Profesa Muhongo: Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati

Profesa Muhongo: Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati

Umeme wa maji katika nchi baridi za kaskazini kama Niagara Falla USA, Yangtse China ni sahihi.

ila nchi za joto za tropiki ambazo wananchi wake wanaharibu mazingira kwa kuwa wengi ni wakulima wadogo na wachoma mkaa umeme wa kutegemea vyanzo vya maji pekee ni changamoto kubwa.

Hii ndiyo tofauti ya kijiografia na hali ya hewa inatakiwa kuzingatiwa kwa nchi za joto za tropiki kuwa na vyanzo mchanganyiko vya umeme yaani gesi ,maji ili kushinda upungufu wa nishati ikitokea ukame n.k

Mkuu suala hapa ni nishati jadidifu Na rahisi kwa wananchi
Haina mjadala umeme wa maji Ndio nishati nafuu kuliko zingine zote ... kwa mazingira kuna hydropower dams za miaka na miaka hapa hapa kwetu bado zinajiendesha vizuri tu !
Kijiografia hilo ni tatizo sio la positioning na location kwani Mazingira ni suala mtambuka ambalo hata huko ulikokutaja wanakabiliana nalo na mabadiliko ya tabia nchi...
So Amna strong reason ya kuzuia tusipate hizo 2100 Megawatts za Nyerere Hydropower zaidi ya ukoloni mamboleo tu !
Hakuna ubaya kujenga bwawa Na kuendelea kutunza Mazingira Na vyanzo vya maji ili kuhakikisha tunaendelea kufaidika nayo kwa muda mrefu zaidi !

Linganisha Bei ya umeme wa
Gesi
Maji
Nyuklia
Mafuta
Jua
Upepo
Nyoto ardhi

Kisha utoe jibu ni umeme upi wa gharama nafuu zaidi ya umeme wa Maji !

Thanks
 
Gas ilishauzwa kwa wachina tunaumilizi wa asilimia 30 tu ya gas yetu
Umepewa 30% na hukuwekeza kwenye research and development ambayo mwekezaji kafanya for about 15 years. Nayo teknolojia huna, mtaji wa mwekezaji bado huridhiki na 30%?
 
Muhongo huu mradi alianza kuupinga siku nyingi toka akiwa waziri wa nishati. Alisema naji hayatoshi. Ila kwa unafiki wake alienda kuzindua mradi wa umeme wa maji Rusumo.

Mi napingana na huyu mnafiki, kwanza duniani kote, kuanzia Uganda, Ethiopia, China hadi Brazil mabwawa ya kuzalisha umeme yanajengwa sana. Mto Congo unaweza zalisha umeme wa kutosha Africa nzima na kwa bei ya chini kabisa.
Pili Muhongo hana data za sasa zinazoonyesha kuwa huo mradi hauna faida. Watz tusiwasikilize sana hawa wasomi wetu, ndiyo wasababishi wa umaskini tulio nao leo, wengi wao ni educated fools.
Wewe unazo hizo data nasisi tusome hapa

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
tukisitisha ujenzi wa hivyo vinu,ni mwanao ndiye atakuja kuona madhara ya kutokuwa na vyanzo vingi vya nishati.kwa sasa wewe unaangalia kitambi chako na akili yako scope hake mwisho ni kkutwa jion,zaidi ya hapo haioni kitu.

reli inajengwa iishi miaka zaidi ya 100,unazungumzia faida ndani ya miezi 3,kwani mnafikirije wenzetu mbona mko slow namna hii!!!!

tanzania inakua ndugu zangu,miaka 10 tu ijayo itakuwa na uhitaji wa kila kitu kwa ukubwa zaidi,iwe heri kwa tanzania mama asisitishe miladi kwa kuogopa kelele za watu kama nyinyi,ni hatari kwa taifa lijalo.

CAG ametumia pua yake na kipara,kutoa tathmini ya miladi,miladi yote inaonekana kuwa haina tija,ni kweli haina tija!!!au tumechoka kufikiri??
Kama Huwezi kutofautisha l na r wewe ni mburula. Kwenye miradi unaandika miladi. Huna ubongo wa kushiriki mjadala huu. Nenda kaoge umsubiri mumeo
 
Nashanganzwa na maoni ya huyu Prof Muhongo aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati. Ati fashion, nasema fashion ya production ya umeme ni ule wa gesi.

