Tujikumbushe, projects kadhaa ambazo Mchungaji Dkt. Kimaro amezifanya akiwa Mchungaji Kiongozi, KKKT Usharika wa Kijitonyama,
1. School of Healing (Morning & Evening Glory) -Youtube Channel (mwanzoni ikiwa Eliona Kimaro TV baadae KKKT Usharika wa Kijtonyama) inayowafikia watu wote Duniani.
2. TAMASHA LA MBINGU KUJAA SIFA (kila mwaka)
3. Jengo jipya la Sunday School (lililogharimu yapata takribani 200m TZS)
4. Ununuzi wa Kiwanja pembezoni mwa kanisa yapata 300m TZS
5. Kusomesha yatima yapata 100
6. World Pray Online (WPO), Call Centre ya maombi masaa 24, siku 7 za wiki.
NB: Ikumbukwe waliokuwa wanasali hizo Morning & Evening Glory wengi hawakuwa waumini wa KKKT bali wa madhehebu mengine na Waislam kuondoka kwake Dkt Kimaro tutarajie mabadiliko kiasi.
***Mchungaji Kiongozi (Mpya) Anna apewe ushirikiano kuendeleza alipoishia Dkt Kimaro.
Mungu ambariki sana Mtumishi wake kwa kutumia vizuri kipawa alichopewa.Nadhani muda wake hapo ulikuwa umeisha,kazi yake ilikuwa imeshakamilika.Sasa itakuwa ameitiwa sehemu nyingine. Pengine labda huko Maneromango,Mkuranga, au Zanzibar na kwingineko ambako kuna hitaji wabunifu kama yeye ili kulijenga na kuliinua kanisa la Bwana.
Tusisaha, kila mahali ulipo kama ikiwa unareport kwa mtu mwingine(yaani unaye bosi) na kabla yako kulikuwa na mtu mwingine.Ujue hapo unapita tuu.atakuja mwingine.Dr.Kimaro alilijua hili kwa sababu hakuanzia huduma hapo,kuna mahali alitoka.Huko atakaoenda atakuta pia kazi walizozifanya walio mtangulia,kama ambavyo Mch.Ana amekuta kazi za Mch.Dr.Kimaro na walio mtangulia.
Uzuri mmoja wa watumishi wa KKKT,wakifika mahali wanasimamiaga maendeleo ya hapo as if watakuwa hapo milele.Hawanaga ubinafsi ule wa nawezaje kufanya maendeleo hivi wakati sina uhakina na kama nitakaa muda gani hapa.
Kile wanachofanya baadhi ya waumini cha kuendelea kuongelea vibaya maamuzi yaliyoganywa na mamlaka iliyojuu yake,ni kuendelea kumfarakanisha Mch Dr.Kimaro na hiyo mamlaka .Ni kumvika roho ya ujeuri,kiburi na majivuno na kuua kabisa roho ya unyenyekevu,hekima utilivu,uvumilivu na utu wema.Yaani wanambebesha lawama kwamba hao wanaofanya hivyo amewatuma yeye(Ingawa mimi binafsi siamini hivyo).Hasa ukichukulia wote walionekana wanaandamana ni wachaga.
Yeye mwenyewe Mch.Dr.Kimaro alisema wazi ametii mamlaka yake atafanya hivyo kama alivyotakiwa kufanya.
Mzee Jakaya Kikwete(kama ,sijakosea) aliwahi kusema,kiongozi bora na mkomavu utamjua pale linapotokea jambo gumu la kumtikisa.Aliyebora atakuwa mtulivu sana (Very calm) .Ila kiongozi wa hovyo likitokea jambo gumu litamvuruga na atakurupuka vibaya