Elias Msuya
Platinum Member
- Dec 23, 2011
- 267
- 1,014
Gwiji la sheria, Profesa Issa Shivji amesema Taifa haliwezi kuponywa wala kujenga demokrasia ya kweli ikiwa hakuna uwajibikaji wa kisheria dhidi ya mauaji ya raia yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Ameyasemanhayo leo Agosti 28, 2026 katika kongamano la Tanzania Democracy lililofanyika katika ukumbi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Dar es Slaam, ambapo ametoa tathmini hali ya demokrasia na masomo yanayopatikana kutokana na uchaguzi huo
Profesa Shivji ameeleza kuwa hadi sasa hakuna hatua zozote za kuwawajibisha waliohusika na maafa hayo, jambo linalotishia ustawi wa nchi.
"Tupo katika maombolezo kutokana na yaliyotokea Oktoba 29, 2025. Hakuna aliyewajibishwa kisheria.
"Mauaji yaliyotokea hakuna aliyefyatua risasi akawajibishwa, hakuna aliyeamrisha amewajibushwa, hakuna aliyesimamia amewajibishwa. Huwezi ukaliponya taifa bila uwajibikaji," amesema.
Misingi Mikuu ya Demokrasia na Utu
Katika uchambuzi wake kuhusu demokrasia, Profesa Shivji alitofautisha kati ya "haki" na "uhuru," akihimiza matumizi zaidi ya dhana ya uhuru:
"Napendelea kutumia dhana ya uhuru kuliko haki, kwa sababu uhuru ni kitu kinachopambaniwa, wakati haki ni kitu unachopewa."
Akitaja misingi mikuu mitatu ya demokrasia—Uhuru, Utu, na Usalama—alibainisha kuwa mambo hayo yameshuka thamani sana nchini. Uhuru wa kujieleza na kujumuika umeunganishwa moja kwa moja na utu wa binadamu, lakini vitendo vya kuteka, kudhalilisha, kutesa na kupoteza watu vimeharibu kabisa msingi wa utu. Aliongeza kuwa hata umaskini na ukosefu wa ajira kwa vijana ni aina nyingine ya udhalilishaji wa utu wa mwananchi.
Uhalali wa Watawala na Wito kwa Vijana
Kwa upande wa watawala, Profesa Shivji alifafanua kuwa serikali yoyote inahitaji Uhalali (Social Justice), Uwajibikaji (Uchaguzi Huru na wa Haki), na Uwazi. Alionya kuwa serikali nyingi zimekosa uwazi, hasa katika uwekaji wa mikataba mikubwa ya nchi.
Akimalizia tathmini yake, Profesa Shivji alitoa wito kwa vijana kutafakari upya mfumo wa demokrasia nchini:
Alisema Mfumo uliozoleka wa 'Liberal Democracy' umeshindwa kwani umezalisha ufisadi, wizi, na rushwa.
"Vijana wasizungumzie siasa pekee kama jambo la kufikirika, bali waiunganishe na mfumo wa kiuchumi unaowagusa wananchi wa kawaida," amesema.
View: https://www.youtube.com/live/yhSZ0PpXR6s?si=2fvOakUOLxZ849Y1