Professor Jeffrey Sachs: Marekani inapigana vita vya Netanyahu

Marekani ina wanasayansi Wayahudi na si waisirael nyinyi mtu akisha kuwa myahudi basi ni muisrael?
Marekani ana isaport Israel kwa kila namna kwa sababu ya kuitumia kuivuruga na kudhibiti mashariki ya kati basi hakuna zaidi ya hilo.
Hizo hoja za wanasayansi hazina mashiko kwa sababu Marekani ina wanasayansi kutoka karibia kila asili hapa duniani .
Vipi na Ukrain nayo ina wanasayansi wangapi ndani ya Marekani mbona ndo inateketeza pesa za walipa kodi wa Marekani mara 5 ya Israel?
Au Misri na Pakistan wana wanasayansi wangapi nchini Marekani mbona kila mwaka anatoa mabilion ya dora kila mwaka kwa nchi hizo?

Mbona wasomi na wanasayansi wa kiajemi walio jazana Marekani hamuwaiti wairan?
Sera nzima ya mambo ya nje ya Marekani inatawaliwa na maslahi yake ya kijiografia na kiuchumi. Huo ndio ukweli.

Kwa nini Iran, Syria na Yemen zimetengwa na Marekani na washirika wake? Kwa nini Gaddafi na Saddam waliondolewa madarakani na nchi za Magharibi? Kwanza hawakuwa na uhusiano wowote na ukiukwaji wao wa haki za binadamu kama US ilivyosema ,sasa kwanini US ikawatoa kwa nguvu madarakani Libya , Iraq na sasa Syria?

Biden anajibu....
"Kama hakungekuwa na Israeli, Ameerika ingelazimika kubuni Israeli kulinda masilahi yake katika eneo hilo."
- Joe Biden

Screenshot 2025-01-13 232833.png

source: Biden says the U.S. would have to invent an Israel if it didn’t exist. Why?
 
Marekani ina wanasayansi Wayahudi na si waisirael nyinyi mtu akisha kuwa myahudi basi ni muisrael?
Marekani ana isaport Israel kwa kila namna kwa sababu ya kuitumia kuivuruga na kudhibiti mashariki ya kati basi hakuna zaidi ya hilo.
Hizo hoja za wanasayansi hazina mashiko kwa sababu Marekani ina wanasayansi kutoka karibia kila asili hapa duniani .
Vipi na Ukrain nayo ina wanasayansi wangapi ndani ya Marekani mbona ndo inateketeza pesa za walipa kodi wa Marekani mara 5 ya Israel?
Au Misri na Pakistan wana wanasayansi wangapi nchini Marekani mbona kila mwaka anatoa mabilion ya dora kila mwaka kwa nchi hizo?

Mbona wasomi na wanasayansi wa kiajemi walio jazana Marekani hamuwaiti wairan?
Kila nchi ina sababu zake mahususi na muktadha wake wa kusaidiwa na Marekani, msaada wa Marekani kwa Tanzania hauwezi kufanana na msaada wa Marekani kwa Haiti, hili halipaswi kuwa jambo gumu sana kuelewa.

Pia hakuna pesa za walipa kodi wa Marekani zinazoteketea Ukraine. Msaada mkubwa unaoenda Ukraine ni silaha ambazo zinazalishwa na makampuni ya silaha ya Marekani. Serikali ya Marekani inayalipa pesa makampuni ya silaha ya Marekani yaliyoajiri Wamarekani na yanayolipa kodi Marekani.
 
Sera nzima ya mambo ya nje ya Marekani inatawaliwa na maslahi yake ya kijiografia na kiuchumi. Huo ndio ukweli.

Kwa nini Iran, Syria na Yemen zimetengwa na Marekani na washirika wake? Kwa nini Gaddafi na Saddam waliondolewa madarakani na nchi za Magharibi? Kwanza hawakuwa na uhusiano wowote na ukiukwaji wao wa haki za binadamu kama US ilivyosema ,sasa kwanini US ikawatoa kwa nguvu madarakani?

Biden anajibu....
"Kama hakungekuwa na Israeli, Ameerika ingelazimika kubuni Israeli kulinda masilahi yake katika eneo hilo."
- Joe Biden

View attachment 3201208
source: Biden says the U.S. would have to invent an Israel if it didn’t exist. Why?
Sera ya Marekani ya mambo ya nje ni pana zaidi kuliko jiografia na maslahi ya uchumi, usalama wa raia wake ni jambo muhimu sana pia hata pale ambako hakuna maslahi ya kiuchumi. Pia kuna suala la utamaduni, dini, ideology, historia n.k

Umechanganya mambo mengi sana pia tofauti katika kapu moja. Iran, Syria na Yemen zimekuwa na issues tofauti sana na Marekani, Gaddafi hakuuwawa na Wamarekani, uvamizi wa Iraq ilikuwa ni kupaniki kwa utawala wa Bush baada mfulilizo wa matukio ya ugaidi na hasa tukio la September 11.
 
