbinu ya kumzonga unayejadiliana naye ili ajae kwenye mtego wako.
Anachokisema Prof. KABUDI ni kwamba HAKUZINGATIA kiapo cha "UADILIFU" na MISINGI yake chini ya Ibara 132 ya Katiba ya nchi. Amekiri KUVUNJA Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya 1995! Huku akifahamu, kwa mujibu wa Sheria ya "MAFAO YA VIONGOZI", anaweza POTEZA mafao yake yote!Kauli hii ya Profesa Kabudi inadhihirisha kuwa Lissu alikuwa sahihi Sana kwa sababu hata kama ni mbinu za kutaka mjadala, kwa wasomi kama maprofesa kutumia mbinu ya uongo "ulio dhahiri" kiasi hiki ulikuwa ni upungufu wa weledi.
Labda tuwasikie Wataalam wa daplomasia ya uchumi waje watufafanulie mbinu hii ya "Uongo mkubwa wa dhahiri" kama Lissu alivyokuwa "Profesorial Rubbish".
======
- Asema zilikuwa mbinu za majadiliano, ataja tishio la Acacia
- Afafanua suala hilo limekwisha, atamtafuta mwigulu amweleze
- Atamba uamzi ule umeleta heshima, faida kubwa kwa nchi
- Asema alikosea kutumia neno jalala, asisitiza kibiblia ni sahihi.
Nukuu za Prof. Palamagamba Kabudi kwenye gazeti la leo la Jamhuri, Oktoba 4, 2022
=============
Mpatanishi Mkuu wa Scrikali (Chief Government Negotiator) Profesa Palamagamba Kabudi amesema Dola Bilioni 190 za kimarekani sawa na Tsh Trilioni 360 walizotakiwa kulipa kampuni ya Acacia, Julai 2017 kama kodi, malimbikizo na faini ya ukwepaji kodi, hakikuwa kiwango sahihi
Kabudi, aliyeteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mpatanishi Mkuu wa Serikali baada ya kutenguliwa uwaziri wa Katiba na Sheria, Januari, 2022 ameliambia Gazeti la JAMHURI mwishoni mwa wiki kuwa serikali ilifahamu tangu mwanzo kuwa kiwango hicho cha Dola bilioni 190 ambazo wakati huo zilikuwa sawa na Sh trilioni 360 kilikuwa hakilipiki.
"Jamani mtu yeyote anayejua, ile haikuwa kodi halali, ilikuwa ni kodi inayobishaniwa. Kwani watu wangapi mmetoa "assessment' (makadirio) ya kodi halafu mnakaa chini? Sasa nikasema siku nyingine nikipata nafasi na nikipata ruhusa, nita-share na wewe, na siyo siri, kwa sababu hata sasa wamekwishalipa ile installment (mkupuo) ya pili ya zile milioni 300.
"Lakini kuna faida nyingine nyingi ambazo tuliingia nazo kwenye mkataba... na ule mkataba sikusaini mimi, ulisainiwa na Waziri wa Madini, Dotto Biteko, mimi nilichokuwa nimekisaini kilikuwa kinaitwa Agreement of Undertaking (Makubaliano ya Utekelezaji), lakini yote, ningependa siku moja nikupe details (taarifa) zote kwa sababu ule mkataba sivo siri. Mimi nasoma JAMHURI kila siku," amesema.
Amesema kati ya mambo ambayo nchi katika Kiswahili ni uandishi wa kutumia lugha ya Kiswahili nchini, ila utaalamu huo umesalia katika JAMHURI.
"Unajua bahati mbaya nilikuwa nasema hata leo, umepoteza ladha ya uandishi wa Kiswahili, sasa miongoni mwa watu ninaopenda kusoma ni safu ya SITANII [unayoandika Balile], sasa mtu ambaye hajajua tamathali atasema, 'huyu anaandika nini?”
"Lakini mimi ninachokipenda ni ile aina ya lugha, kwa hiyo nashukuru na nikija Dar es Salaam nitakutafuta ili tukamilishane mawazo katika mambo yatakayotusaidia kujenga.
