Profesa wa Chuo Kikuu Oxford amshauri Rais Samia kuhusu miradi aliyoianzisha Hayati Magufuli kwa pupa

Profesa wa Chuo Kikuu Oxford amshauri Rais Samia kuhusu miradi aliyoianzisha Hayati Magufuli kwa pupa

Profesa Stefan Dercon amekubaliana na comments nyingi ambazo wana JamiiForums wamekuwa wakitupia hapa tangu enzi za Rais John Pombe Magufuli yupo madarakani.


Sasa kwa kuwa maoni ya nguli huyu wa chuo kikuu cha Oxford umewekwa gazeti, ushauri kwa serikali iwe inachukua hatua haraka maoni ya wanaJF badala ya kusubiri ushauri wa kutoka nje ambao umekuja umechelewa na nchi ina mzigo mzito wa "mamiradi"



SPICE FM

Prof. Stefan Dercon ni mjuzi wa mazingira ya Tanzania kwa kina na pia ameandika kitabu cha Gambling on Development / Kucheza Kamari ya Maendeleo ...

PROF. STEFAN DERCON - GAMBLING ON DEVELOPMENT
Explained : Why Some Countries Win Economically and Others Lose - Prof. Stefan Dercon


Source : SpiceFM

Hakuna kitu zaidi ya kurudishana nyuma tu
 
Wasimchanganye. Wanataka kumtoa kwenye reli maana wanajua ni wale wa kujipendekeza kwa wazungu.
Miradi wala sio ya magafuli ila ni ilani za chama cha mapinduzi. Mama ashikilie tu usukani hakuna mradi wowote utakua wa hasara. Wao wanapofikiria hasara wanafikiria muwekezaji binafsi lakini miradi yetu ni ya umma. Haijaanzishwa kiwazimu. Faida zake mingi ni ya kuonekana muda mfupi na mingi muda mrefu.
 
Profesa wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Oxford amemshauri serikali ya Samia kuwa na uangalifu kuhusiana na kutekeleza miradi mikubwa aliyoianzisha Magufuli kwa pupa kwa kuwa inaweza kuliingiza taifa kwenye madeni makubwa yatakayoathiri uchumi wake

Magufuli alipoingia madarakani alianzisha miradi mingi kwa fujo kama vile kuhamia Dodoma, ununuzi wa ndege kwa fujo, ujenzi wa SGR, ujenzi wa bwawa la Nyerere huku akihadaa wananchi wasio na uelewa kuwa miradi hiyo yote inatekelezwa kwa fedha za ndani

Hadi sasa deni la taifa linakribia kufikia trilioni 100 kutokana na miradi hiyo kutumia fedha nyingi, na hakuna uhakika itakamilika lini

View attachment 2497178
Hao Ma-ProfJalalans wako wapi mpaka Ma-ProfBeberus watushauri.
 
Tizama hakuna mradi hata mmoja mbaya. Miradi yote hii ilitakiwa itekelezwe na marais waliopita lakini....Huyu rais mmoja alikuja na kutekeleza yote tena kwa kipindi kifupi. Tatizo liliopo ni kwamba hakuna msimamizi na mfuatiliaji Basi huo ndio ukweli....Nchi lazima iwe na ndege zake angalia nchi kama Swaziland au Malawi pamoja na umasikini wao wanazo ndege zao sembuse TZ.. Mwanamume anaweza kukosa kuwa na rungu lakini bakora lazima anakuwa nayo kama hana basi sio Mwanamme huyo. Kule Zanzibar rais Karume 1 alijenga yale magorofa marefu mengi tu na kuvunja zile nyumba za majani zilizokuwepo zamani na asingefanya hivyo mpaka leo zingekuwepo. Toka alipokufa marais waliomfuata walishindwa kujenga hata jumba moja mpaka alipokuja rais Karume mwanae akamalizia jengo moja tena kwa taabu na mikopo mingi. Hata hivyo supplier wa matofali anajulikana vizuri ni nani. Ukitaka kufanya maendeleo ya nchi unahitaji kufanya maamuzi magumu tena unafanya maamuzi kama huna akili nzuri vile, bila ya kujali matusi na kejeli za watu hapo utafanikiwa.
 
Back
Top Bottom