Profesa Muhongo: Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati

Inamaana na ethiopia wako tayari kupigana na misri sababu ya outdated project ?
 

Kama utakumbuka. Magufuli hakuwa ccm, ndiyo maana mwaka 2015 alikuwa akisema chagua Magufuli, na si ccm. Na hivi invyoonekana ccm kukosa muelekeo, ndiyo furaha yake. Maana yeye hakuwa sehemu ya sisiem masilahi ambayo imeamua kugawana fito.
 
Muhongo anaongea pumba tupu hata hajui kuwa gesi inapatikana katika nchi chache sana na siyo rahisi kuzifikia nchi nyingi kwa matumizi ya umeme bali mpaka iwekwe kwenye mitungi na kusafirishwa kwa matumizi ya nishati na siyo umeme wa matumizi ya nyumbani na viwandani.
Kweli Paka akiondoka panya ujitawala.
Muhonga anatakiwa kujua hatuwezi ku manage vizuri madini mapya wakati tunayoyachimba sasa hivi yametushinda, tutaishia kuibiwa tu.
 
Hali halisi ya mto Rufiji inaanzia mkoa wa Mbeya kupitia Iringa, Dodoma, Morogoro na Pwani. Mto Ruaha si ule wa miaka ya sitini, daraja la Mkapa lilijengwa kwa kiwango cha upana wa mto Rufiji miaka ya sitini ambapo sasa kiko chini ya nusu
Sasa badala ya kutunza catchments mnahangaika na dirty sources?

Hayati aliweka hadi jeshi usu unafikiri kwanini? Ilikuwa ni mapambo au?
 
Ethiopia wako kwwnye conflict na Egypt kwa sababu ya grand Ethiopian Dam, na wenyewe wamekurupuka? Au hawana maono?
Hao wafanyabiashara watano uliowataja ndio tunawategemea waendeleze mradi wa SGR?
Come Rain Come Sun Bwawa la Stigliers Geog
e litajengwa.(Ije Mvua lije Jua)
 
[emoji106][emoji106][emoji106]
 
Wala Magufuli hakubisha ila alikataa terms zilizopo ktk mradi wa Gas ya Msimbati ili Watanzania waweze kuutumia kwa affordable charges. Hili nalo Propesa Muhogo kaliongelea ktk wasilisho lake?.

Najua WATANZANIA watanikumbuka kwa mambo mazuri.
 
[emoji106][emoji106]
 
Mkuu usiongee Kama si mtu mkomavu kwenye siasa za Tanzania.
Unapozungumza kuhusu namna gani aliwabana watu wa madini na kuwasema wapinzani wanauza nchi hakuwa amekosea mana ni kweli mtu Kama Lissu alifikia hatua kusema tukigusa hiyo mikataba tutashitakiwa MIGA huko process yote ya mabadiliko ya mikataba ya madini ilipingwa vikali sana na wapinzani hata humu jukwaani ushahidi upo humu mfono Zitto Kabwe alitoa makala nyingi sana humu kupinga hii mikataba Lissu aliziita ripoti zile kuwa Rubbish nadhani unakumbuka lakini mpambano ule mwisho ukaja na majibu mikataba ikabadilishwa.

Kaburi la gas nalo lilikuwa na mambo yake mengi mno kumbuka vurugu za mtwara enzi za mkwere kutaka gas kuletwa bagamoyo. Unapotaka kumsema Magufuli kwenye hili itabidi pia uangalie matatizo hayo yalianzia wapi hili suala la gas lingekuwa jepesi asingeacha kuligusa ila mikataba yake imekuwa tofauti na hii mingine na huwezi kufukua makaburi yote lazima Kuna mengine yatakushinda tu huo ndio ukweli ( labda tumnange tu kisiasa lakini ukweli ni huo).

Leo tunamsikia Mama anasema hadharani Kuna mambo amejaribu kusolve yamemshinda why wakati yeye ndio rais?

Hapo ndio ujue kuwa Kuna vitu vingine ni vigumu kuviondoa hata Kama una nia njema mkuu.

Hili suala la Magufuli hakuwa rais muadilifu unalitengeneza hivo ili likupe nguvu kwenye hoja yako huku hata wewe mwenyewe ukijipinga hapo juu kuwa alipigania madini kwa nguvu zote why ikawe yeye si muadilifu?

