Profesa Muhongo: Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati

Profesa Muhongo: Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati

Wote waliufyata Ali manusura utokee mdomoni
Walichokuja wanafanya kila alichofanya hata akiharibu wanasifia wakiwa pembeni kina Nnape na Kinana wanamwita mshamba, kachanganyikiwa. Tatizo kila kitu alijifanya anajua, wanaojua wanaanza kupiga makofi na kushangilia ili maisha yasonge.
 
Hivi kuna mtu mwenye akili timamu anamwamini huyu Muhongo anachokisema?
 
Gesi ya nchi hii inakuaje mali ya watu??? Kama rais aliingia madarakani akakuta tayari gesi ya mtwara ni mali ya watu ni akina Nan hao ambao alishindwa kuwatambua mpaka aanzishe mradi mwingine ambao pengine alikua na maslahi nao!! Kwani tukisema rais wenu alikua dhaifu tunakosea???
Rais wetu? Mbona umejiondoa mkuu kwanini?
Unashangaa nikisema gas tumepigwa? Angalia bei ya gas huko mitaani ndo utajua yetu au ina wenyewe.
 
Gesi kitu gani watu wanazungumzia umeme wa nguvu za nyuklia,

Professor wa wapi huyu , hata Maji marefu anamzidi??
 
Mhuni huyu.
ANA JIFANYA HAJUI GHARAMA ZA UENDESHAJI WA GESI NI JUU KULIKO MAJI.
 
Nimeipenda sana hii Elimu kubwa uliyoitoa hapa, mimi sio mtaalamu kabisa wa umeme na ninaheshimu sana elimu, lakini nina akili timamu. Sasa tuje kwenye uhalisia wa gharama za huo umeme maji. Kabla ya kuanza kutumia umeme wa mafuta mazito na gas, tulikuwa tunatumia umeme wa maji, mbona wakati huo umeme bado haukuwa rahisi? Kwenye nchi za Afrika mashariki bado sisi hatukuwa na bei ndogo ya gharama ya umeme. Sasa nikichukua hii elimu yako na ukweli huo wa bei, huoni kama unatuvuruga?
huko nyuma tulikuwa tunazalisha umeme kwa kiwango kidogo na serikali ilichukua mda mrefu haiwekezi hivyo gharama za uendeshaji tanesco kama shirika zilikuwa juu.

kwa sasa tunatazama kuzalisha umeme kwa kiwango kikubwa ambao gharama za kiuendeshaji wa shirika hazina athari kubwa kwenye bei.
 
Dooh nimecheka saana haya watu wanafufuka mmoja mmoja wanaaanza upya kuchomoa makucha yao.

Hawana tena cha kuhofia mana enzi za shamba la bibi zinarudi kila mtu anaanzisha ubunifu mpya wa kupiga pesa.

Huyu ni Muhongo tayari bado namsubiri Ngereja naye atakuja na lipi.

Na muda si mwingi tutasikia Accacia nayo imefufuliwa upya na kupewa mgodi huko geita kwasababu nchi inahitaji zaidi wawekezaji kuliko wao wanavyo tuhitaji.
Mwendazake alikua jambazi wa aina yake kuwahi kutokea duniani,alifikiria uwizi wake utabaki kua siri
 
Tundu Lissu, Muhongo, Lema na Chadema kwa ujumla mkitaka kuuwa legacy ya hayati rais Magufuli kwa watanzania itabidi ufanye yafuatayo.

Unapokula kichwa mradi wa umeme kutoka bwawa la Nyerere ambao umefikia 50% itabidi watuambie umeme tutatoa wapi?.

Unapokula kichwa serikali kuhamia Dodoma na kusema ni hasara itabidi wajieleze.

Unapokula kichwa reli ya kisasa ambayo inakaribia Makutupora itabidi wajieleze kwa watanzania hiyo Tanzania ya viwanda itawexekana vipi.

Unapokula kichwa ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makuu itabidi watueleze watatusafirisha na nini?

Wanapokula kichwa ndege zetu itabidi tuwawekee video za kina Heche ,Lema,Lisu wakitukana serikali iliyoshindwa kununua ndege

Watakaposema wachimbaji wadogo, bodaboda na mama ntilie wafukuzwe itabidi watueleze wanafanya haya kwa faida ya nani?

Watakapoamua zahanati na hospitali zote zilizojengwa na Magufuli zifungwe ,itabidi watueleze tutaenda kutibiwa wapi?

Watakaposema wamefuta elimu bure itabidi watueleze kodi zetu zinafanya kazi gani?

Watakaposema lazima watanzania millioni 60 wachanjwe, itabidi watueleze wao mpaka sasa
hawajachanjwa
Nyungu hawajapiga,
Hawajajifungia ndani wanaenda kazini kila siku
Mbona hawajafa na corona sasa?

Watakaohoji haya maelezo siyo Magufuli wala watoto wa Magufuli ni watanzania.

Anayedhani itakuwa rahisi kuuwa legacy ya Magufuli atakutana na nguvu ya uma.

