Profesa Muhongo huna credibility ya kuwashauri watanzania kuachana na mradi wa JNHPP na usidanganye watu kuwa Hydro power zimepitwa na wakati

Profesa Muhongo huna credibility ya kuwashauri watanzania kuachana na mradi wa JNHPP na usidanganye watu kuwa Hydro power zimepitwa na wakati

Muhongo hana akili.

Hapo anadalalia mabwana zake wa marekani wanaouza mitambo ya gesi ili inunuliwe yeye apate kidogo.

Asisahau kua tunajua alikua ana renew leseni za uchimbaji madini bila ridhaa ya baraza la mawaziri.

Asisahau kua tunajua alichangia/kushawishi bodi ya wakurugenzi kumsimamisha mkurugenzi wa TPDC pale alipokataa vimemo vyake vya mabwana zake kupata upendeleo wa vitalu vya gas vya TPDC hadi Magufuli alipoamua kumrudisha kazini.

Asisahau kua tunajua alitaka kujaza wajita wenzake Tanesco kwenye idara ya fedha na wizara ya nishati na madini wakati huo.

Muhongo ni msanii laghai
Mama akiingia mkenge Tu amekwisha
 
tunatengeneza simu aina zote pamoja na computer, Tunapatika Kariakooo karibu kabisa na stand ya mwendo kasi GEREZANI 0715 378899 View attachment 1747724View attachment 1747725
090300805A-1.jpg
 
Kwa hiyo wewe profesa ulietetea wizi wa fedha za Escrow kwa nguvu nyingi mpaka ukatukana watu ni matumbili leo hii unapata wapi ujasiri wa kutuambia watanzania kuwa umeme maji unachelewa kuanza kuzaa faida na umepitwa na wakati?

Kwa hiyo huko Usa na China ambazo ni nchi zilizoendelea kwa kila namna wanapojenga Hydropower stations au kuendelea kutumia HEP kuzalisha umeme ni watu wasio na uelewa wa mambo?

Lini ilishawahi kutokea kupata nishati kama umeme ikawa ni fasheni ya kudai HEP imepitwa na wakati na sasa tutumie gas? Au unaleta dharau zako?

Hasira za wewe kufukuzwa uwaziri kisa tu ulishazoea kupiga madili makuwa hapo wizara ya nishati isiwe sababu ya kutuharibia mipango ya kukamilisha JNHPP. Kaaa kimya uendelee kutafuna posho za Escrow.
Yaani Profesa wa Geology na Geophysics hajui kwamba nishati ya gesi sio renewable siku moja itakwisha?

Naona labda watu wanamsingizia Muhongo hawezi kujitoa ufahamu mpaka kufikia kiwango cha kutoa hoja kama a layman!!
 
Mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu wa mazingira hauwezi kuiacha hiyo miradi ya maji salama. Tungewekeza kwenye wind na solar
Solar na wind? Unauelewa Kwenye masuala ya umeme kweli au?

Largest solar power station haijavuka 2500MW hapo hujagusa gharama zake

Mabadiliko gani ya Tabia ya nchi unayosemea?

Venus ilichukua miaka miilioni kadhaa kutoka kuwa kama Dunia na kuwa kama ilivyo leo...

Hata miaka 1000 ipite mto Rufiji utakuwa haujakauka...

Kinachoweza kufanya Mabadiliko ya tabia nchi yatokee ghafla labda dunia yetu igongwe astreoid, au zitokee volcano ambazo sisi hatujizui...
 
Leo nimeshituka kusikia maneno ya Professor Muongo (Mtaalamu wa Nishati) akisema umeme wa Maji sasa Umepitwa na wakati na Uchumi ni Umeme wa Gesi.

Huenda ni kweli ujenzi wa Hydro Electric Power Plant ukawa na gharama mwanzoni na sio kila nchi / sehemu inaweza ikawa na HEP sababu lazima kuwe na viable infrastructure.

