Profesa Muhongo huna credibility ya kuwashauri watanzania kuachana na mradi wa JNHPP na usidanganye watu kuwa Hydro power zimepitwa na wakati

Profesa Muhongo huna credibility ya kuwashauri watanzania kuachana na mradi wa JNHPP na usidanganye watu kuwa Hydro power zimepitwa na wakati

Gas alishauziwa mchina tuna chini ya asilimia 40 kwenye gas yetu anachotaka huyu mpuuzi ni tuingie mikataba na wachina watuuzie gas YETU naona ashaitwa pembeni na macho kengeza ...GAS TULISHALIWA KICHWA KITAAAMBO

Hili ndio tatizo lillomkwaza mwendazake
 
Kwa hiyo wewe profesa ulietetea wizi wa fedha za Escrow kwa nguvu nyingi mpaka ukatukana watu ni matumbili leo hii unapata wapi ujasiri wa kutuambia watanzania kuwa umeme maji unachelewa kuanza kuzaa faida na umepitwa na wakati?

Kwa hiyo huko Usa na China ambazo ni nchi zilizoendelea kwa kila namna wanapojenga Hydropower stations au kuendelea kutumia HEP kuzalisha umeme ni watu wasio na uelewa wa mambo?

Lini ilishawahi kutokea kupata nishati kama umeme ikawa ni fasheni ya kudai HEP imepitwa na wakati na sasa tutumie gas? Au unaleta dharau zako?

Hasira za wewe kufukuzwa uwaziri kisa tu ulishazoea kupiga madili makuwa hapo wizara ya nishati isiwe sababu ya kutuharibia mipango ya kukamilisha JNHPP. Kaaa kimya uendelee kutafuna posho za Escrow.
Hao ndiyo wana ccm wenye akili siyo kama wewe shehe ubwabwa
 
Mitambo mibovu kama nn. Uendeshaji wke ni wa gharama kuliko kawaida imagine spea unatafuta USA na haiwez fika kw wakat.
Muingo atulie tu aache uongo.
Toka aondolewe uwazir hajawai ongea kitu leoo ndioo anaibukaaa...
Kainua pua baada ya kiboko yake kuzama shimoni
 
Kwa hiyo wewe profesa ulietetea wizi wa fedha za Escrow kwa nguvu nyingi mpaka ukatukana watu ni matumbili leo hii unapata wapi ujasiri wa kutuambia watanzania kuwa umeme maji unachelewa kuanza kuzaa faida na umepitwa na wakati?

Kwa hiyo huko Usa na China ambazo ni nchi zilizoendelea kwa kila namna wanapojenga Hydropower stations au kuendelea kutumia HEP kuzalisha umeme ni watu wasio na uelewa wa mambo?

Lini ilishawahi kutokea kupata nishati kama umeme ikawa ni fasheni ya kudai HEP imepitwa na wakati na sasa tutumie gas? Au unaleta dharau zako?

Hasira za wewe kufukuzwa uwaziri kisa tu ulishazoea kupiga madili makuwa hapo wizara ya nishati isiwe sababu ya kutuharibia mipango ya kukamilisha JNHPP. Kaaa kimya uendelee kutafuna posho za Escrow.
Prof. Muhongo hajawahi kumuita mtu tumbili angalia facts zako.

Pili, tumsikilize anachoshauri kina mantinki sio kumuhukumu kwa past yake.

Asante
 
Niwakati taifa liwe na sera inayofuatwa na kila Rais. Kikwete na Nduguye Muhongo walisema sera sasa ni umeme wa gas.
Magufuli na Ndugule Kalemani wakatukarudisha kwenye hydropower/maji.

Naona dalili za Samia S kuja ni kona nyingine. Usishangae akaja na umeme wa nyukilia. Maana hata majirani zetu wameanza study ya umeme wa Nyukilia.

Nimeona huko dunia kila nchi inachanzo chake kikubwa cha umeme ikitegemea na geography na raslimali zake.

..Rais Samia Suluhu Hassan lazima aje na mradi wake mkubwa wa kimkakati.🤣

..miradi inayotekelezwa sasa hivi ni ya Jpm, Rais mpya lazima aache alama / legacy yake.
 
Ongea tu kiswahili bana ! Kiingereza hujui!
"He is gone"× ?!!!!!!! ni " He has gone"√

Ushauri wa bure, Ukiona mtu kaandika maneno ya kiingereza na wewe ukaona kakosea kwanza jaribu kupeleleza kabla ya kumsahihisha kwani yawezekana wewe ndiye usiyejua kulingana na muktadha wa hilo jambo.

Huyo ndugu hajakosea; "Is gone" na "has gone", zote zinatumika lakini zina maana tofauti, "is gone" maana yake ni hayupo, na "has gone" maana yake ni ameondoka au amekwenda.