Lakini mambo mengine mimi hapana, kwa sababu ni vizuri kuona watu wanavyotafsirivitu. "Namtafuta Mwigulu (Waziri wa Fedha) nimwambie kuwa ile ilikuwa ni kodi inayobishaniwa. Na wao pia walitupeleka
kwenye ICSD (Kituo cha Kimataifa cha Kusuluhisha Migogoro) na wenzetu wakawa wanasema mtashitakiwa, mtafilisiwa.
"Unajua hizo trilioni zilipigwa baada ya wao kuwa wamepeleka mashitaka makubwa ICSD ya kudai close to two billion US dollars (karibu dola bilioni 2 za Marekani), sasa vitu vingine huwezi kuvieleza kwa sababu hizo ni mbinu za negotiations (upatanishi).
“Ukivieleza utavuruga, lakini ulichosema ni kweli... wewe hiyo kodi utaitoa wapi? Inazidi GDP za nchi zote, halafu nikasema huyu bwana kweli hatanii," amesema Kabudi.
Amesema tangu mwanzo walijua kuwa kiasi hiki hakilipiki ila walitumia kiwango hicho kama mbinu za majadiliano na upatanishi.
Ameliambia JAMHURI kuwa kwa vyovyote iwavyo, katika mgogoro kati ya Acacia na serikali, Tanzania iliibuka na ushindi na kwa masilahi mapana ya biashara hata Acacia walipata ushindi kwa kufanya biashara inayokubalika kwa pande zote mbili.
"Mimi nasoma JAMHURI kila ikitoka, sasa huko nyuma uliandika kitu nikakaa kimya, lakini cha jana nimekisomaa, nikatafakari, nikasema hebu nirudi kwa Balile niongee naye," amesema Kabudi.
Amesema kabla ya mgogoro huu, Tanzania haikuwahi kupata kitita cha Dola milioni 300 sawa na Sh bilioni 700, ambapo Acacia mwaka 2019 walitoa Dola milioni 100 kwa mpigo na wameendelea kutoa gawio mwaka hadi mwaka bila kuacha.
Huku akisisitiza kuwa hata mwaka huu serikali imepokea fedha nzuri tu kutoka kwenye madini, akaongeza kuwa nchi imepata hisa asilimia 16, inapata mgawo wa asilimia 50 ya faida inayopata Kampuni ya Twiga ambayo ni tanzu, inayomilikiwa kwa ubia kati ya Tanzania (16%) na Barrick (84%), uwazi umeongezeka kila kinachofanywa kinaonekana.
Ameongeza kuwa kuna faida kubwa na Tanzania imekuwa mfano kwa mataifa mengi ya Afrika ambayo sasa yanaiga.
Kabudi amesisitiza kuwa mgogoro wa Acacia/Barrick ulikwisha Oktoba, 2019, hivyo waliruhusiwa kusafirisha makinikia yaliyokuwa yamezuiwa bandarini, wakaanza kulipa kodi kwa mujibu wa makubaliano na deni la Dola bilioni 190 likafutwa katika vitabu vya serikali.
Kati ya fedha hizo, Dola bilioni 40 zilitajwa kuwa ni kodi iliyokwepwa na Dola bilioni 150 zilitajwa kuwa ni faini, malimbikizo na riba ya kukwepa kodi tangu mwaka 2000.
Katika kinachoonekana kuwa Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, ana hoja mahususi aliyoishikilia, Novemba 5, 2021 ikiwa ni miezi sita baada ya kifo cha Rais Dk. John Magufuli, alihoji zilipo Sh trilioni 360 ambazo Serikali ya Awamu ya Tano iliwadai Acacia na kupeleka shauri kwenye Baraza la Kodi....
Huwezi kujua, maisha matamu ingawa siku hizi watu wanasema bia tamu!Kabudi kwahiyo ni nani kati ya Magufuli na mwananchi ulimgeuza mpumbavu?
tuwekee video ya maneno haya mimi sina imani na hayo maelezo ya gazeti moja.Kauli hii ya Profesa Kabudi inadhihirisha kuwa Lissu alikuwa sahihi Sana kwa sababu hata kama ni mbinu za kutaka mjadala, kwa wasomi kama maprofesa kutumia mbinu ya uongo "ulio dhahiri" kiasi hiki ulikuwa ni upungufu wa weledi.