Profesa Shivji: Hatuwezi kuliponya Taifa bila kuwawajibisha waliotekeleza mauaji Oktoba 29, 2025

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014


Gwiji la sheria, Profesa Issa Shivji amesema Taifa haliwezi kuponywa wala kujenga demokrasia ya kweli ikiwa hakuna uwajibikaji wa kisheria dhidi ya mauaji ya raia yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Ameyasemanhayo leo Agosti 28, 2026 katika kongamano la Tanzania Democracy lililofanyika katika ukumbi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Dar es Slaam, ambapo ametoa tathmini hali ya demokrasia na masomo yanayopatikana kutokana na uchaguzi huo

Profesa Shivji ameeleza kuwa hadi sasa hakuna hatua zozote za kuwawajibisha waliohusika na maafa hayo, jambo linalotishia ustawi wa nchi.

"Tupo katika maombolezo kutokana na yaliyotokea Oktoba 29, 2025. Hakuna aliyewajibishwa kisheria.
"Mauaji yaliyotokea hakuna aliyefyatua risasi akawajibishwa, hakuna aliyeamrisha amewajibushwa, hakuna aliyesimamia amewajibishwa. Huwezi ukaliponya taifa bila uwajibikaji," amesema.

Misingi Mikuu ya Demokrasia na Utu
Katika uchambuzi wake kuhusu demokrasia, Profesa Shivji alitofautisha kati ya "haki" na "uhuru," akihimiza matumizi zaidi ya dhana ya uhuru:
"Napendelea kutumia dhana ya uhuru kuliko haki, kwa sababu uhuru ni kitu kinachopambaniwa, wakati haki ni kitu unachopewa."

Akitaja misingi mikuu mitatu ya demokrasia—Uhuru, Utu, na Usalama—alibainisha kuwa mambo hayo yameshuka thamani sana nchini. Uhuru wa kujieleza na kujumuika umeunganishwa moja kwa moja na utu wa binadamu, lakini vitendo vya kuteka, kudhalilisha, kutesa na kupoteza watu vimeharibu kabisa msingi wa utu. Aliongeza kuwa hata umaskini na ukosefu wa ajira kwa vijana ni aina nyingine ya udhalilishaji wa utu wa mwananchi.

Uhalali wa Watawala na Wito kwa Vijana
Kwa upande wa watawala, Profesa Shivji alifafanua kuwa serikali yoyote inahitaji Uhalali (Social Justice), Uwajibikaji (Uchaguzi Huru na wa Haki), na Uwazi. Alionya kuwa serikali nyingi zimekosa uwazi, hasa katika uwekaji wa mikataba mikubwa ya nchi.

Akimalizia tathmini yake, Profesa Shivji alitoa wito kwa vijana kutafakari upya mfumo wa demokrasia nchini:
Alisema Mfumo uliozoleka wa 'Liberal Democracy' umeshindwa kwani umezalisha ufisadi, wizi, na rushwa.
"Vijana wasizungumzie siasa pekee kama jambo la kufikirika, bali waiunganishe na mfumo wa kiuchumi unaowagusa wananchi wa kawaida," amesema.


View: https://www.youtube.com/live/yhSZ0PpXR6s?si=2fvOakUOLxZ849Y1
 
Gwiji la sheria, Profesa Issa Shivji amesema Taifa haliwezi kuponywa wala kujenga demokrasia ya kweli ikiwa hakuna uwajibikaji wa kisheria dhidi ya mauaji ya raia yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.✍🏿✔💪🏿
 
Watasema siyo raia achunguzwe
 
Halafu anatokea mburukenge kutoka Lumumba akiita mauwaji Yale ni ya watu wavutabangi na eti walikuwa vibaka?

Pumbavu kabisa

Damu Ile isipotendewa haki, itaangusha utawala wote wa maccm na anguko baya la chama chenu Cha mauwaji
 
Huyu mzee watamtafutia case ya uhaini, serikali ya awamu hii, wanajua kubambikia case, kuteka, kuua. Baasi.

Wana avoidd backlash kenye jamii maana mzee hayuko affiliated na pande yoyotr anaongea facts.
Ila kama ujuavyo wajinga wakishika hatam mambo yanakuwaje
 
Hana deni mzee huyu na wote waliojitokeza wamekubali kusimama na sisi kwenye kipindi hichi kigumu bila hofu wala mashaka
 
Suala la msingi, mengine baadaye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…