Poor logic and thinking indeed. Kenya AU zambia au Malawi, wasiokuwa na gesi vipi?

Na initial costs as compared to operational costs inakuwaje?

Inabidi tujikumbushe kuwa mtu kuwa Proffessor haina maana ni proffessonal katika eneo alilosomea.

Katika hili Prof Muhongo amebugi vibaya.

Mi si mpenzi sana wa Magufuli kutokana na tabia zake za kutofuata demokrasia, lakini mradi huu wa Nyerere Hydropower Dam uachwe ukamilike.

Lakini tuchunguze nyuma ya pazia, pengine kuna ka beberu kamepenyeza rupi!
 
Ethiopia walifukie tu lile bwawa na china nao walibomoe tu lile bwawa lao watumie gas umeme wa maji umepitwa na wakati.
 
0a7ec864acfa472d865222e2abc12c41.jpg
 
Ethiopia wako kwwnye conflict na Egypt kwa sababu ya grand Ethiopian Dam, na wenyewe wamekurupuka? Au hawana maono?
Hao wafanyabiashara watano uliowataja ndio tunawategemea waendeleze mradi wa SGR?
Elimu ya Watanzania kwa kweli ni duni. Unajuwa kabisa wako kwenye mgogoro na Misri kuhusu Grand Renaissance Dam bado unaniuliza je wamekurupuka?

Jibu ni ndiyo wamekurupuka. Walipaswa kuangalia treaties za mwaka 1893 na nyingine ya 1910
 
Dooh nimecheka saana haya watu wanafufuka mmoja mmoja wanaaanza upya kuchomoa makucha yao.

Hawana tena cha kuhofia mana enzi za shamba la bibi zinarudi kila mtu anaanzisha ubunifu mpya wa kupiga pesa.

Huyu ni Muhongo tayari bado namsubiri Ngereja naye atakuja na lipi.

Na muda si mwingi tutasikia Accacia nayo imefufuliwa upya na kupewa mgodi huko geita kwasababu nchi inahitaji zaidi wawekezaji kuliko wao wanavyo tuhitaji.
Na leo usiku uongozi wote unatua Dar subiri kesho kutwa utasikia....
 
Akichangia katika mpango wa maendeleo wa Serikali bungeni amesema anashangaa watu wanavyohangaika na umeme wa maji na huku dunia ya sasa ni umeme wa gesi

Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati.

Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema uchumi wa gesi pekee ndiyo utakaoifikisha Tanzania kwenye uchumi thabiti.

Profesa Muhongo ametoa kauli hiyo wakati akichangia kwenye mpango wa Serikali leo Aprili 9,2021 bungeni Jijini Dodoma

Waziri huyo wa zamani wa Wizara ya Nishati na Madini amesema Tanzania kuendelea kuwaza kuhusu madini yaliyopo ni kuchelewa huku akikosoa mawazo ya kutegemea uzalishaji wa umeme mkubwa kwa kutumia maji.

Amesema Tanzania inatakiwa ijikite katika matumizi ya umeme mchanganyiko badala ya kutegemea mabwawa ya Maji ambayo wakati wowote yanaweza kukauka.

"Kuwekeza katika umeme wa maji halafu unasema utaleta fedha, huko ni kujidanganya kwani umeme wa maji huchukua muda mrefu kuanza kutoa faida, huko wenzetu wamepita wanafanya mambo kisasa” amesema Profesa Muhongo.

Amesema dunia ya sasa imegeuka na madini mengi yanayotarajiwa Tanzania yapo lakini wengine wameelekeza kwenye dhahabu, Tanzanite na madini mengine ya zamani lakini wanaacha kuangalia madini mapya ambayo yataliingizia Taifa fedha nyingi.

NB: Baada ya Dkt. Magufuli kuondoka sasa kila mtu CCM rangi yake ya zamani imeanza kurudi

Hivi kweli mmeanza kupinga project ya Rufiji baada ya Dkt. Magufuli kudondoka

CCM acheni unafiki
Daah hata kama ni kudanganya si kwakiasi hicho, watu wanaenda kwenye smart technology yeye anadai fossil fuels ndiyo energy option ya 21st century?

Duniani kuna watu na viatu!
 
Sasa hivi kwa mujibu wenu matatizo yote ameondoka nayo Magufuli, maana yeye ndio akikuwa tatizo hapa nchini kwa hiyo jiandaeni kuishi kwa neema!