Mradi wa bandari ya bagamoyo ambao aliukuta mezani hauja pitishwa na rais ameukataa huku akieleza ubaya wa mkataba huo ambao kama ungepitishwa kabla hajaingia nina hakika asinge weza kuubali haya yote yanaonyesha uadilifu wake Leo amekufu wenye tamaa wanataka kuurudisha wapige hela kisha unakuja kumuita Magufuli si muadilifu angekubali fungu akawaweka mezani wachina wakampa chochote asingekubali huo mradi? Kwanini useme Magufuli si muadilifu ?

Tukija kwenye huu mradi nina kila sababu ya kumuamini Magufuli zaidi ya hawa maprofesa ambao rangi zao tunazijua tangu mwanzo.
Figisu za kuzuia huu mradi zilianza zamani kwa kigezo cha kuharibu mazingira na wanaharakati wa humu humu ndani waliunga mkono huku wakijua kabisa hatuna umeme wa uhakika na mazingira yalivyo kwa nchi yetu ni bora huo umeme wa maji ni nafuu kuliko gas na vyanzo vingine kwa Tanzania yetu hii bado hatuna uwezo huo.
Leo wakiibuka watu Kama hawa kwangu inakuwa ngumu kuwamini labda naweza kusema kuwa watu hawa ni mawakala wa huo umeme mbadala wanao unadi na kunafungu wanapata huku wakitudanganya wananchi na vile wengi elimu ni ndogo basi ndio tatizo kabisa.

Hiyo gas ambayo tunamiliki 30% eti ndio itumike kuzalisha umeme wa kutosha taifa zima? Serious?
Hebu fuatilia bei za gas za majumbani tu humo uone hali jinsi ilivyo.

Mkuu mimi naishia hapa, wakiona huu mradi ni mbovu okay fine waufute kisha walete hiyo miradi ambayo haijapitwa na wakati kisha baada ya miaka 10 Mungu akitupa uzima turudi tena kujadili outcome yake.
 

Nimecheka kwa nguvu hiki ulichoandika hapa, sio kwamba una utetezi wa nguvu, bali umejaribu kuweka maelezo marefu ukidhani ndio utakuwa umeweza kutetea utakacho.

Tuanze na hilo la uadilifu, toka ameingia madarakani tumeona vikundi vya mauaji kwa jina la watu wasiojulikana, wengi wa wanaomkosoa wametekwa, kuuawawa, kushambuliwa na hata kuachwa na vilema vya maisha, huku serikali yake ikaicha kuchukua hatua stahiki. Chaguzi zote za nchi tumeona zikigubikwa na mauaji, wizi wa kura wa wazi, ushenzi, ukatili na uhayawani wa wazi, na haya yote yalikuwa ni maagizo yake. Aliondoa uhuru wa vyombo vya habari, ili aweze kufanya mambo kwa namna aitakayo yeye, bila hayo kuwekwa hadharani. Hakuna mtu muadilifu anafanya mambo haya, wala kukwepa uwazi. Toa utetezi usioacha shaka wa uadilifu wake kwenye maeneo haya.

Kwenye hilo la kwamba wapinzani wanataka kuuza nchi, nimetaka uniambie ni hatua gani kachukua kwenye waliouza nchi kwa vitendo kama hiyo Gas. Hakuna mzungu atasubiri auziwe nchi na mtu asiye madarakani, wakati walioko madarakani wanaweza kumuuzia kirahisi. Lisu alitoa maoni yake, kuwa hiyo mikataba ni michafu hivyo mazingira ya kushitakiwa yako wazi, mfano wa uchafu wa hiyo mikataba ni huo wa Gas. Hapa naona ulibebwa na propaganda, ndio maana unatumia kwenye utetezi wako, lakini huna content za maana zinazobeba utetezi wako zaidi ya propaganda mfu.

Hayo ya madini, ili nijue kweli una uhakika na ukisemacho kuhusu mikataba ya madini kubadilika, maana sio ww au mimi tumeona mikataba, huenda ww mwenzangu umeona mkataba. Sasa naomba unitolee ufafanuzi wa ule mkataba wa Barrick/Twiga wa sisi kupata 16% na faida ya 50/50, maana huwa sielewi Kabudi huwa anaongea nini. Zingatia mama juzi kasema huko kwenye mkataba wa Barrick kuna mambo hayako sawa. Ukitoa ufafanuzi wa hili nitajua unajua unachoongea, au ni wale wa kubebwa na porojo za kisiasa.

