Profesa Shivji: Mkataba wa Bandari unaegamia zaidi upande mmoja na hauna ukomo wa muda. Hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile

Profesa Shivji: Mkataba wa Bandari unaegamia zaidi upande mmoja na hauna ukomo wa muda. Hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile

Wakishamaliza kugawana keki ya taifa, watakuja mpaka kwenye maboga na viazi vyetu.
 
Mkataba huu (wa bandari) unaegemea zaidi upande mmoja na pia hauna ukomo wa muda. Wajibu wote ni wajibu wa serikali ya Tanzania lakini haki zote ni haki za DP WORLD

View attachment 2671928

Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari) ni mkataba kati ya nchi na nchi kuhusu uwekezaji, na mkataba unasema ni kuhusu ushirikiano wa kiuchumi lakini ukweli ni kwamba mkataba huu ni aina ya mikataba ya uwekezaji

Katika mkataba huu wa bandari kuna mambo mawili, jambo la kwanza, mkataba unahusu ushirikiano wa kiuchumi lakini sio ushirikiano wa kiujumla bali ni katika eneo la bandari za bahari na bandari za maziwa. Na jambo la pili ni kwamba mwekezaji ameshatambulika

Watu waliokuwa wanasema mkataba wa bandari ni wa miaka 100 hawakuwa wanamaanisha moja kwa moja ni miaka 100, walichomaanisha ni kuwa mkataba huu ni wa muda mrefu. Na ni kweli ni mkataba wa muda mrefu na utaisha pale ambapo mikataba yote ya miradi saba ya awamu ya kwanza itapokuwa imetekelezwa. Na kama kutakuwa na migongano au mifarakano, hadi itakapokuwa imetatuliwa.

Mkataba huu hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile hata kama tumevunja uhusiano wa kidiplomasia na U.A.E (Falme za Kiarabu)

Chanzo: Jambo Tv
Hata uki plead non est factim huutengui.
 
Spinning.


Huo mkataba wa bandari uko wapi?

Uwekeni hapa, kuna MOU ya TPA na DP World mbona hamuiweki ujionee?
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Nipo hapa na mimi nasubiria majibu bloangu
 
MWENDO NI ULE ULE.

IMG_7387.jpg

IMG_7381.jpg

IMG_7386.jpg



SABABU ZINAJIELEZA HAPO JUU
 
Najiuliza sana!

Inawezekanaje Profesa Shivji awe mwanasheria na azijue sheria kumzidi mbobezi wetu wa sheria ndugu Zembwela?!

Kwamba mnataka niamini Shivji ni nguli wa sheria kumzidi Maulid Kitenge!

Eti Profesa Shivji ana mzidi kudadavua sheria za mikataba mwana sheria mbobezi wa sheria za mikataba ndugu Msigwa?!

Acheni kuniaminisha ujinga atiii!

NB: Mod, andiko langu ni swali tafadhari msiuunganishe ili niweze kupata majibu.
Ni wajinga tu watakaomwamini Shivji na kumpuuza Mwanasheria Mbobezi kama Zembela na Jaji aliyehukumu kesi nyingi za migogoro ya mikataba Mheshimiwa Maulid Mwana wa Kitenge.
 
Shivji hajaona kifungu cha 5:4?


Wazi kabisa kinasema miezi 12 au ile miezi 12 mkataba uliiweka pale ya nini?


Nyinyi hata mki spin vipi, mkataba ni mwema sana kuliko mikataba yote tuliongia nchi hii.

Hicho kifungu unakielewaje, ili tujadiliane? Nanukuu kwa tafsiri isiyo rasmi:
5:4. Nchi Wanachama zinakubali kwamba Miradi ya Awamu ya 1 (kama ilivyofafanuliwa katika Kiambatisho 1) itakuwa ndiyo miradi ya kipaumbele katika kuiendeleza na kuitekeleza. Serikali ya Tanzania itahakikisha kwamba TPA haitaongeza mapendekezo mengine yoyote ya Miradi yoyote ya Awamu ya 1 kuanzia Tarehe ya Kusainiwa hadi tarehe ambayo majadiliano kati ya DPW na TPA kwa Miradi ya Awamu ya 1 yamesitishwa au baada ya kumalizika muda wa miezi 12 kutoka Tarehe ya kusainiwa kwa Mkataba huu, yoyote iliyo ya mapema.
 
Jeshi liko wapi ili litimize wajibu wake wa kikatiba wa kulinda uhuru na mipaka ya nchi?

Ina maana jeshi halijui kuwa bandari ni mpaka?

Ina maana Jeshi halioni kuwa kwa mkataba huu Sovereignity ya nchi iko pabaya?

Majeshi ya nchi yanayojitambua hayawezi kukubaliana na kitu kama hiki!
Jeshi linalokubali kutumika kisiasa haliwezi kufanya lolote nje ya mitazamo ya watawala. Kinachofanyika ni kuhakikisha viongozi wa jeshi wanapata marupurupu yasiyoendana na kazi yao, kisha kwa ajili ya ubinafsi wanawatii viongozi wa kisiasa hata kwa mambo ya hatari.
 
Shivji Mkomunisti huyo, anapenda siasa za kimaskini.
Kwani kakataa uwekezaji au kaeleza mkataba ulivyo!¿
Tatizo mnapenda kusikia mnayoyataka......ukweli hauna tabia hizo, yaani hauna kona
 
Back
Top Bottom