Profesa Makame Mbarawa anatushinda kumng'oa?

Barabara ya Kibaha Chalinze jamani ujenzi uanze kwa vitendo tuone.

Tumuenzi Magufuli kwa vitendo.
 
Sasa yeye na mkubwa wake siyo watanganyika unategemea mali za Tanganyika zibaki salama? huu ndo upuuzi wa siasa za nchi hii......inakuwaje mzanzibari anakuja kutawala Tanganyika na watu wanaona ni jambo la kawaida? tulieni tu kuni zituwakie...
 
Mkataba hauonyeshi ukomo,maana yake ni mpaka labda Yesu atakaporudi na pia mkataba unakataza pande zote kuvunja mkataba ata itokee tsunami au Watanzania tufe wote na pia kila serikali itakayoingia madarakani hairuhusiwi kuvunja mkataba.
 
Mtoa Mada, umeongea kwa hisia sana kuhusu ubinafsishaji wa Bandari zetu.

Huyo Prof. Mbarawa tunaweza kuwa tunamuonea, huyo anapewa Maelekezo na Boss wake.....

Kwa maoni yangu, jambo la uuzaji/ubinafsishaji wa Bandari tulitakiwa Wananchi wote kusimama na kupinga ili Serikali iachane na mpango huo.

Pia kuna haja ipatikane Katiba Mpya itakayo wapunguzia Mamlaka hawa Viongozi, haiwezekani Kiongozi mwenye miaka 60+ afanye maamuzi ya kuligharimu Taifa kwa miaka 99 zaidi wakati huo Yeye atakuwa ameshapumzika kwa Amani.

Hii sio sahihi, alianza Ben akabinafsisha migodi, Viwanda, Benki n.k na sasa hayupo ila Wanaoumia ni Watanzania

Na huyu naye anafata njia ya Ben na JK vile vile.


Kuna haja wenzetu wa Usalama watusaidie kutuondolea hawa Viongozi kabla hawajashika madaraka makubwa na kutuumiza. Hii ni aibu kwa Nchi.

Wale watakoishi kufika 2050 huko watakuwa na maswali ya kujibu wa Watoto wetu.
 
Reactions: nao
Kwani hii ni mara ya kwanza kusikia sakata la DP World na Bandari? Toka sakata la kwanza MoU ilikuwa tayari Sasa MoU sio mkataba..

Mwisho kwani Kuna tatizo lipi hasa?
 
Mkuu

Nakuunga mkono asilimia zote, ukoo wa majini umekuja huku bara kumrejesha sultan kwa mgongo wa uwekezaji wa kinyonyaji. Npiga kura huyo waziri aondoke au seikali nzima iwajibike
 
Wabunge wa CCM mnaiuza nchi yetu,ardhi yetu tuliyopewa na Mungu. Na Mungu awalaani ninyi na vizazi vyenu.
 
Mawala atakuwa amewekwa hapo kwa kazi maalumu......!!
 
kwa kosa gani?
 
Ameambiwa aweke Ushahidi wa 99 anaruka ruka tu,
Inchi haiendeshwi kwa majungu
Halafu hao wanaojidai kutetea tz ukute wote ni warundi sasa walitaka kujimilikisha sema Mungu fundi aisee
Asante Mungu
Warundi rudini kwenu
 
Shida ya ke kupewa mambo makubwa Toka mwanzo wa maandiko tulishaambiwa hawafai tumeshupaza shingo, mpk 2030 tutakuwa tumeuzwa mpk tunapolala
 
Sidhani kama wewe umewahi kufanya biashara yoyote inayotumia bandari zaidi ya kuja na negativity zile zile za kitanzania.

Ndugu zetu wanaoendesha bandari ile ni wezi watupu, kazi yao kuchora michoro ya wizi kila wanapoenda kazini asubuhi.
 
Kwanini ufikirie wao kama waharibifu, vipi kuhusu uharibifu wetu wa tangu mwaka sitini na moja?. Punguza kuangalia mabaya tu.

Wafikirie wale importers wanaoagiza mizigo na kulazimika kutoa rushwa kwa uzembe na upuuzi wa hawa ndugu zetu wanaofanya kazi pale bandarini.

Fikiria kwa mapana juu ya masuala mengi nyeti.
 
Mkuu huwezi kwenda mbinguni kama hukubali kufa. Huwezi kupata maendeleo bila ya kuwa na moyo wenye utayari wa kurisk.

Unachofanya ni shughuli nyepesi sana ya kulaumu na kunyooshea vidole. Kumbuka kuwa biashara ya bandari ikirahisishwa na maisha huku mtaani yanarahisishwa.

Chunga usiwe unatumika na hawa wapigaji wa bandarini wanaohisi mirija yao ya ulaji inakwenda kukatwa.
 
Sasa yeye na mkubwa wake siyo watanganyika unategemea mali za Tanganyika zibaki salama? huu ndo upuuzi wa siasa za nchi hii......inakuwaje mzanzibari anakuja kutawala Tanganyika na watu wanaona ni jambo la kawaida? tulieni tu kuni zituwakie...
Akili za kizwazwa ndizo hizi. Jikite kwenye hoja zenye mantiki achana na huu upuuzi wa ubaguzi. Unayajua madhara ya ubaguzi?.

Tafuta hotuba ya Nyerere pale Kilimanjaro Hotel ya March tisini tano.
 
Jeshi ni chama kinaitwa CCM ...hilo weka kichwani kuing'oa CCM madarakani ni mpaka ndani ya jeshi kufanyike uhasi fullstop zingine ni ngonjera. So kulitegemea jeshi kututetea sahau. Hapa namaanisha kila chombo cha ulinzi na usalama yaani vyote ni chama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…