Profesa Shivji: Mkataba wa Bandari unaegamia zaidi upande mmoja na hauna ukomo wa muda. Hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile

Nawakumbusha tu huyo ni Profesa wa sheria kwahiyo mnapochangia mkumbuke hili.
 
Unatoka hapa unaenda Dubai au nje ya nchi kusaini mkataba unaohusu rasilimali yako, unafikiri nguvu za kubargain utazipata wapi?

Wenzetu wana akili, ukifika huko wanakutreat kama mfalme, utapewa hotel ya nyota 5 na kila kitu cha thamani utumie. Ukirudi kwenye mkataba huna tena nguvu ya kukataa au kubisha

Waziri wa Kenya nae ilimkuta hii wakati dp world wanaitaka bandari ya Mombasa. Yule waziri kurudi Kenya akakutana na vikwazo, dp world wakakataliwa.

Waafrica tukubali tuna shida sehemu. Hotel ya nyota 5, shopping na vitu vya kupita tunavipa thamani Sana bila kujali mustakabali wa nchi kesho.

Falme za kiarabu wangecheza na mafuta yao, Kama siso tunavyocheza na vya kwetu, leo hii hata hiyo Dubai isingekuwepo
 
Issue si uamuzi wa kufurahisha, ni uamuzi wa kuuza uhuru na ardhi ya nchi.
 
Mkataba huu (wa bandari) unaegemea zaidi upande mmoja na pia hauna ukomo wa muda. Wajibu wote ni wajibu wa serikali ya Tanzania lakini haki zote ni haki za DP WORLD

Watu waliokuwa wanasema mkataba wa bandari ni wa miaka 100 hawakuwa wanamaanisha moja kwa moja ni miaka 100, walichomaanisha ni kuwa mkataba huu ni wa muda mrefu. Na ni kweli ni mkataba wa muda mrefu na utaisha pale ambapo mikataba yote ya miradi saba ya awamu ya kwanza itapokuwa imetekelezwa. Na kama kutakuwa na migongano au mifarakano, hadi itakapokuwa imetatuliwa.

DP WORLD wakipata faida huwezi kuwatoza kodi lakini pia hakuna kifungu chochote (katika mkataba wa bandari) kinachozungumzia revenue sharing (mgawanyo wa mapato), kama nchi itafaidika vipi?

Mkataba huu hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile hata kama tumevunja uhusiano wa kidplomasia na U.A.E (Falme za Kiarabu)

Shughuli zilizotajwa katika awamu ya kwanza (ya mkataba wa bandari) sio za bandari pekee, kuna Special Economic Zone (maeneo mahususi ya kiuchumi), trade corridor, free zone.

Eneo ambalo sio la DP WORLD lakini ni karibu na eneo la DP WORLD, mtu akitaka kujenga barabara au flyover ambayo interfere (itaingilia) shughuli za DP WORLD hairuhusiwi kwa mujibu wa mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari). Serikali itahakikisha kwamba shughuli hizo hazitokuwepo kando kando na eneo la DP WORLD.

Profesa Issa Shivji
Mdahalo UDSM kuhusu Suala la Bandari



Chanzo: Jambo TV
 
hyu mzee ni jasiri na mzalendo kuliko yule scout master mvaa ma-skafu waziri.. na sio kwa tukio hili tu
 
... kuna kifisadi kimoja kimebebwa na jina huko Bungeni uliletwa uzi humu jana kikidai kama mwenye nchi kakubali chenyewe ni nani kipinge? Serpent offspring is also a serpent!
Serpent brought us all this 🤣🤣
 
Chocheeni kuni tanuru Bado haijaiva 👍👍
 
Basi vizuri
 
Nawakumbusha tu huyo ni Profesa wa sheria kwahiyo mnapochangia mkumbuke hili.
Born in Kilosa, Tanzania in 1946, Shivji was for 36 years a distinguished professor in constitutional law in the University of Dar es Salaam's Faculty of Law. He is a professor of international renown, having built his reputation through the publication of over 18 books, numerous articles and book chapters. Shivji has served as advocate of the high court and the Court of Appeal of Tanzania since 1977 and advocate of the high court in Zanzibar since 1989.

He has received several national and international distinguished scholar awards, including an honorary doctorate from the University of East London, UK and one from Rhodes University, South Africa. Shivji has devoted most of his life to addressing issues on the exploitation of Tanzanians through both the national and the international economic and legal orders. Shivji presently occupies the Mwalimu Julius Nyerere Research Chair in Pan-African Studies of the University of Dar es Salaam.

Most recently, he has been working on the political economy of economic reforms in Tanzania. While mostly based in Tanzania, he has been visiting professor in various locations: El Colegio De Mexico, the University of Zimbabwe, the University of Warwick, the National Law School of India University, the University of Hong Kong, the Centre of African Studies of the University of Cape Town, South Africa, the Institute for Poverty, Land and Agrarian Studies at the University of the Western Cape and CODESRIA, Dakar, Senegal.

Shivji earned his LL.M and PhD at the London School of Economics and Political Science (LSE) and the University of Dar es Salaam respectively. He also holds an LL.B from the University of Dar es Salaam in Tanzania. He is married with children, his son Amil Shivji is a filmmaker. ... (c) Wikipedia.
 
Ikiwa serikali itaziba masikio na kuendelea na jambo hili
La Bandari na mkataba huu basi miaka ijayo yakitokea mambo ambayo watu walikuwa wanaionya serikari basi ndio utakuwa mwisho na amani aliyoanzisha mwalimu ,machafuko tuyatengee na Tanganyika mambo ya sudani yanaweza kutokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…