Projects za Mchungaji Kimaro akiwa KKKT Kijitonyama

Projects za Mchungaji Kimaro akiwa KKKT Kijitonyama

Safi sana Kimaro!

Kwapiga kwenye mshono! Yani mlitaka aondoke pale usharikani kimyakimya bila kusema?

Aondoke tu akafungue kanisa lake. Kwanza Kimaro sio mchungaji per se ni motivational speaker. Mjungaji huwezi kusema vijana wa dini Fulani sio waaminifu. Umefanya research wapi? Mchungaji alitakiwa awaite vijana awafundishe uaminifu.
 
Tujikumbushe, projects kadhaa ambazo Mchungaji Dkt. Kimaro amezifanya akiwa Mchungaji Kiongozi, KKKT Usharika wa Kijitonyama,
1. School of Healing (Morning & Evening Glory) -Youtube Channel (mwanzoni ikiwa Eliona Kimaro TV baadae KKKT Usharika wa Kijtonyama) inayowafikia watu wote Duniani.
2. TAMASHA LA MBINGU KUJAA SIFA (kila mwaka)
3. Jengo jipya la Sunday School (lililogharimu yapata takribani 200m TZS)
4. Ununuzi wa Kiwanja pembezoni mwa kanisa yapata 300m TZS
5. Kusomesha yatima yapata 100
6. World Pray Online (WPO), Call Centre ya maombi masaa 24, siku 7 za wiki.

NB: Ikumbukwe waliokuwa wanasali hizo Morning & Evening Glory wengi hawakuwa waumini wa KKKT bali wa madhehebu mengine na Waislam kuondoka kwake Dkt Kimaro tutarajie mabadiliko kiasi.

***Mchungaji Kiongozi (Mpya) Anna apewe ushirikiano kuendeleza alipoishia Dkt Kimaro.


Ngoma ikivuma sana hupasuka.
 
Wanasahau kuwa kanisa sio jengo au hivyo vyama(madhehebu) ambavyo vinapewa usajili kama kama vingine tu.Mimi sio Mlutheri lakini nimeabudu pale mara nyingi mno sababu ya moto tu uliopo kiroho.Ttatizo watu wamekazana kujenga falme za dini na madhehebu yao badala ya kujenga KANISA LA KRISTO ambalo haliangalii dhehebu ila kumuamini Yesu kama Bwana na Mwokozi.Mwisho uko karib sana

Huwezi kuleta taratibu zako ndani ya kanisa nankulazimisha zifutwe. Tuwe wa kweli. Kimaro akafungue kanisa lake Basi.
 
Hakuna alichokosea?. Kuwaita KKKT kanisa la madalali na Katoliki kanisa la kweli?. Ukweli ndio Nini? Kesi za ufiraji zipo kanisa gani? Tuache kutetea mambo kisa kasema Fulani. Huyo alitakiwa kufukuzwa kabisa aende huko Katoliki.
Kwenye ufiraji kunahusiana nini na Kanisa? ufiraji ni tabia ya mtu binafsi usichanganye mambo mawili kwa pamoja.
 
Safi sana Kimaro!

Kwapiga kwenye mshono! Yani mlitaka aondoke pale usharikani kimyakimya bila kusema?
Simfahamu,sijawahi kumuona zaidi ya kumsoma hapa.... Nachangia tu kama wengine humu......
 
Tumsubiri huyo Mchungaji Msaidizi kama ataweza kuendesha hizo projects (maana nina uhakika pesa ilikua inatoka kwa waumini ambao wamestuka kwa Dkt Kimaro kupewa likizo na kuhamishwa Kijitonyama.

Ataweza Sana na atafanya makubwa. Maana sio mtu wa mapicha picha.
 
Aondoke tu akafungue kanisa lake. Kwanza Kimaro sio mchungaji per se ni motivational speaker. Mjungaji huwezi kusema vijana wa dini Fulani sio waaminifu. Umefanya research wapi? Mchungaji alitakiwa awaite vijana awafundishe uaminifu.
Acha kufundisha watu unafiki ww. Mnapenda mtu anaye sugur-coat uovu ili iweje.
 
Kabisa mwaya! [emoji848][emoji848]

Tulishapasahau miaka mingi tangu enzi za ile kwaya ya wakongo ya wimbo hakuna Mungu kama wewe Kijitonyama ilikuwa kama haipo,

Usharika huo umekuja kujulikana baada ya Pastor Kimaro kuja huo ndio ukweli.

Hivi huyo Anna anazani ataweza kutembelea nyota ya Kimaro kweli ?

Acheni hizo. Kijitonyama ilikuwepo na itaendelea kuwepo. Kimaro aliikuta na ameiacha.
 
Mnanishangaza sana.
Hata Yesu aliwasifu mafarisayo kwa kuwatolea mfano wanafunzi wake kuwa;
" Haki yenu isipozidi haki ya mafarisayo kamwe hamtauona ufalme wa Mungu"

Hapo kuwasifia waislanu katika eneo wanalofanya vizuri kuna tatizo?

Nimegundua Wakristo wengi ni zero katika ufahamu wa neno la Mungu.

Wewe ndio ziro kabisa. Mfano wa Yesu mbona ni tofauti na Kimaro?. Mchungaji unadai vijana wa kikikristo wote sio waaminifu. Kisa umeibiwa na vijana wako wa kanisani kwako?

Alitakiwa kuaanda semina ya kufundisha vijana kuhusu uamnifu na sio kutoa kauli ya jumla kwa vijjana wote. Yule sio mchungaji ni motivational speaker
 
ukitenda mazuri kwa wanadamu chukizo kwa
wanadamu tena
Chukizo gani, kuna ubaya gani akipelekwa mahali pengine kusambaza neema kama hizo. Yeye ni mchungaji anayeweza kufanya kazi popote pale. Acheni umbeya.
 
Back
Top Bottom