Profesa Lipumba ashangazwa na Rais Samia kumuachia mtu aliyekula njama katika wizi wa shilingi zaidi ya bilion 300 za Escrow kwa kutoa bilion 26 tu

Mimi nashangaa watu humu wanamuona Lipumba ni mnafki na kigeugeu lakini sioni sifa hizo kupewa Lissu au Mbowe kwa kigeugeu cha kumpa fomu ya kugombea urais kwenye chama mtu ambaye miaka yote wamekuwa wakimtambua kama fisadi, na walishatoaga kauli kuhusu huyo mtu ambazo zinapingana na walichokuja kukifanya 2015.

Pamoja na yote hayo ila hukuti hao watu kuitwa wanafki,binafsi nashindwa kuelewa.
 
Lipumba alikataa uhuni wa Seif
 
Unajua maana ya kitu kinaitwa maridhiano....
au ww ni mtu wa visasi tu....
 
Prof Lipumba anatakiwa awashauri waanasheria wa serikali kupeleka ushahidi unaothibitisha kuwa Habinger Seth Ni mwizi wa pesa za escrow unless ni uonevu na dhuluma ya haki za kibinadamu kumuweka mtu Mahabusu miaka zaidi ya mitatu eti mnatafuta ushahidi.
Tunakwama wapi?

Mama Samia alisema kesi zisizokuwa na ushahidi Ni kufutilia mbali Kwasababu ndizo zinazoleta chuki katika jamii
 
Kwani Rais Samia ndiye aliyemuachia kigogo wa escrow au Mahakama?
 
Kweli kabisa, Angalia yule anamshauri rais eti viwanda vya nyungu vifichwe jeshini!, mwingine anamshauri Mama eti madeni ya mifuko ya jamii yageuzwe kuwa hati fungani na eti hiyo inakwenda kumaliza shida ya wastaafu kutolipwa kwa kuwa serikali imekopa fedha zao.
Na hao wengine eti katiba mpya isubiri uchumi ukue, vijana wapate ajira - sijui lini. Hawajui kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya democrasia na kukua kwa uchumi. Wengine eti katiba mpya si ilani ya CCM na haina bajeti - wanasahau kuwa hata uwanja wa ndege msalato hauna bajeti
 
Tangu alipowavuruga kwa kujiudhuru akaja kwa mabavu ya msajili wa vyama,hata aongee point vipi.Huwa namuunga mkono msukuma ambaye husema wasomi wanatuchanganya
 
profesa njaa tuu huyo hana lolote, zile bilioni tatu alizopewa na jakaya akasema anaacha siasa, zilipo karibia kukata na kuona upande wa znzbar cuf inakaribia kushinda akakimbilia zanzibar kuunga cuf mkono na akarudi tena kwenye siasa.

Huyu profesa ccm walimtumia sana, kibaraka wa ccm, huyu wa kupuuzwa tuu anatafuta ugali kwa mama. Yake hayaoni anaona yawenzake tuu.
 
Uko sawa, ila kama alilipa 26bn zilikuwa za nini?
 
hawa maprofesa wetu mungu anawona...huwa sometimes wanatuvuruga sana
 
Kwanza kabisa fedha za escrow sio za wananchi pesa ya wananchi ni kodi tu...kwa hiyo sio kweli kuwa bill 300 zote ni za wananchi
 
Hahahahahhah
siasa za Tanzania trust no one....wote wanahangaikia matumbo yao tu..hata mm nikipelekwa huko lazima nifanya hivyo...

only solution for all this ni kuwa na katiba mpya yenye kujitosholeza
 
Umetoka nje ya maada
 
Ajabu eti Chadema wanafurahia na kushangilia akiachiwa Singa singa wa escrow.2
Walichoshauri ni suala la upelelez umalizike hukumu itoke na sio kuwekwa mahabusu tu, je vp waliobeba jala kweny sandarusi? Ni bora kuliko wanaoshangilia singa kua uraiani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…