Gwajima anamtuhumu Mh. Rais Samia kuwa amehongwa hela ili kukubali chanjo,huyu amevuka mipaka ashughulikiwe.
 
Zipo taasisi/kampuni zitaweka sera ya kuchanja wafanyakazi wao wote kwa lazima. Najua serikali wanasoma maoni yetu, utolewe muongozo utaosimamia raia wake juu ya uhuru/hiari kushiriki hizi chanjo.

Twende na hili swala kwa akili!
Uzuri ruhusa ya kuhamia burundi tayari ipo.
 
Tanzania siyo nchi ya kwanza kuchanjwa. Nchi nyingi tu wameshachanjwa kwa zaidi ya miezi 5 sasa .... Kudai kuwa tusibali kufanyiwa majaribibio huo ni upotoshaji wa hali ya juu .... Nchi karibia zote walishapokea chanjo na sisi mpaka sasa ni katu ya nchi cheche ambazo hazijapokea. Nchi kama South Africa tu kuna watu zaidi ya million 5 tayari wameshachanjwa, Mauritius wamechanja zaidi ya 60 % ya watu wao, Seychelles almost every adult ....!!
 
Naunga mkono hoja,
P
 
Upo sahihi kabisa, cha ajabu serikal haita ongea kitu
Zipo taasisi/kampuni zitaweka sera ya kuchanja wafanyakazi wao wote kwa lazima. Najua serikali wanasoma maoni yetu, utolewe muongozo utaosimamia raia wake juu ya uhuru/hiari kushiriki hizi chanjo.

Twende na hili swala kwa akili!
 
Mwizi wa kura anapata wapi moral authority ya kumzungumzia Yesu na mambo ya wokovu? Hiki ni kituko cha karne.
Siyo tu mwizi, mtu aliyeshiriki ujambazi wa kura alafu kusema YESU NDIO KAMSHINDIA.
 
Ni jambo la ajabu sana nchi ipo kwenye mapambano dhid ya Covid,

Serikali inajitahd kutoa elimu kwa Raia halafu anakuja mpumbavu mmoja ambaye hajawai hata kutengeneza panadol anapotosha umma kwa tafiti zake za kipumbavu.

Huyu mtu anaachwa hivi hivi? tunapiga hatua mbele anakuja mjinga mmoja kuturudisha nyuma kwa sifa zake?

Aliwai kufanya tafiti za Afya? ni mwanasayansi? ni daktari?

Huyu mpaka mda huu angekua ameshavuliwa uanachama,

Halafu na ww mama ukiwa mpole sana matokeo yake ndio haya, serikali inasema hv mjinga mmoja anaelekeza vile

oke
 
Alishasema bungeni so karudia tena mlifukuza wapinzani mkadhani mkiwa wenyewe ndio mtaongea lugha moja?? Acha aseme ukwelimbona Nchi waiochanja bado wanaugua?
 
1.Kanisa lake lifungwe kwa upotoshaji.

2. Avuliwe uanachama wa CCM kwa kupiga kampeni ya kupingana na Mwenyekiti wake.
 
Hii ni hoja au ndo ngebe zenyewe? Suala la afya ni la mtu binafsi na ndo maana Mh.rais alisema chanjo ni hiari.
Na mimi nimemsikiliza Gwajima anasema mama kafanya maamuzi mazuri ili wanaotaka kuchanjwa wapate haki yao na wasiotaka wasilazimishwe.Sasa kama wewe unataka kuchanjwa si uende ukachanjwe? shida yako ni nini si chanjo tayari ipo nchini?
 
CCM haipangwi na inaheshimu Uhuru wa kuongea(freedom of speech).Muda huu mngekuwa mmejikita kupata barua ya Afisa mtendaji wa Kata husika Kwa ajili ya kumtoa Abubakar sero.
 
Gwajiboy aligombea ujumbe wa NEC mama na kamati yake wakamuona hatoshi wakampiga panga. Hiki kitu kilimuuma sana Gwajiboy.

Sasa hivi anatumia chanjo kummaliza mama kisiasa. Ajenda ya Gwajiboy sio kupinga chanjo ila ni kummaliza mama kisiasa.
Mama awe makini. Gwaji atatumia chanjo na ukabila kummaliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…