Profesa wa Chuo Kikuu Oxford amshauri Rais Samia kuhusu miradi aliyoianzisha Hayati Magufuli kwa pupa

Hakuna kitu zaidi ya kurudishana nyuma tu
 
Wasimchanganye. Wanataka kumtoa kwenye reli maana wanajua ni wale wa kujipendekeza kwa wazungu.
Miradi wala sio ya magafuli ila ni ilani za chama cha mapinduzi. Mama ashikilie tu usukani hakuna mradi wowote utakua wa hasara. Wao wanapofikiria hasara wanafikiria muwekezaji binafsi lakini miradi yetu ni ya umma. Haijaanzishwa kiwazimu. Faida zake mingi ni ya kuonekana muda mfupi na mingi muda mrefu.
 
Hao Ma-ProfJalalans wako wapi mpaka Ma-ProfBeberus watushauri.
 
Tizama hakuna mradi hata mmoja mbaya. Miradi yote hii ilitakiwa itekelezwe na marais waliopita lakini....Huyu rais mmoja alikuja na kutekeleza yote tena kwa kipindi kifupi. Tatizo liliopo ni kwamba hakuna msimamizi na mfuatiliaji Basi huo ndio ukweli....Nchi lazima iwe na ndege zake angalia nchi kama Swaziland au Malawi pamoja na umasikini wao wanazo ndege zao sembuse TZ.. Mwanamume anaweza kukosa kuwa na rungu lakini bakora lazima anakuwa nayo kama hana basi sio Mwanamme huyo. Kule Zanzibar rais Karume 1 alijenga yale magorofa marefu mengi tu na kuvunja zile nyumba za majani zilizokuwepo zamani na asingefanya hivyo mpaka leo zingekuwepo. Toka alipokufa marais waliomfuata walishindwa kujenga hata jumba moja mpaka alipokuja rais Karume mwanae akamalizia jengo moja tena kwa taabu na mikopo mingi. Hata hivyo supplier wa matofali anajulikana vizuri ni nani. Ukitaka kufanya maendeleo ya nchi unahitaji kufanya maamuzi magumu tena unafanya maamuzi kama huna akili nzuri vile, bila ya kujali matusi na kejeli za watu hapo utafanikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…