Profesa Lipumba ashangazwa na Rais Samia kumuachia mtu aliyekula njama katika wizi wa shilingi zaidi ya bilion 300 za Escrow kwa kutoa bilion 26 tu

Tuliwaambia JPM alikuwa mzalendo halisi na mtamkumbuka. Haya sasa mbona!??? Bi Mkubwa ajiuzulu tuu asingoje ilee 2025.

Ndugu punguza chuki zako kwa mama.. kumfananisha jpm na Mama samia ni kumkosea sana mama wa watu.. ndio kwanzaa ana siku 100 na kidogo sasa mnataka maendeleo gani ya haraka ivyo.. ipo siku mtamkubali huyu mama.


Na achaneni na RIP zenu hizo kila day, mara ohh tutamkumbuka baba, mara sijui nini!!! Hata mimi nirikua namkubali japo kuna mabaya na mazuri amefanya..


Mwishoe munakufuru kwa uyu mbaba aise.

Mwisho kabisa Mama samia ndio mzalendo, ana imani na huruma.
 
Hili la kigogo wa Escrow hata mimi najiuliza, analipa bilioni 26 kati ya bilioni 350 zilizobaki atalipa nani?
 
Shida ya Lipumba ni unafiki.Leo kaongea km Profesa halisi wa wa uchumi.Lakini wakimuwekea bahasha mezani tu anajitoa ufahamu wote mpaka mtu unajiuliza,Hivi huyu ndo Prof Lipumba au msukule wake?!!! Aache kubadilika badilika km kinyonga.
Umesahau na mbowe pia alilegaza paja mbele ya pesa zaowass mbona hukuwahi kushangaa
 
Hapana sio akina Seth, alichosema huyo atalipa b.26 zilizobaki atalipa nani? Kwa maana nyingine wasakwe waliogawiwa na wote warudishe mgao, je itawezekana?
 
Uongozi ni kuonyesha njia iliyonyooka ambayo wengine wanaweza wasiipenda kabisa. Ukishakuwa na kiongozi anayetaka kumfurahisha kila mtu, basi elewa kuwa hajui ni njia ipi anataka kuwaongoza watu wake.
 
Bora hizo 26B kuliko kumfunga tukakosa hata hicho kidogo, ESCROW kuna akina JK huko ndani ndiyo maana hakuna kesi zaidi ya utapeli tu.
 
Lipumba alikataa uhuni wa Seif

Sitaki kumtetea Lipumba hivyo wanavyomuona kuwa ni mnafki ila nashangaa kwamba kwanini na wengine pia waliyofanyaga unafki ila hawakuwahi kuitwa wanafki mpaka leo na bado wanaendelea kuaminiwa ila kwa Lipumba ni tofauti? 2015 kulifanyika unafki mkubwa sana watu walishuhudia kitu ambacho hawakuwahi kufikiri kama ingewezekana kufanyika ila watu walijilazimisha kuwaelewa Chadema kwa walichokifanya hawakuwaita wanafki ila Lipumba ndio kabaki kuitwa mnafki.
 
Sasa mkuu kama hakukuwa na "financial loss" inakuwaje wamdai kiasi kikubwa hivyo.
 
Hivi jamani kwanza tusahihishe kiswahili chetu na maana ya maneno tunayotumia. Huyu mtu anatuhumiwa kuiba au kula njama za kuiba? Kula njama haimaanishi kuwa alifanikiwa kuiba.
 
Kwenye suala la ESCROW ukitaka kusimamia haki kwa asilimia zote vigogo wa CCM na baadhi ya viongozi wa dini hakuna hata mmoja atakayesalimika, Magufuli mwenyewe pamoja na umwamba wake kwenye suala la ESCROW aliufyata mwenyewe zaidi ya kuishia kusema kuwa tuwaache wapumnzike wametufanyia mengi, yaani mengi ni pamoja na kutupiga kwenye ESCROW.
 
Achana na mambo ya chadema maana hayo maufisadi yote yalifanya ccm ikiwa madarakani,polisi wenu,takukuru ya kwenu,mahakama zenu na Dpp wenu.aya tunaomba matokeo ya kesi za ufisadi mlizofungua na hukumu zake.
 
Achana na mambo ya chadema maana hayo maufisadi yote yalifanya ccm ikiwa madarakani,polisi wenu,takukuru ya kwenu,mahakama zenu na Dpp wenu.aya tunaomba matokeo ya kesi za ufisadi mlizofungua na hukumu zake.
Kwanini niachane na mambo ya chadema Ni kwamba hutaki kujadili makosa ya chadema au vp?
 
Anashangaa nini sasa hajui ikulu iko Msoga?
Tudai tu Katiba mpya hakuna namna tena...enough is enough!
 
Hapana sio akina Seth, alichosema huyo atalipa b.26 zilizobaki atalipa nani? Kwa maana nyingine wasakwe waliogawiwa na wote warudishe mgao, je itawezekana?
Ninavyojua Singasinga dhamana yake ni mitambo mpaka akimaliza deni.

Fact ni kwamba siyo 350B yote ilikuwa ya TANESCO.
 
Rais SSS shikilia hapohapo! Kenge ametoka shimoni mchana kweupee baada ya njaa kutamalaki. Enzi za mwendazake hili jamaa lilikuwa jeuri alipokuwa anakula meza moja na JPM.
 
Rais SSH shikilia hapohapo. Kenge moja ametoka shimoni mchana kweupee baada njaa kuwa kali. Hili lipropesa lilikuwa likisifu mambo yote ya hayati kwa sababu alikuwa akila naye meza moja.
 
Sasa mkuu kama hakukuwa na "financial loss" inakuwaje wamdai kiasi kikubwa hivyo.
Fines

adhabu ya kosa la kula njama

hakuna hela iliyoliwa mazima

bali hela ililiwa njama

angeiba angeshtakiwa kuiba, sio kula njama
 
Prof baregu (hayati)

Alimfata lipumba nyumbani kwake akamuuliza profesa kulikoni ,nimerudi cuf naona kunawatu(maalim seif) ,anataka kuuvunja muungano..



Lipumba prof
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…