Profesa Muhongo huna credibility ya kuwashauri watanzania kuachana na mradi wa JNHPP na usidanganye watu kuwa Hydro power zimepitwa na wakati

Duniani kote mabwawa yanajengwa. China, Ethiopia, Uganda, Brazil etc. Hawa wanajiita wasomi ndiyo wamefanya hadi leo tupo kwenye umaskini. Si wakusikilizwa.
Tufikirie na mabadiliko ya mazingira na hali ya hewa pia
 
Alipohusika kuuza gas yetu ilikuwa ni sehemu ya weledi na uzoefu?

Muujiza gani amelifanyia taifa before JPM na after?

Ni nduguyo ama?

 
Ethiopia wanajenga Bwawa kubwa la umeme halafu huyu anatuambie tuachane na maji,mfano kwa gas ipi tuliyonayo?,hii hii tu waliopewa wachina?
 

Hebu tutajie hapa hayo mataifa makubwa
Yanamtumia huyu Dalali Muhongo
Weka evidence tafadhali
 
Mgogoro huo hauwezi kuisha..., Nile ni lifeline ya Taifa la Misri, kuzuia maji / kuyapunguza yasifike huko ni kama kuwauwa..., Busara ingetumika Ethiopia kutafuta other sources ama sivyo Mgogoro huu una-potential ya kuendelea vizazi na vizazi
Sitakubaliana na wewe Maji ni God given right

Flow ya Maji ya White Nile ni kubwa sana hata imefikia kutengezeneza Ziwa linaloitwa Lake Naser

Hayo maji ni mengi Wamisri waache tamaa
 
Ethiopia wanajenga Bwawa kubwa la umeme halafu huyu anatuambie tuachane na maji,mfano kwa gas ipi tuliyonayo?,hii hii tu waliopewa wachina?
 
Wakati anasema imepitwa na wakati,China wanajenga the second largest hydroelectric dam nchini kwao hivi sasa na week hii wameanza kulijaza maji
 

kutumiwa na mataifa yaliyotuzidi ni sawa.lakini pia upeo aa mtu unachoka jamaa yangu.

inawezekana kabisa prof amechoka akili baada ya kutumika huko.
 
Muhongo analeta mbwembwe na kujifanya anajua kila kitu ili mama ampe wizara
Aende kufanya udalali kama zamani...

Ni dalali mkubwa sana wa private investors..

Anazungumzia faida wakati wenzie tunazungumzia huduma
Muhongo hana akili.

Hapo anadalalia mabwana zake wa marekani wanaouza mitambo ya gesi ili inunuliwe yeye apate kidogo.

Asisahau kua tunajua alikua ana renew leseni za uchimbaji madini bila ridhaa ya baraza la mawaziri.

Asisahau kua tunajua alichangia/kushawishi bodi ya wakurugenzi kumsimamisha mkurugenzi wa TPDC pale alipokataa vimemo vyake vya mabwana zake kupata upendeleo wa vitalu vya gas vya TPDC hadi Magufuli alipoamua kumrudisha kazini.

Asisahau kua tunajua alitaka kujaza wajita wenzake Tanesco kwenye idara ya fedha na wizara ya nishati na madini wakati huo.
 
Mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu wa mazingira hauwezi kuiacha hiyo miradi ya maji salama. Tungewekeza kwenye wind na solar
Unajua weakest link ya hizo solar na Wind ? STORAGE....

Jua linapowaka au upepo unapovuma unatengeneza umeme mwingi huenda kuliko mahitaji.., ila unapohitaji huenda hakuna jua wala upepo na kwa taarifa yako storage is expensive...

HEP pia inaweza kutumika kama battery mahitaji yakiwa madogo unapump maji mpaka kwenye bwawa la juu... yakiongeza unaachia maji yanashuka (hii ndio advantage kubwa ya HEP)
 
SSH ni dhaifu ndio maana kila mtu anajaribu kushawishi ujinga wake. Amefungalia mlango akitaka kuonyesha ana akili kumbe ameonyesha udhaifu wake.
Kushawishiwa ni jambo moja na kukubali ushauri ni jambo jingine
 
Inaleta siasa kwenye mambo ya kitaalamu, naomba uweke data kamili hapa na sio kuweka tu eti ni gharama zisizopimika
 
Muhongo hapo amegeuka entertainer, yani nilijua jamaa ni pure talented kumbe hamna kitu. Hakuweza kuwa game changer alipokuwa wizarani.

Ni unaa tu umemjaa.
 
Muhongo lost his credibility at the Ministry of Energy. He couldn't or didn't want to stop the crafty operators imposing extortinary tariffs on TANESCO. He found it easier to play the Politician rather than the professional. I am abut surprised at this:the math between gas and hydro is 101, need no PhD.
 
Duniani kote mabwawa yanajengwa. China, Ethiopia, Uganda, Brazil etc. Hawa wanajiita wasomi ndiyo wamefanya hadi leo tupo kwenye umaskini. Si wakusikilizwa.
Wameibuka sasa. Mimi sikujua kama Muhongo bado yuko nchi hii.
Itabidi mama Samia awe makini kweli kwani kila mtu sasa anataka kuibuka na kamuhogo kake - kwa maneno ya Generali Ulimwengu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…