Profesa Lipumba ashangazwa na Rais Samia kumuachia mtu aliyekula njama katika wizi wa shilingi zaidi ya bilion 300 za Escrow kwa kutoa bilion 26 tu

Profesa Lipumba ashangazwa na Rais Samia kumuachia mtu aliyekula njama katika wizi wa shilingi zaidi ya bilion 300 za Escrow kwa kutoa bilion 26 tu

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Akiongea na waandishi wa habari leo profesa Lipumba ameonyesha kushangazwa na hatua ya Rais Samia kumuachia huru mtu aliyekula njama za kukwapua zaidi ya shilingi bilion 350 za Escrow kwa kutakiwa kulipa shilingi bilion 26 tu, Profesa anahoji hizo pesa nyingine sasa zinakwenda wapi, na tutazipataje?

Akiongea kwa utulivu na kwa data, profesa Lipumba pamoja na kutambua baadhi ya mambo mazuri ambayo rais Samia ameyafanya ndani ya siku 100 za uongozi wake, Profesa Lipumba ameendelea kusisitiza kuwa Demokrasia ndiyio msingi wa uchumi shirikishi, kwamba huwezi kujenga uchumi shirikishi wenye kunufaisha wananchi bila demokrasia.

Profesa anasema kuwa licha ya rais Magufuli kufungia shughuli za kisiasa kwa madai hayohayo ya kukuza uchumi kwanza lakini takwimu zinaonyesha kuwa thamani yote ya pesa za uwekezaji nchini ilipungua kutoa zaidi ya dola bilion 2 mwaka 2015 hadi dola milion 800 tu mwaka 2019 tena kabla ya gonjwa la korona halijaikumba dunia, Profesa anahoji kuwa kama kuzuia shughuli halali za kisiasa ndiyo kukuza uwekezaji mbona basi uwekezaji ulishuka kipindi cha Magufuli?

Profesa akaendelea kusema kuwa uwekezaji ulishuka nchini kwa sababu Magufuli alikuwa haheshimu sheria, kitu ambacho Rais Samia amekionyesha kuwa naye atakuwa siyo mheshimu sheria baada ya kutoa tangazo la kuzuia shughuli halali za kisiasa kama zinavyoruhusiwa na sheria za nchi. Kutoheshimu sheria kunaua confidence ya wawekezaji na wenye mitaji yao!

Profesa Lipumba anasema kuna uwezekanao Wahafidhina ndani ya Chama cha Mapinduzi wanamshauri vibaya rais Samia ili asikutane na wapinzani na kumshawishi kuchukua hatua za kuvunja sheria kama hizi tunazoanza kuona akichukua.

Profesa anasema kuwa rais Samia anayo nafasi adhimu ya kukumbukwa kwa kuacha urathi (legacy) ya maana iwapo atawaachia wananchi katiba mpya, Profesa anasema kwamba kwamba hoja ya rais Samia kwamba tusubiri ajenge uchumi kwanza ndo tuzungumze habari za katiba ni ya kushangaza, ni ya kushangaza kwa sababu wao wanasema sisi tayari tuko katika uchumi wa kati, Profesa anahoji anasema au Samia anataka hadi tuwe uchumi wa juu ndo afikirie habari za katiba mpya?

Profesa Lipumba pia ametoa maoni yake pia kuhusu bajeti ya nchi, Amesema kwamba bajeti ya shilingi trilion 36 iliyosomwa bungeni haitekelezeki, anasema haoni means ambazo seriakli itaweza kupata fedha za kutosheleza bajeti hiyo

MY TAKE:
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Profesa ameongea mambo mazito sana leo na ni fact tupu!

1.Tunataka tujue ni nini hatma ya pesa za wananchi za Escrow, Habinder Seth ameachiwa , kwa nini kalipa bilion 26 tu, zilizobaki zitalipwa na nani? (By the way Profesa kasema Habinder Seth kalipa shilingi milioni 200 tu kwa hiyo hata hiyo bilioni 26 nayo ina question mark)

2. Bila Political reforms na economic reforms vikienda kwa pamoja rais Samia atashindwa kukidhi mahitaji ya wananchi, ajiandae ama kuwa dikteta kuzidi Magufuli ili kunyamazisha watu, au aonyeshe leadership kwa kuachana na wahafidhina ndani ya CCM wanaomshauri afuate njia zilizofeli za kutoheshimu sheria na kuminya haki za makundi mbali mbali ya kijamii

3. Samia kuendelea kukumbatia baraza la mawaziri la Magufuli na baadhi ya wateule wa Magufuli akidhani kuwa atawamudu kwa kuwa yeye ni rais, bila shaka ni ishara ya kuendeleza status quo, na kwa kuwa hawa ndiyo washauri wake wakubwa basi tutegemee mambo ya Kimagufulimagufuli yakirudi polepole maana hiyo ndiyo njia pekee wanayoijua ya kulinda vyeo vyao, hawawezi kumshauri awe fair kwa wapinzani wake hawa maana fairness inahitaji kujiamini na kujenga hoja za ushawishi mbele ya wananchi badala ya ujanjaujanja tuliouona katika miaka 5 iliyopita

