Ni jambo la kukera sana pale viongozi wanapolazimisha watu kufuata mikumbo bila kutumia akili. Ama ni kuwafanya kwamba watu hao hawana haki, au uwezo wa kufikiri na ama kujibinafsisha nafsi za watu wengine ambalo ni kosa kwa Mungu. Kibaya zaidini ile picha ya wapiga debe wa ccm wa mitandaoni ambao ni dhahiri elimu zao ni za chini, wanapolazimisha watu wafuate mikumbo, na hata kuzuiliwa kutoa maoni boreshi kwa maslahi ya taifa na ama mtu binafsi . Angalieni hapa, Gwajima kawapiga bao!, Mnasemaje? Na hawa nao hawana akili ila ninyi tu? Hizo chanjo mmezitengeneza ninyi hadi mpoteze kodi za Watanzania kujadili Gwajima kumtafutia makosa kwa sababu hoja anazoziongea hamwezi kuzitolea majibu? Mtu mzima akivuliwa nguo huchutama.
Dunia nzima iko na Gwajima. Mnaweka wapi nyuso zenu?