Bloodstone
JF-Expert Member
- Feb 16, 2016
- 920
- 994
Umeme wa maji katika nchi baridi za kaskazini kama Niagara Falla USA, Yangtse China ni sahihi.
ila nchi za joto za tropiki ambazo wananchi wake wanaharibu mazingira kwa kuwa wengi ni wakulima wadogo na wachoma mkaa umeme wa kutegemea vyanzo vya maji pekee ni changamoto kubwa.
Hii ndiyo tofauti ya kijiografia na hali ya hewa inatakiwa kuzingatiwa kwa nchi za joto za tropiki kuwa na vyanzo mchanganyiko vya umeme yaani gesi ,maji ili kushinda upungufu wa nishati ikitokea ukame n.k
Mkuu suala hapa ni nishati jadidifu Na rahisi kwa wananchi
Haina mjadala umeme wa maji Ndio nishati nafuu kuliko zingine zote ... kwa mazingira kuna hydropower dams za miaka na miaka hapa hapa kwetu bado zinajiendesha vizuri tu !
Kijiografia hilo ni tatizo sio la positioning na location kwani Mazingira ni suala mtambuka ambalo hata huko ulikokutaja wanakabiliana nalo na mabadiliko ya tabia nchi...
So Amna strong reason ya kuzuia tusipate hizo 2100 Megawatts za Nyerere Hydropower zaidi ya ukoloni mamboleo tu !
Hakuna ubaya kujenga bwawa Na kuendelea kutunza Mazingira Na vyanzo vya maji ili kuhakikisha tunaendelea kufaidika nayo kwa muda mrefu zaidi !
Linganisha Bei ya umeme wa
Gesi
Maji
Nyuklia
Mafuta
Jua
Upepo
Nyoto ardhi
Kisha utoe jibu ni umeme upi wa gharama nafuu zaidi ya umeme wa Maji !
Thanks