Kila nchi ina sababu zake mahususi na wake wa kusaidiwa na Marekani, msaada wa Marekani kwa Tanzania hauwezi kufanana na msaada wa Marekani kwa Haiti, hili halipaswi kuwa jambo gumu sana kuelewa.

Pia hakuna pesa za walipa kodi wa Marekani zinazoteketea Ukraine. Msaada mkubwa unaoenda Ukraine ni silaha ambazo zinazalishwa na makampuni ya silaha ya Marekani. Serikali ya Marekani inayalipa pesa makampuni ya silaha ya Marekani yaliyoajiri Wamarekani na yanayolipa kodi Marekani.
Basi kwa mantiki hiyo Marekani ana isaport Israel kwa sababu ya kuhodhi siasa za Mashariki ya kati kwa sababu waarabu hawaaminiki anahofia kumgeuka wakati wowote na sio hizo ngojera zenu za sijui Marekani anawategemea waisirael kwenye sayansi sijui kitekinolojia.
Siku Israel ikianguka basi na ushawishi wa Marekani utakuwa umekufa automatically katika eneo la mashariki ya kati.

Marekani amepata maendeleo ya kiuchumi na kitekinolojia hata kabla ya Israel haijafikiliwa kuanzishwa.

Kuhusu kodi za wamarekani kutumika kwenye vita hayo sio maneno yangu bali ni maneno ya wamarekani wenyewe.
 
Sera ya Marekani ya mambo ya nje ni pana zaidi kuliko jiografia na maslahi ya uchumi, usalama wa raia wake ni jambo muhimu sana pia hata pale ambako hakuna maslahi ya kiuchumi. Pia kuna suala la utamaduni, dini, ideology, historia n.k

Umechanganya mambo mengi sana pia tofauti katika kapu moja. Iran, Syria na Yemen zimekuwa na issues tofauti sana na Marekani, Gaddafi hakuuwawa na Wamarekani, uvamizi wa Iraq ilikuwa ni kupaniki kwa utawala wa Bush baada mfulilizo wa matukio ya ugaidi na hasa tukio la September 11.
Iraq haikuvamiwa kwa sababu ya tukio la Sept 11, na ninaweza thibitisha hilo, Iraq ilivamiwa kwa kudhaniwa kuwa na silaha za maangamzi(WMD, Weapons Of Mass Destruction).
Baada ya kuivamia Iraq US na washirika wake hawakukuta hizo silaha za maangamizi kama walivyo aminisha washirika wake.

Sasa ndipo naomba unijibu kwanini US iliivamia Iraq? Je intel ya ya US ilikuwa chini kiasi kwamba hawakufahamu kama Iraq ina WMD au haina? Je ilivamia Iraq kisa kwa sababu zipi?
Au niseme tu 9/11 ilikuwa kisingizio...?

Tutaongea mengi sana hapa, hadi kuhusu kikundi kama Reaganite kilichoanzishwa mwaka 1997 ambapo ilikuwa ni think tank wakiitwa the Project for the New American Century, wikipedia page hii >>>> Project for the New American Century - Wikipedia
Ikisemekana kikundi hiki waliamua kuweka malengo kwamba nani ni mkubwa kuingia karne ya 21? nani ni boss kuingia karne ya 21? kwa kuzidhoofisha nchi ambazo ziliidharau USA ikiwa target kubwa wakati huo ni Saddam ambae alionyesha dunia UN na US ni wanyonge...

Petroldollar, Saddam alikuwa anaenda kuuza mafuta ya Iraq kwa sarafu ambayo haikuwa dola za Kimarekani na alikataa kuuza katika treasury bonds.
Na hilo ndilo jibu, Us imeziadhibu nchi nyingi ambazo hazikutaka kuuza mafuta yao kwa dola, na ndicho kimetokea Libya ilipotaka kuuza mafuta kwa dhahabu , na ndio ugomvi unaoendelea kati ya US ,Venezuela na Iran...
 
Marekani ina wanasayansi Wayahudi na si waisirael nyinyi mtu akisha kuwa myahudi basi ni muisrael?
Marekani ana isaport Israel kwa kila namna kwa sababu ya kuitumia kuivuruga na kudhibiti mashariki ya kati basi hakuna zaidi ya hilo.
Hizo hoja za wanasayansi hazina mashiko kwa sababu Marekani ina wanasayansi kutoka karibia kila asili hapa duniani .
Vipi na Ukrain nayo ina wanasayansi wangapi ndani ya Marekani mbona ndo inateketeza pesa za walipa kodi wa Marekani mara 5 ya Israel?
Au Misri na Pakistan wana wanasayansi wangapi nchini Marekani mbona kila mwaka anatoa mabilion ya dora kila mwaka kwa nchi hizo?