Ila ni ukweli usiopingika kwamba umeme wa maji ni renewable (yaani unaweza ukazalishwa tena na tena na tena) Gesi unless otherwise ni Biogas basi uchimbaji wa gesi sio renewable... Nisiwachoshe kuna hii article hapa chini kuhusu gharama ya renewables na umeme wa maji bado ni cheaper... as of 2017 nadhani hii 2021 hali haijabadilika sana

Amesema umeme wa maji pekee umepitwa na wakati kwasababu ya mabadiliko ya hali ya hewa
 
SSH ni dhaifu ndio maana kila mtu anajaribu kushawishi ujinga wake. Amefungalia mlango akitaka kuonyesha ana akili kumbe ameonyesha udhaifu wake.
What a shit!

Dyou think buying is all what leadership is?

You better behave and know that We respect Mama big time!
 
Hapana mimi ni mnyonge, bahati mbaya tu Rais wangu amedanja! Ila alichokuwa anasema Prof. Muhongo kurudisha gharama zilizotumika kwenye umeme wa maji huchukua muda mrefu kutokana na gharama kubwa ya miundombinu tofauti na umeme wa gesi!
Kwa hiyo tunanyeje?
 
Dunia nzima inaenda kwenye nuclear, gas na solar. Sisi bado tumegomea kwenye maji
Mzee!! Nuclear, gas na solar?

Hapa umeme wa uhakika ni Nuclear na Gas unajua cost yake, Unajua Gharama ya kujenga Nuclear reactor, Gharama ya Kuindesha...

Nuclear sio carbon emission source of electricity lakini waste zake, ndio zinawafanya watu waache kuzitumia
 
Leo nimeshituka kusikia maneno ya Professor Muongo (Mtaalamu wa Nishati) akisema umeme wa Maji sasa Umepitwa na wakati na Uchumi ni Umeme wa Gesi.

Huenda ni kweli ujenzi wa Hydro Electric Power Plant ukawa na gharama mwanzoni na sio kila nchi / sehemu inaweza ikawa na HEP sababu lazima kuwe na viable infrastructure.

Ila ni ukweli usiopingika kwamba umeme wa maji ni renewable (yaani unaweza ukazalishwa tena na tena na tena) Gesi unless otherwise ni Biogas basi uchimbaji wa gesi sio renewable... Nisiwachoshe kuna hii article hapa chini kuhusu gharama ya renewables na umeme wa maji bado ni cheaper... as of 2017 nadhani hii 2021 hali haijabadilika sana

Rubish pro kwani kitu gani kinatofautisha umeme wa maji na gas zaidi ya gharama za uzalishaji, watu wanazungumzia kwamba eti maji hayaaminiki kwahiyo itafika wakati tutaambiwa maji hayafai kwa matumizi tutumie gas,hawajuhi kuwa nchi nyingi zinazozalisha umeme wa gas mala nyingi huwa hazina vyanzo vya umeme wa maji sasa mjinga mmoja anakurupuka heti umeme wa maji umepitwa na wakati,aende china kuna mabwawa yanayozalisha 50k meg ,blazil ,na nchi nyingi tu.
 
Prof Muhongo ni poyoyo!
Simkubali sana Magufuli kwa faulo alizo zifanya lakini kwa hili la umeme alilipatia vizuri.

Umeme siyo fashion.
Hoover Hydropower Dam ya Marekani iliyojengwa na kumalizika mwaka 1933 na mpaka leo linatoa umeme tena mdogo kidogo kuliko la Rufiji.
Hoover Dam 2080MW
La kwetu litakuwa 2115MW

Muhongo tunajua ana bifu na Magufuli asiliingize bifu kwenye umeme.
Uwe na kiasi. Muhongo hakuwa na heshima kwa watu zamani, lakini huwa haropoki. Ni kweli umeme wa bei rahisi ni wa maji. Lakini ukweli zaidi ni kuwa nchi ziendazo kisasa mchango wa umeme wa maji ni mdogo mno. Jiandae kuushangaa ukweli huu: Kati ya umeme wote wa Russia, umeme wa maji ni 20%; China 18%; EU haizidi 10 ( France 10, Germany 3); USA 6.6; UK 2. Tafuta ukweli huu hata kwa google
 
OK umeme wa kizamani anataka mradi uachwe pesa iliyotumika iachwe ife ili mwendazake aonekane hakufaa? siasa bw.
 