4. Hii ya kumuachia mtu anayetuhumiwa kula njama za kuiba mabilioni ya fedha za wananchi, na ile tuliyoishuhudia kutoka kwa mtangulizi wa rais Samia ya kufunga watu kiuonevu ni Uthibitisho usioyumba kuwa wananchi tunahitaji katiba mpya ili tuweze kuondoa abuse hii ya mamlaka, kinyume cha hapo, kwa katiba hii hata ukiujenga uchumi ukawa kama Singapore bado inatoa mwanya mchwa kuutafuna kifisadi huku wakilindwa na katiba!
 
Hapa ndyo tutamuelewa Kigogo2014 na Lissu,Samia hana jipya kwa kuwa na yeye ni product ya wizi wa kura za October, 2020
Hata mimi nimeanza kuona kuwa kuna tatizo sehemu.
Hii ya kutaka kuendelea na mambo ya mwendazake ya kutoheshimu sheria huku akitoa excuse lame kabisa imenitia wasiwasi sana!
 
Na wale vigogo serikalini, taasisi za jamii, taasisi za imani, wabunge, maaskofu na marafiki waliofaidika na pesa za ESCROW walilipa kodi stahiki za mapato yao yote kwa TRA ikiwemo takrima waliyopokea ?

Kwa upande mwingine, mchanganuo linganifu wa ufanisi wa kodi kwa nchi za Afrika Mashariki unaonyesha kwamba, Tanzania iko nafasi ya tatu nyuma ya Kenya na Rwanda...
 
Profesa anasema kuwa licha ya rais Magufuli kufungia shughuli za kisiasa kwa madai hayohayo ya kukuza uchumi kwanza lakini takwimu zinaonyesha kuwa thamani yote ya pesa za uwekezaji nchini ilipungua kutoa zaidi ya dola bilion 2 mwaka 2015 hadi dola milion 800 tu mwaka 2019 tena kabla ya gonjwa la korona halijaikumba dunia, Profesa anahoji kuwa kama kuzuia shughuli halali za kisiasa ndiyo kukuza uwekezaji mbona basi uwekezaji ulishuka kipindi cha Magufuli?
Legacy ya Mwendawazimu imeua uchumi wetu. MATAGA mpo.
 
Nimemuelewa sana mzee lipumba.

Sasa hapa ilitakiwa wawepo watu wa kumsemea raisi wajibu hoja kwa hoja wanamchi tunaewa mbivu na mbichi.

Sio huyu anaongea alafu hoja inakuwa haijibiwi.

Ningekuwa mimi ndo samia nawapa teuzi hawa akina zito,mbowe,lipumba,lissu alafu nawachooraaa tuuuuu wasimamie sheria katika maeneo niliyowachagua
 
Hata mimi nimeanza kuona kuwa kuna tatizo sehemu.
Hii ya kutaka kuendelea na mambo ya mwendazake ya kutoheshimu sheria huku akitoa excuse lame kabisa imenitia wasiwasi sana!
Wakati mwingine wajanja wanaweza poteza ushahidi, ni vyema kuchukua kiasi cha bilioni hizo maana serikali inaweza kuishia kupoteza zote
 
Pamoja na maneno matamu ya Profesa Lipumba, naomba kumuuliza Prof. mbona hatukumuona akiyasema haya kumshauri Bwana Magufuli? PILI, naomba kujua wakati Prof. anakipokea chama chake kwa kuwapora wananchi na kujimilikisha, kilikuwa na hali gani?

Wabunge wangapi? na sasa chama hicho kipo wapi? Naomba Prof. anijuze kabla ya kutoka nje kuhangaika na kibanzi kilicho kakika macho ya wenzake, anatoaje maboriti yaliyo katika macho yake?
 
Shida ya Lipumba ni unafiki.Leo kaongea km Profesa halisi wa wa uchumi.Lakini wakimuwekea bahasha mezani tu anajitoa ufahamu wote mpaka mtu unajiuliza,Hivi huyu ndo Prof Lipumba au msukule wake?!!! Aache kubadilika badilika km kinyonga.
 
Ajabu eti Chadema wanafurahia na kushangilia akiachiwa Singa singa wa escrow.2

Kuna popote umeona tangazo la cdm kuhusu huyo Singasinga? Hata hivyo huyo Singasinga hiyo hela aliichukua bila ushirikiano na watu wa serikalini? Je wako wapi watendaji wa serikalini waliongia mkataba na Singasinga? Acheni kufanya watu wajinga.
 
Back
Top Bottom