Mbona wasomi na wanasayansi wa kiajemi walio jazana Marekani hamuwaiti wairan?
Shida sisi waswahili mahaba ya Imani zetu tunayaleta kwenye jukwaa hili ,hebu tuwe tunazungumzia facts kama great thinkers . Mfano hawapo wanasayansi kutoka afrika, Elon musk tajiri namba Moja katokea wapi? Vipi mataifa mengine kama vile ujerumani Russia uingereza Irani misri ugiriki ,Je hakuna wanasayansi wenye asili ya hizo nchi marekani.au michango Yao haionekani
 
Elon Musk ni mwanasayansi wa kitu gani?
 
Iraq haikuvamiwa kwa sababu ya tukio la Sept 11, na ninaweza thibitisha hilo, Iraq ilivamiwa kwa kudhaniwa kuwa na silaha za maangamzi(WMD, Weapons Of Mass Destruction).
Baada ya kuivamia Iraq US na washirika wake hawakukuta hizo silaha za maangamizi kama walivyo aminisha washirika wake.

Sasa ndipo naomba unijibu kwanini US iliivamia Iraq? Je intel ya ya US ilikuwa chini kiasi kwamba hawakufahamu kama Iraq ina WMD au haina? Je ilivamia Iraq kisa kwa sababu zipi?
Au niseme tu 9/11 ilikuwa kisingizio...?

Tutaongea mengi sana hapa, hadi kuhusu kikundi kama Reaganite kilichoanzishwa mwaka 1997 ambapo ilikuwa ni think tank wakiitwa the Project for the New American Century, wikipedia page hii >>>> Project for the New American Century - Wikipedia
Ikisemekana kikundi hiki waliamua kuweka malengo kwamba nani ni mkubwa kuingia karne ya 21? nani ni boss kuingia karne ya 21? kwa kuzidhoofisha nchi ambazo ziliidharau USA ikiwa target kubwa wakati huo ni Saddam ambae alionyesha dunia UN na US ni wanyonge...

Petroldollar, Saddam alikuwa anaenda kuuza mafuta ya Iraq kwa sarafu ambayo haikuwa dola za Kimarekani na alikataa kuuza katika treasury bonds.
Na hilo ndilo jibu, Us imeziadhibu nchi nyingi ambazo hazikutaka kuuza mafuta yao kwa dola, na ndicho kimetokea Libya ilipotaka kuuza mafuta kwa dhahabu , na ndio ugomvi unaoendelea kati ya US ,Venezuela na Iran...
Hapo mkuu mi naweza kuchangia kidogo, au kuongezea nyama Marekani hawezi kubali liinuke taifa lolote la kiarabu liwe na nguvu kiuchumi au kijeshi bila mkono wake. Kwasababu litakuwa tishio Kwa mwanae isael na maslahi yake. Waarabu wanapopata nguvu nikitisho Kwa Marekani na Israel. Kwahiyo sera ya nje ya Marekani mashabiki ya kati ni uwe kibaraka wao au tukuvuruge
 
Mkuu, ukiwa mwekezaji unakuwa na mchango kwenye maendeleo ya sayansi, ninavyomchukulia huyu jamaa anachangia pakubwa katika eneo hilo
Sema anachangia nini katika sekta ya teknolojia za silaha hapo Marekani.
 
Iraq haikuvamiwa kwa sababu ya tukio la Sept 11, na ninaweza thibitisha hilo, Iraq ilivamiwa kwa kudhaniwa kuwa na silaha za maangamzi(WMD, Weapons Of Mass Destruction).
Baada ya kuivamia Iraq US na washirika wake hawakukuta hizo silaha za maangamizi kama walivyo aminisha washirika wake.

Sasa ndipo naomba unijibu kwanini US iliivamia Iraq? Je intel ya ya US ilikuwa chini kiasi kwamba hawakufahamu kama Iraq ina WMD au haina? Je ilivamia Iraq kisa kwa sababu zipi?
Au niseme tu 9/11 ilikuwa kisingizio...?

Tutaongea mengi sana hapa, hadi kuhusu kikundi kama Reaganite kilichoanzishwa mwaka 1997 ambapo ilikuwa ni think tank wakiitwa the Project for the New American Century, wikipedia page hii >>>> Project for the New American Century - Wikipedia
Ikisemekana kikundi hiki waliamua kuweka malengo kwamba nani ni mkubwa kuingia karne ya 21? nani ni boss kuingia karne ya 21? kwa kuzidhoofisha nchi ambazo ziliidharau USA ikiwa target kubwa wakati huo ni Saddam ambae alionyesha dunia UN na US ni wanyonge...