Leo nimeshituka kusikia maneno ya Professor Muongo (Mtaalamu wa Nishati) akisema umeme wa Maji sasa Umepitwa na wakati na Uchumi ni Umeme wa Gesi.

Huenda ni kweli ujenzi wa Hydro Electric Power Plant ukawa na gharama mwanzoni na sio kila nchi / sehemu inaweza ikawa na HEP sababu lazima kuwe na viable infrastructure.

Ila ni ukweli usiopingika kwamba umeme wa maji ni renewable (yaani unaweza ukazalishwa tena na tena na tena) Gesi unless otherwise ni Biogas basi uchimbaji wa gesi sio renewable... Nisiwachoshe kuna hii article hapa chini kuhusu gharama ya renewables na umeme wa maji bado ni cheaper... as of 2017 nadhani hii 2021 hali haijabadilika sana

Muhongo sio mtaalamu wa nishati, yeye ni mtaalamu wa miamba.

Aache kabisa kuingilia fani za watu.
 
Kwa CV yake tu huyu Profesa, Uweledi wake, Uzoefu wake na Uwezo wake mkubwa wa Akili nakubaliana nae tena kwa 100% juu ya huu Mtazamo wake.

Ni Rais Mpumbavu tu pekee ndiyo hatotaka kufanya Kazi na Mtu very competent kama Profesa Muhongo ambaye hata Mataifa Makubwa na yaliyotuzidi kila Kitu hadi Akili walifanya nae Kazi na sasa wanamtumia pia kama Independent Consultant katika Masuala ya Madini na Jiolojia pia.

Majungu dhidi yake hayasaidii ni Upuuzi.
Badala ya kujibu hoja na kutoa ufafanuzi we unampamba mtu[emoji1][emoji1]
 
Uwe na kiasi. Muhongo hakuwa na heshima kwa watu zamani, lakini huwa haropoki. Ni kweli umeme wa bei rahisi ni wa maji. Lakini ukweli zaidi ni kuwa nchi ziendazo kisasa mchango wa umeme wa maji ni mdogo mno. Jiandae kuushangaa ukweli huu: Kati ya umeme wote wa Russia, umeme wa maji ni 20%; China 18%; EU haizidi 10 ( France 10, Germany 3); USA 6.6; UK 2. Tafuta ukweli huu hata kwa google
Hii umeiongea kwa Summary.

China sehemu kubwa ya umeme wake unatokana na Non Renewable sources hasa Makaa ya mawe...
Power plants kubwa ya coal ni Kama Megawatts 6000MW na hawa ndio wana largest power plants.

Kwenye Nuclear Japan ndio wana powerplants kubwa ila ni 7000MW ila dunia nzima inakumbuka ajali ya Fukushima

Kwenye Gas (ambayo sisi tunayo) ni Qatar hawa wanazalisha 8000MW

Solar India na China ndio wana zalisha umeme mwingi karibu 2500MW pekee

Wind wachina ndio wana power plants kubwa kama megawatts 7000

Kwenye Hydro China wana bwawa kubwa kabisa duniani 22,000 MW

Ukiangalia Wachina Waliwekeza Nguvu nyingi sana kwenye umeme wa maji alafu ndio wakaja huko kwingine...

Hebu jaribu kuangalia bwawa moja tu China linazalisha karibu mara tatu ya umeme wote unaotokana na gesi asilia wa Qatar...

Alafu mtu kama Professor anakuja kusema Umeme wa maji hauna Mashiko
 
Back
Top Bottom