Kuna mahali fulani niliandika maneno ya kiingereza na nilianza hivi; "If that were truth-----" basi alikuja mtu mmoja kafura kwa hasira na matusi, anauliza wewe hicho kiingereza umejifunzia wapi???!!, nieleze pimbi weee!! nataka kupima uwezo wa akili yako, mimi nimeanza kuongea kiingereza nikiwa nimo tumboni kwa mama yangu"🤣🤣🤣--- alipokuja kujua kwamba yeye ndiye mjinga na hakuwa anajua kitu alibaki kunitukana tu.

Hivyo tusikosoe kabla hatuja jiridhisha kwanza na tuwe open kupokea elimu mpya.

Shukrani.
 
Mleta mada unachanganya concepts za “renewable” na “sustainable”. Umeme wa maji ni salama kwa mazingira kwa maana hauna carbon footfrint lakini sio sustainable kwa kuwa maji yanapungua kadiri muda unavoenda (global warming). Mradi ule umeleta uharibifu mkubwa wa mazingira na kwa kuwa mazingira ni chanzo cha maji - huenda mradi mzima ukaja kuwa ni hasara kubwa sana.

Tulipaswa kujikita kwenye gesi! Prof. Muhongo yuko sahihi.
 
Leo nimeshituka kusikia maneno ya Professor Muongo (Mtaalamu wa Nishati) akisema umeme wa Maji sasa Umepitwa na wakati na Uchumi ni Umeme wa Gesi.

Huenda ni kweli ujenzi wa Hydro Electric Power Plant ukawa na gharama mwanzoni na sio kila nchi / sehemu inaweza ikawa na HEP sababu lazima kuwe na viable infrastructure.

Ila ni ukweli usiopingika kwamba umeme wa maji ni renewable (yaani unaweza ukazalishwa tena na tena na tena) Gesi unless otherwise ni Biogas basi uchimbaji wa gesi sio renewable... Nisiwachoshe kuna hii article hapa chini kuhusu gharama ya renewables na umeme wa maji bado ni cheaper... as of 2017 nadhani hii 2021 hali haijabadilika sana

Muhongo mwenyewe amepitwa na wakati, he is himself rubbish
 
Kwa CV yake tu huyu Profesa, Uweledi wake, Uzoefu wake na Uwezo wake mkubwa wa Akili nakubaliana nae tena kwa 100% juu ya huu Mtazamo wake.

Ni Rais Mpumbavu tu pekee ndiyo hatotaka kufanya Kazi na Mtu very competent kama Profesa Muhongo ambaye hata Mataifa Makubwa na yaliyotuzidi kila Kitu hadi Akili walifanya nae Kazi na sasa wanamtumia pia kama Independent Consultant katika Masuala ya Madini na Jiolojia pia.

Majungu dhidi yake hayasaidii ni Upuuzi.
Kwa kazi ipi ya Maana alowahi kuisimamia ikaleta matokeo chanya??

Ni Ile ya kusimamia mitambo ya symbion na kuruhusu umeme wa majenereta kariakoo kutawala siyo?

Au Ile ya kuwananga Watanzania kwamba pesa zao ni za kuwekeza Kwenye madafu baada ya kugomea kumpa hongo??
 
Kwa CV yake tu huyu Profesa, Uweledi wake, Uzoefu wake na Uwezo wake mkubwa wa Akili nakubaliana nae tena kwa 100% juu ya huu Mtazamo wake.

Ni Rais Mpumbavu tu pekee ndiyo hatotaka kufanya Kazi na Mtu very competent kama Profesa Muhongo ambaye hata Mataifa Makubwa na yaliyotuzidi kila Kitu hadi Akili walifanya nae Kazi na sasa wanamtumia pia kama Independent Consultant katika Masuala ya Madini na Jiolojia pia.

Majungu dhidi yake hayasaidii ni Upuuzi.
Unamjua Muhongo au unakuja na ushabiki maandazi?
 
Duniani kote mabwawa yanajengwa. China, Ethiopia, Uganda, Brazil etc. Hawa wanajiita wasomi ndiyo wamefanya hadi leo tupo kwenye umaskini. Si wakusikilizwa.

Wrong examples. Nchi zote hizo zimetumia mabavu kulazimisha hiyo miradi. Profesa yuko sahihi.

Amandla...
 
Mleta mada unachanganya concepts za “renewable” na “sustainable”. Umeme wa maji ni salama kwa mazingira kwa maana hauna carbon footfrint lakini sio sustainable kwa kuwa maji yanapungua kadiri muda unavoenda (global warming). Mradi ule umeleta uharibifu mkubwa wa mazingira na kwa kuwa mazingira ni chanzo cha maji - huenda mradi mzima ukaja kuwa ni hasara kubwa sana.

Tulipaswa kujikita kwenye gesi! Prof. Muhongo yuko sahihi.
Ukiifunga akili kwa kutazama mazingira ya pale bwawani pekee utaona hali ipo hivyo, lakini ukiifungua na kuboresha mazingira kule yanakotokea maji na hasa Njombe, Iringa, Mbeya na Morogoro itawezekana kabisa kuwa na maji ya kutosha mwaka mzima,
 
Back
Top Bottom