Muda utaongea .
Labda nguvu ya uma na kijiko,meko alikua jambazi wa kodi za watanzania .....hata mzikiri mzuti uwizi wake haufichiki
 
Mm binafisi siitaki tena ccm baada tu ya magufuli kufariki wameanza kumgeuka wamesahau kabisa kabla ya 2015 walikua wakipita mjini na manguo yao kijani walikua wana zomewa wengine wana diriki kusema rais ali shauriwa vibaya, inaoneka walikua wana jali matumbo yao tu wa tz tuamukeni.
Msimu wa embe umeisha nyani wote wa mataga mtakufa na njaa
 
Eti umeme wa maji umepitwa na wakati na watu wamo wanachekelea huu uzombi. Ethiopia wapo tayari kupigana na Egypt kwa umeme wa maji. China amejenga the biggest DAM ambayo wanasayansi wanasema hata mzunguko wa dunia umepungua kidogo. Dunia inahangaika na Renewable energy yeye anpendekeza tutegemee limited energy 😀
 
Hahahaaaa...... Bado naamini Magufuli alikuwa kiongozi jasiri zaidi kuwahi kutokea hapa nchini akifuatiwa na mzee Abdul Jumbe!
Kwa ujambazi wake kweli ni mfano kuwahi kutokea hapa nchini n duniani,kwani nasema uwongo bwashee
 
huko nyuma tulikuwa tunazalisha umeme kwa kiwango kidogo na serikali ilichukua mda mrefu haiwekezi hivyo gharama za uendeshaji tanesco kama shirika zilikuwa juu.

kwa sasa tunatazama kuzalisha umeme kwa kiwango kikubwa ambao gharama za kiuendeshaji wa shirika hazina athari kubwa kwenye bei.

Unachojaribu kuongea hapa ni matamanio yako,na sio lazima iwe kweli. Kama huo mradi ni wa fedha za mkopo, huo urahisi wa bei ya umeme umeujuaje? Unajua terms za mkopo?
 
Maisha ni hatua,acha tuanze na maji then tutafika huko wenzetu waliko,mambo ya gesi wenyewe mliingia mikataba ya ovyo leo mwajifanya kutoa ushauri.unafiki wa kiwango cha juu Sana
Akichangia katika mpango wa maendeleo wa Serikali bungeni amesema anashangaa watu wanavyohangaika na umeme wa maji na huku dunia ya sasa ni umeme wa gesi

Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati.

Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema uchumi wa gesi pekee ndiyo utakaoifikisha Tanzania kwenye uchumi thabiti.

Profesa Muhongo ametoa kauli hiyo wakati akichangia kwenye mpango wa Serikali leo Aprili 9,2021 bungeni Jijini Dodoma

Waziri huyo wa zamani wa Wizara ya Nishati na Madini amesema Tanzania kuendelea kuwaza kuhusu madini yaliyopo ni kuchelewa huku akikosoa mawazo ya kutegemea uzalishaji wa umeme mkubwa kwa kutumia maji.

Amesema Tanzania inatakiwa ijikite katika matumizi ya umeme mchanganyiko badala ya kutegemea mabwawa ya Maji ambayo wakati wowote yanaweza kukauka.

"Kuwekeza katika umeme wa maji halafu unasema utaleta fedha, huko ni kujidanganya kwani umeme wa maji huchukua muda mrefu kuanza kutoa faida, huko wenzetu wamepita wanafanya mambo kisasa” amesema Profesa Muhongo.

Amesema dunia ya sasa imegeuka na madini mengi yanayotarajiwa Tanzania yapo lakini wengine wameelekeza kwenye dhahabu, Tanzanite na madini mengine ya zamani lakini wanaacha kuangalia madini mapya ambayo yataliingizia Taifa fedha nyingi.


NB: Baada ya Dkt. Magufuli kuondoka sasa kila mtu CCM rangi yake ya zamani imeanza kurudi

Hivi kweli mmeanza kupinga project ya Rufiji baada ya Dkt. Magufuli kudondoka

CCM acheni unafiki
 
Sisi ni watu wa ajabu sana, kipindi mzee yupo haya tunayo yapinga leo yalikua na mantik nzuri, ila leo yamekosa uhalisia kabisa.

Kuna watu wanajaribu kujitengenezea popuparity walio ipoteza,
 
Dooh nimecheka saana haya watu wanafufuka mmoja mmoja wanaaanza upya kuchomoa makucha yao.

Hawana tena cha kuhofia mana enzi za shamba la bibi zinarudi kila mtu anaanzisha ubunifu mpya wa kupiga pesa.

Huyu ni Muhongo tayari bado namsubiri Ngereja naye atakuja na lipi.

Na muda si mwingi tutasikia Accacia nayo imefufuliwa upya na kupewa mgodi huko geita kwasababu nchi inahitaji zaidi wawekezaji kuliko wao wanavyo tuhitaji.

Bora angebaki mwamba apige peke yake kifo hiki daaa
 
Leteni generators mtaani ili demand ya fuel izidi kupaa juu, watu wakae juu.
Kuhofia mabwawa kukauka mhofie na ukataji miti ovyo kwa ajili ya nishati kuni! Yatakauka sana!
 
Hata Ethiopia wanaojenga Bwawa kubwa la Umeme hapa Afrika nao wanapoteza muda??

Huko China na Ulaya bado wana Hydro Power Plant kubwa tu...nao vp wazijunje??

Acheni kuchotwa akili na WANASIASA MATUMBO
Hao Ni mihemuko inawasumbua China wana largest hydroelectric power plant Misri na Ethiopia Africa wanaongoza shida wanatanguliza mihemuko na chuki na hyo profesa aishia kushauri serikali iwekeze pia vyanzo vingine ningemuelewa stop kuponda tu hyo stiglers
 
Back
Top Bottom