Hilo la gas sioni kama una uelewa nalo maana umetoa mfano wa bei ya gas ya majumbani. Kwa taarifa yako gas ya majumbani sio hii ya hapa kwetu, ni vyema ukae kimya kwenye hili maana utaaibika. Hilo la kwamba eti 30% ndio izalishe umeme wa nchi nzima, hapa pia umeonyesha uelewa finyu. Kwanza unajua tunahitaji % kiasi gani ili kuzalisha umeme wa kututosha? Huenda tunahitaji 10-20% tu kwa mahitaji yetu. Nakushauri kwenye hili la gas, hebu jipe muda wa kujua nini unaoongea, maana naona unabebwa na hisia zaidi, huku ukionyesha huna lolote ulijualo kwenye hili.

Hilo la mradi wa Bagamoyo, mimi nadhani ni rahisi, huo mkataba na hata wakati unazuiwa tulishauri mapungufu ya mkataba yaangaliwe, kisha yafanyiwe kazi halafu mradi uendelee. Lakini sio unazuia mkataba huo huku kukiwa na kificho cha mkataba husika, halafu unaenda kujenga uwanja wa ndege wa karibia 40b kijijini kwako, huku kukiwa hakuna uhitaji wowote wa hivyo.
 
Kama Huwezi kutofautisha l na r wewe ni mburula. Kwenye miradi unaandika miladi. Huna ubongo wa kushiriki mjadala huu. Nenda kaoge umsubiri mumeo

muda uliopoteza kujua r na l zinatakiwa zikae wapi,ungeutumia kwenye mambo mengine,usingekuwa hapa unajadili umuhimu wa umeme wa maji.


ni jitu jinga tu,ndio halijui hata gharama za uzalishaji wa umeme wa vyanzo vingine ila linajua matumizi ya r na l.
 
bi samia ana mwezi madarakani.

mmeshamshangilia kana kwamba hakuwahi kuwepo kabisa duniani.

Tunamshangilia kwa kujitenga na siasa za kidhalimu, lakini tathmini halisi ya awali ya utendaji wake, tutaitoa ndani ya siku 100.
 
Elimu ya Watanzania kwa kweli ni duni. Unajuwa kabisa wako kwenye mgogoro na Misri kuhusu Grand Renaissance Dam bado unaniuliza je wamekurupuka?

Jibu ni ndiyo wamekurupuka. Walipaswa kuangalia treaties za mwaka 1893 na nyingine ya 1910

wewe ni bungo maji kabisa.
 

umezingatia nini kuandika haya!!!

huyu CAG mwenye pua kama kitenesi,ndio kaandika hiyo tathmini yake.bado una nafasi ya kufikiri kwa kina.si kila msomi ana akili.

tanzania bado inahitaji umeme wa bei nafuu zaidi,ili kuendana na hali ya maisha yetu ya kila siku,mmawaza umeme wa neuclear na gesi mnajua gaharama zake na bei kwa kila moja!!!
life span ya mtera dam ni mwaka wa ngapi sasa na inaelekea kuacha kufua umeme lini??
 
Tunamshangilia kwa kujitenga na siasa za kidhalimu, lakini tathmini halisi ya awali ya utendaji wake, tutaitoa ndani ya siku 100.

nikafikiri ni baada ya miaka hata miwili hivi.

unajua ndio maana hamueleweki mnasimamia kitu gani.leo samia kwa kutamka tu maneno jukwaani anaonekana sio wale wale,ila utendaji ukiwa tofauti mnatumia majukwaa tena kumpinga.

ifae kuswma CCM inajua mdhaifu yenu,na namna ya kudeal nayo.
 
Akili azitoe wapi wakati kachanganya audit ambazo sio sehemu ya majukumu yake.

Environmental audit ni kazi ya NEMC sio CAG. Kichele ni fisadi alietumwa kumchafua Magufuli he needs to be sucked.

hawa watoto tunawaambia hapa wanaleta hisia tu mkuu.

kama wana nia njema na taifa hili wasitishe tu miladi yote.
halafu sisi wananchi tutawahoji wanataka tanzania ipi isiyo na umeme wa uhakika??isiyo na reli ya uhakika?,isiyo na shirika la ndege la uhakika??,wala miundombinu ya uhakika.
 
Ngereja hata bungeni hayupo ataibukia wapi ?
 
Hoja za Dam55 zimekuzidi uwezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…