Sasa hivi kwa mujibu wenu matatizo yote ameondoka nayo Magufuli, maana yeye ndio akikuwa tatizo hapa nchini kwa hiyo jiandaeni kuishi kwa neema!
Kuishi kwa neema ni mambo mengine, tunafurahi kutokuwa chini ya mtu dhalimu na jizi la kura.
 
Akichangia katika mpango wa maendeleo wa Serikali bungeni amesema anashangaa watu wanavyohangaika na umeme wa maji na huku dunia ya sasa ni umeme wa gesi

Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati.

Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema uchumi wa gesi pekee ndiyo utakaoifikisha Tanzania kwenye uchumi thabiti.

Profesa Muhongo ametoa kauli hiyo wakati akichangia kwenye mpango wa Serikali leo Aprili 9,2021 bungeni Jijini Dodoma

Waziri huyo wa zamani wa Wizara ya Nishati na Madini amesema Tanzania kuendelea kuwaza kuhusu madini yaliyopo ni kuchelewa huku akikosoa mawazo ya kutegemea uzalishaji wa umeme mkubwa kwa kutumia maji.

Amesema Tanzania inatakiwa ijikite katika matumizi ya umeme mchanganyiko badala ya kutegemea mabwawa ya Maji ambayo wakati wowote yanaweza kukauka.

"Kuwekeza katika umeme wa maji halafu unasema utaleta fedha, huko ni kujidanganya kwani umeme wa maji huchukua muda mrefu kuanza kutoa faida, huko wenzetu wamepita wanafanya mambo kisasa” amesema Profesa Muhongo.

Amesema dunia ya sasa imegeuka na madini mengi yanayotarajiwa Tanzania yapo lakini wengine wameelekeza kwenye dhahabu, Tanzanite na madini mengine ya zamani lakini wanaacha kuangalia madini mapya ambayo yataliingizia Taifa fedha nyingi.

NB: Baada ya Dkt. Magufuli kuondoka sasa kila mtu CCM rangi yake ya zamani imeanza kurudi

Hivi kweli mmeanza kupinga project ya Rufiji baada ya Dkt. Magufuli kudondoka

CCM acheni unafiki
Makosa ni ya Magu mwenyewe ambaye kila aliyejaribu kumshauri tofauti na mawazo yake alimuona kama adui, kibaraka wa mabeberu na kumtishia kazi yake au maisha moja kwa moja kwa hiyo watu wakaamua kumuacha alisongeshe anavyotaka wakijua fika atakwama!
 
Dooh nimecheka saana haya watu wanafufuka mmoja mmoja wanaaanza upya kuchomoa makucha yao.

Hawana tena cha kuhofia mana enzi za shamba la bibi zinarudi kila mtu anaanzisha ubunifu mpya wa kupiga pesa.

Huyu ni Muhongo tayari bado namsubiri Ngereja naye atakuja na lipi.

Na muda si mwingi tutasikia Accacia nayo imefufuliwa upya na kupewa mgodi huko geita kwasababu nchi inahitaji zaidi wawekezaji kuliko wao wanavyo tuhitaji.
Mbona alikuwepo na wamepiga pesa Sana?
 
Kaka hiyo gas yenyewe iko wapi kaka, gas ile tulisha pigwa tangu enzi za mkwere hakuna gas kule ile ni mali ya watu. Magu ameingia kakuta tayari hakuna chetu kule ndio mana akaona bora aje na huo mradi wa umeme wa maji.

Unaposema nchi haina sera maalum ni kweli sikupingi na sababu kubwa ni hawa viongozi wenye tamaa za kifisi fisi.

Wafute tu miradi yote waanzishe mipya wapige hela

Kama aliweza kuwabana wazungu wa kwenye madini mpaka Boss wa Barrick akaja, kilimshinda nini huko kwenye Gas? Kama kwenye gas tumepigwa na kina JK, mbona alikuwa hawaambii wananchi, bali alikuwa anatumia propaganda chafu kusema wapinzani wanatumika na mabeberu kutaka kuuza nchi, wakati hakuna mkataba wowote wapinzani wamewahi kuingia na wageni?

Kama yeye aliogopa kuwataja waliouaza raslimali za nchi, na kuishia kuwachafua wasiohusika, una uhakika gani na huu mradi wake wa maji, hasa ukizingatia kuwa Magufuli hakuwa rais muadilifu?
 
Back
Top Bottom