Petroldollar, Saddam alikuwa anaenda kuuza mafuta ya Iraq kwa sarafu ambayo haikuwa dola za Kimarekani na alikataa kuuza katika treasury bonds.
Na hilo ndilo jibu, Us imeziadhibu nchi nyingi ambazo hazikutaka kuuza mafuta yao kwa dola, na ndicho kimetokea Libya ilipotaka kuuza mafuta kwa dhahabu , na ndio ugomvi unaoendelea kati ya US ,Venezuela na Iran...
Tangu Urusi iache kuuza gas, mafuta na rasilimali zake nyingine kwa dola ya Marekani nini kimetokea kwa $? Kipi kimebadilika kwa dola ya Marekani??

Mambo ya ubora wa taarifa za Intelejensia kuhusu maadui wa Marekani hayakutiliwa umuhimu tena baada ya September 11, sera ya Bush ilibadilika na kuwa ni "either you are with us, or you are with the terrorists'' , “Shoot first, ask questions later” na ni kwa mrengo huo ndivyo Iraq walivyovyamiwa. Hakuna cha Saddam sijui kuachana na petroldollar, kutumia gold au mashanikizo ya Industrial military complex kama conspiracists wengi wanavyoamini.
 
Israel ya zamani ilisha futwa na Roma makarne kibao yaliyo pita tatizo lilikuja pale watu walipo taka kurudisha taifa ambalo limesha kufa miaka mingi sana iliyo pita.

Kwa mfano leo hii tukitaka tufufue mataifa yaliyo anguka na kufa miaka mingi iliyo pita hii dunia haiwezi kukalika.
Wewe sio mkristo ndo maana huwezi elewa hivi vitu

Wakati wa mfalme wa mwisho wa yuda sedekia kupitia nabii yeremia israel ilipewa ya kwenda ulaya kama utumwa kwa kuwa wakaidi na kutumikukia miungu mingine

Kwa sababu ya agano la ibrahim, isaka na jacob waliahidiwa watarudi lakin hawakujua ni lini exactly adhabu itaanza na lini watarudi

Baada ya kumsulubusha Yesu ndo hapo adhabu ya kwenda utumwan ulaya ilianza walipelekea kwa lazima lakini ilikua ni sehemu ya adhabu

Kuanzia miaka 1800 waisraeli kila kona walikua wanapigwa vita ulaya in-short mda wao wa utumwa ulaya ulikua umeishaisha ila hawakuelewa alichofanya hitler ni kuhitimisha kile ambacho kilianza miaka ya 1980 na kutumiza agano la Mungu alilolisema kupitia kinywa cha yeremia
 
Sema anachangia nini katika sekta ya teknolojia za silaha hapo Marekani.
Bila sataraiti za Aron musk Ukraine ingepoteana kwenye uwanja wa vita maana Urusi ilikuwa imefanikiwa kuvuruga mifumo ya mawasiliano kwenye jeshi la Ukraine.
 
Dunia haiongozwi kwa misingi wala sheria za kikirisito bali inaongozwa na sheria za kimataifa.
 
Huwezi helewa ila biblia kwa asilimia kubwa imeelezea historia ya wayahudi na Mungu wao (Yahweh) kile alichoongea kupitia kinywa cha yeremia ndo kimeshatimia kwamba wataenda ulaya kama watumwa na kurejea imetimia mwaka 1948
 
Yeye kawezekeza kwenye eneo la mawasiliano yaani satellite ambayo ni muhimu kijeshi, tumeona hata Ukreni amefaidika kwenye uwanja wa vita. Pia mawasiliano ya kwaida mfano internet
Starlink za Elon Musk huko Ukraine ni kwa ajili ya matumizi ya internet ya kiraia kama zilivyo kwenye nchi nyingine mfano Kenya n.k kilichotokea ni kwamba Ukraine walianza kutumia internet ya Starlink kijeshi ndipo kelele zikazuka. Starlink zinatumika Cuba, Iran, Gaza n.k Inashangaza unaposema ni silaha ya kijeshi. Starlink ni sawa na barabara, bandari au Airport tu inayoweza kutumika kiraia au kijeshi kupitishia silaha.
 
Bila sataraiti za Aron musk Ukraine ingepoteana kwenye uwanja wa vita maana Urusi ilikuwa imefanikiwa kuvuruga mifumo ya mawasiliano kwenye jeshi la Ukraine.
Msipende kurahisisha mambo magumu kirahisi hivyo, starlink zina miaka mitano tu, watu wamekuwa wanapigana vita kwa maelfu ya miaka kwa namna nyingi tu za mawasiliano.
 
Back
Top Bottom